Ni nani aliyefadhili ujenzi wa Uwanja wa michezo wa JAKAYA KIKWETE kidongo chekundu , DSM ?

Ilitakiwa ujengwe Uwanja wa Simba na Jk akamwita Rage ( akiwa Rais wa Simba wakati huo) akubaliane na Masharti ya Jamaa hao wa Sunderland ambao pia ni Wabia wa Symbion lakin kwa Sharti ya Nembo yao yenye Rangi ya Njano iwe inavaliwa na Simba Muda wote Rage akakataa kwa Maelekezo kuwa Simba wangempindua akikubali hilo la kuvaa Nembo ya Njano ndipo jk akaona kuliko kukosa hiyo Offer bora wakajenge Kile Kituo.

Na Ilichaguliwa Simba ndio wajengewe kwa kuwa kabla ya kuwa Simba ilikuwa inaitwa Sunderland Miaka hiyo ya nyuma sana

Hayo yakisemwa na Jk mwenyewe Siku ya Ufunguzi
 
Asante mkuu , kumbe ujenzi wake ulifanyika kitambo namna hiyo ?
Ujenzi umekamilika mwaka.juzi na kikwete kabla ya kuondoka madarakani aliufungua.... nadhani umefunguliwa september 2015.

ni uwanja uliojengwa na Mwekezaji kampuni ya kufua umeme ya symbion power. Uwanja umekabidhiwa serikali lakini Operations and Maintenance wanafanya Symbion Power.

Ni uwanja wenye viwango vya fifa, mtanzania yoyote anaruhusiwa kwenda kufanya mazoezi pale bure kabisa. Japo kuna taratibu maalum za kujisajiri pale getini.

Kama ni taasisi au shule pia wanapaswa kupeleka maombi na kupangiwa ratiba ya kufanya mazoezi au hata kucheza mechi bure kabisa.
 
Back
Top Bottom