Hizo zilikuwa enzi ambazo Nchi yetu ilikuwa nchi. Dawa ilikuwa kuwashughulikia walioiba sio kuyaua. Sasa hivi tuko hoi wakati wageni wanafaidi nchi yetu. Watanzania kibao hawana kazi, maana yaliajiri sana. Sijui tutafanyaje kujikwamua. Nyerere hakukosea aliposema njia kuu za uchumi zitamilikiwa na Watanzania. Alikataa wazungu wasichimbe madini kwa mikataba yao mibovu akasema ntasubiri watanzania wasome watachimba wenyewe. Kinyume chake watanzania wanaambulia mashimo na umaskini.