Ni muda sasa wa wanasiasa kuwepo Frontiers kwenye maandamano

Mpunilevel

JF-Expert Member
Sep 14, 2015
3,140
1,871
Nimekua nikifuatilia maandamano mbali mbali yanayofanyika sehemu mbali mbali duniani, afrika mashariki na hapa nchini mwetu.
Mara nyingi lengo la maandamano hayo huwa ni kufikisha ujumbe sehemu husika. Nini hakipendezi jamii. Au pongezi kwa jambo flani.

Nataka nijikite hapa nchini mwetu kuhusu maandamano mbali mbali yanayofanyika siku zilizopita na pengine yajayo kwani ni muhimu inapobidi. Ila yawe ya amani na si ya uvunjifu wa amani.
Kama kichwa cha makala kinavyojieleza. Kwanini mara nyingi waasisi wa maandamano hawajumuiki na wafuasi wao mstari wa mbele kufikisha ujumbe sehemu husika.
Mara nyingi tunaona wafuasi bila viongozi wao. Hua wanaogopa nini? Kua na wafuasi wao pamoja.
Kisheria hairusiwi kujumuika?

Au ndo wafuasi ni chambo? Na ngazi ya kufikia malengo flani?

Naomba Michango yenu wadau.
 
Imagine Lowassa aongoze maandamano......yataitwa maandamano ya kobe
 
Wanatakiwa kuwepo mstari was mbele kwenye maandamano wanayopanga ili kusudi washirikiane kufikisha ujumbe mfano uhaba wa sukari na bei kubwa.
 
Acha hao wanaotumia vichwa vyao kutenganishia masikio pekee ndiyo watangulizwe.

Ukiwaambia tu,"Hakuna dhambi mbaya kama uoga". basi wewe rudi nyumbani ukasubirie taarifa ya habari saa mbili kusikia wangapi wamevunjwa miguu maanake maandamano mengine hata kibali huwa hayana.

Division of labor,acha mazuzu wawe fursa.
 
Mbona Mgaya na Mukoba walitangulia wakati wa maandamano ya Mei Mosi, au we unamaanisha haya maandamano yanayoandaliwa na UVCCM na unataka wamtangulize Kinena na Nepi?
 
Mbona Mgaya na Mukoba walitangulia wakati wa maandamano ya Mei Mosi, au we unamaanisha haya maandamano yanayoandaliwa na UVCCM na unataka wamtangulize Kinena na Nepi?
Hapana ni yale yanayoandaliwa na bavicha. Atangulizwe mboe na Tundu lissu.
 
Back
Top Bottom