Ni nani mmiliki wa mimba?

kALEnga kidamali

JF-Expert Member
Nov 19, 2015
491
1,000
Wakuu,

Mama anapotaka kutoa mimba, baba humwambia, "Tafadhali usitoe mimba yangu!"

Baada ya mtoto kuzaliwa na kukua, naye anasema, "Nisingekuwa hai hii leo kama si baba kumzuia mama kutoa mimba yangu!"

Baba anasema "Mimba yangu" na mtoto anasema "Mimba yangu".

Hivi mimba huwa ni ya nani?

Chukua na mfano huu: Mama akishika ujauzito, humfuata mwanaume wake na kumwambia, "Nina mimba yako", lakini mama huyohuyo akishajifungua, kuna siku utamkuta akisema, "Nilipokuwa nimebeba mimba ya mwanangu wa kwanza niliumwa sana."

Hebu wana Jf tusaidiane hapo, mimba huwa ni ya nani?.... Mimi bado niko njia panda..
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom