Ni nani mzalendo na nani Mpinzani wa kweli? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni nani mzalendo na nani Mpinzani wa kweli?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kalunguine, Jan 13, 2012.

 1. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #1
  Jan 13, 2012
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Ni nani mpinzani wa Kweli na Nani Mzalendo wa Kweli nchini Tanzania?

  Wimbi la kuvurugana kwenye vyama vya upinzani bado linaendelea kuvitesa vyama hapa nchini!

  Kina David Kafulila kufukuzwa, Hamad naye huko CUF vivyo hivyo hadi unajiuliza maswali mengi tu kama vile je hawa walifanya makusudi ama kwa kurubununiwa na kutumwa ili wadhoofishe upinzani kwa kisingizio cha kutoa siri za vyama vyao? Au ni watu kama kina Mbat** wanaosemwa ni NCCM ndio wanafanya kazi waliotumwa?

  Huko CHADEMA nako sitashangaa kusikia baadhi ya viongozi wa juu huenda wana ajenda za siri kuhusu upinzani na mustakabali wake - na wengine wametuhumiwa hivyo

  Frankly ukweli wa uzalendo na wa upinzani unabakia siri yako wewe moyo wako kama una uchungu na nchi yako na hatima ya wanyonge wa Tanzania inaendelea kuwekwa rehani kwa unafikli na maslahi binafsi ya wengi wetu ambao ni wasaliti!
   
 2. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #2
  Jan 13, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  wazalendo tupoila tumefunikwa mbaya,usicheze na njaa.
  wewe ni mgeni tanzania nini?
   
 3. Secretary General

  Secretary General Member

  #3
  Jan 13, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mzalendo wa kweli ni mtu mwenye uwezo wa kufikiria hadi kizazi cha saba (7th Generation) Mtu asiye mbinafsi na mwenye mawazo endelevu. Kwa wanasisa walio wengi hapa nchini wanajifikiria wao na familia zao tu na huo ndio mwanzo wa migogoro mingi ndani ya vyama vya siasa.
  Mfano, Uundwaji wa katiba mpya ni kitu ambacho ni muhimu sio tu kwetu lakini pia kwa manufaa ya vizazi vijavyo, lakini kwa wanasiasa wengi ndani ya chama tawala wanahofia mslahi yao binafsi na hivyo kuudhoofisha mchakato wote wa uundwaji wa katiba.
   
 4. Gwalihenzi

  Gwalihenzi JF-Expert Member

  #4
  Jan 13, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 5,117
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Tangu lini maskini, mjinga na mwenye njaa akawa mzalendo?
   
Loading...