Ni nani ‘Master mind’ wa Rais Magufuli? Mwambieni watanzania hawataki vurugu

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,224
3,290
Uongozi ni dhamana. Dhamana ni Kuchunga ahadi ya utii wa taratibu na sheria ili kuongoza jamii ilioyokubaliana juu ya jambo fulani.

Tanzania ina Katiba , sheria, kanuni, Miongozo na UTAMADUNI. Utamaduni ulikuwepo , ulitangulia na kukaziwa na Katiba na sheria ili uendelee kudumu. Miongoni mwa Ustaarabu wa watanzania ni kuishi kwa amani, kuheshimiana na kusaidiana.

Tokea kuingia awamu ya tano, huu ustaarabu umeanza kumongonyoka. Upo ushahidi wa kimazingira kutumika kwa taasisi za kimamlaka kuvuruga taratibu, miongozo na Desturi zetu kwa kuruhusu milengo na visasi kuamua. Taasisi zinazotajwa na kuhusishwa si tu Mahkama, Bunge na Polisi bali na taasisi nyengine za Serikali kwa kubambikia watu kesi mbali mbali na kuleta taharuki.

Yamepita mengi tokea kunyimwa HAKI ZA kisiasa, Uonevu wa watuhumiwa wa kesi mbali mbali kuwekwa ndani bila kufuata taratibu, maagizo ya kimahakama kutotekelezwa n.k. Hili ni vurugu limeruhusiwa ndani ya awamu ya tano. Kwa nini kuwe na uthubutu wa kukemewa japo kwa maneno wala rushwa lakini wasikemewe japo kwa kinafiki wavunja sheria na Haki za watu, wapotezaji watu na wauaji?

Nchi sasa inaelekea kwenye Chaguzi muhimu. Hapa Afrika chaguzi ni vyanzo vya vurugu na mauaji, tayari kumeanza chokochoko kwenye kuelekea Chaguzi za serikali ya Mitaa. Vurugu zilianza kwa kutokuwekwa bayana ratiba na sasa kuna kuunga unga taratibu. Watanzania hawajui nini hasa kinakusudiwa kwenye hili?

Kuna Choko choko na majaribio ya Rais kutaka kuongezewa muda ingawa Mwenyewe amekanusha. Hawa wapambe ni nani na nani anawapa nguvu? Alianza Mkamia sasa Mkulima. Tena mkulima kaenda Mahkamani. Hapa kuna nia gani ? Jee Mahkama yetu inaaminika kiasi gani isije ikawa ndio inataka kupiga muhuri wa MOTO. Watanzania hawataki hizi vurugu.

Leo nimesikia Vyombo vya Ulinzi vinaandaliwa kupiga kura siku moja kabla ya Uchaguzi Mkuu kunani tena kama si Vurugu zinaandaliwa kwenye huu Utawala wa Magufuli. Nani Mshauri wa haya Mambo?

Watanzania waachwe wapambane na ugumu wa kutafuta riziki, wasilazimishwe kufanya mengine. Utamaduni wetu haukubali haya mambo.

Kama kuna nia njema kwa nini utawala haukukubali kuletwa Katiba mpya? na sasa kunafanyika ujanja wa kutaka kuleta vurugu zisizo maana?

Yamepita mengi, watu wana makovu na visasi tele moyoni,.
Naombeni tusiijaribu amani yetu kwa kuangalia madaraka ya mpito.

Huyu master Mind wa Rais Magufuli ni nani? Mwambieni watanzania hawataki vurugu.

Kishada.
 
Mkuu umenena vyema sana. Maana wasijetupeleka shimoni.

What if the mastermind ni yeye mwenyewe ?
what if the mastermind anapenda vurugu?
what if the mastermind hayuko stable in thinking?
what if ...
what if..

Mkuu If ni nyingi kwa kweli na zinafikirisha.
 
Kuna mtu hataki kuonekana dictator pekee yake katika ukanda huu. Analazimisha na kushauri vibaya kiongozi wetu ili waonekane kama ni wengi ndani EA. Ndo maana unaona kila kitu ni copy and paste
Kwani sisi hatuna Dira yetu? Hao waioko jikoni ni nani? kiasi cha kuruhusu Miiko kuchezewa? Lazima kuna tatizo mahali.

Watanzania hawataki vurugu.
 
Wenye Wajibu wasiruhusu na kufanya Makosa yatakayokuja kuigharimu nchi miaka mingi. Kiukweli awamu hii imepanda sumu mbaya sana ya kutoheshimiwa Haki za watu kuanzia za faragha hadi za kuishi. Tofauti za mawazo zipo kikatiba kwa nini leo zinaambatanishwa na uhujumu Uchumi , kukosa Uzalendo au uhaini? Hizi lugha zinatumika kuhalalisha kuwatia watu hatiani kweenye hii awamu ya Tano.

#Watanzania hawataki Vurugu
 
Magufuli kisiasa ni zimwi nyonya damu lilokuja kuvuruga hii nchi ole wenu watanzania mukiendelea kumchekea kiama chenu hakitakuwa na kiasi vizazi na vizazi asiruhusiwe kuvuruga umoja wa nchi huyo anayejiita kichaa
Mtanyooka tu labda mrudi kuzimu mlikotoka..
 
Wenye Wajibu wasiruhusu na kufanya Makosa yatakayokuja kuigharimu nchi miaka mingi. Kiukweli awamu hii imepanda sumu mbaya sana ya kutoheshimiwa Haki za watu kuanzia za faragha hadi za kuishi. Tofauti za mawazo zipo kikatiba kwa nini leo zinaambatanishwa na uhujumu Uchumi , kukosa Uzalendo au uhaini? Hizi lugha zinatumika kuhalalisha kuwatia watu hatiani kweenye hii awamu ya Tano.

#Watanzania hawataki Vurugu
Sumu ilishapandwa siku nyingi kinachofanyika ni kutoa hiyo sumu ndiyo maana ya kelele hizo unapiga, tiba ya ugonjwa wowote mara zote si rahisi kumeza, usilaumu tiba laumu kwa nini uliruhusu malazi!
 
Back
Top Bottom