Mzalendo wa kweli ni mtu mwenye uwezo wa kufikiria hadi kizazi cha saba (7th Generation) Mtu asiye mbinafsi na mwenye mawazo endelevu. Kwa wanasisa walio wengi hapa nchini wanajifikiria wao na familia zao tu na huo ndio mwanzo wa migogoro mingi ndani ya vyama vya siasa.
Mfano, Uundwaji wa katiba mpya ni kitu ambacho ni muhimu sio tu kwetu lakini pia kwa manufaa ya vizazi vijavyo, lakini kwa wanasiasa wengi ndani ya chama tawala wanahofia mslahi yao binafsi na hivyo kuudhoofisha mchakato wote wa uundwaji wa katiba.