Nkobe
JF-Expert Member
- Feb 17, 2013
- 2,230
- 3,333
Hawa jamaa nimekuwa nikiwafuatilia siku nyingi.
Huko Iraq wamekuwa ndio kimbilio la watu walio wachache, wanyonge ambao wanakimbia kuchinjwa na ISIS.
Naona jamii ya watu wa Yazid na Wakristu wachache wamekuwa wakikimbilia maeneo ya Wakurdi ili kunusuru roho zao.
Jana katika taarifa ya BBC swahili nimeona wanapambana na ISIS katika milima ya Sinjar ili kuwaokoa watu jamii ya Yazid waliokimbilia huko kwa siku kadhaa kwa hofu ya kuchinjwa.
Pia inaonekana wako msitari wa mbele kuokoa Iraq nzima zidi ya ISIS. Najiuliza, mbona hawa jamaa wana roho ya kipekee kiasi kwamba hata wanawake nao wamejitolea kupigana jeshini, kuna mwanamke wa Kikrudi yuko vitani mpaka leo kwa miezi kadhaa na amekuwa maarufu duniani.
Ni akina nani hawa Wakurdi, hao nao wamejaliwa akili kama Wayahudi? au Wana asili ya Kiyahudi?