Ni muda muafaka sasa iPhone waombe msaada kwa Tecno watengenezewe betri imara

Ni muda muafaka sasa iPhone waombe msaada kwa Tecno watengenezewe betri imara

LICHADI

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2015
Posts
4,727
Reaction score
13,466
Kama kuna kitu kinawaangusha Apple Inc katika bidhaa zao basi sio kitu kingine ni Battery za devices zao tofauti kutokukaa na chaji kwa muda mrefu, yaani ukimkuta mtumiaji wa iphone basi pembeni ni lazima atakuwa na power bank.

Ila upande wa Tecno japo upande wa software wanatuangusha lakini kwenye betri wapo vizuri sana, Betri zao huwa zinadumu sana na chaji huwezi mkuta mtumiaji wa tecno anatembea na mipower bank. Ni muda sasa Apple waombe hata ujuzi kwa Tecno awatengenezee betri maana simu zao ni nzuri kwenye software lakini kwenye betri wanachemka kila kukicha.

Nafikiria kuiuza iphone yangu ni heri nihamie Xiaomi au Huawei maana nao wapo vizuri, suala la betri linachosha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kweli Tecno sio simu yaani kigezo cha betri is very minor problem kuliko namna tecno zinavyo stuck plus many hallucinations mtoa uzi unatumia iPhone gani aseeee
 
Hapa niko na tecno jana inaniambia storage imejaa na sms siwezi kupokea kwa sababu zimejaa nashangaa nimefuta sms zote hamna kitu.

Nimefuta app nyingi bado majanga nikaona kesi hii vipi,nimerestore saivi ahueni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tumia simu ya mahitaji yako, sio kwa ajili ya trend au fashion

If it isn’t perfect ,it’s not good enough
 
Sidhani kama iphone hawana uwezo huo, ila tatizo simu zao zina vitu vingi mno na uendeshaji wa simu unaotumia power zaidi ya Tecno.

Tecno zinakaa na chaji kwa kuwa utofauti wake na simu za button ni ile touch screen na mfumo wa android😁😁😁😁
 
mimi na run 3 small business via insta.. per day najibu dm, napost, whatsapp sms na mengineyo mengi.. natumia tecno f2 ya laki na 30 na inamudu... ila nina wadogo zangu mabinti wana i phone 6 plus zao.. wanaomba vocha kila siku kwangu.. nikiwaambia wahamie tecno hela zingine waweke vocha wanasema blaza mkoloni na mshamba...
 
[QUOTE="FRESHMAN,

Kaka ni kweli unayosema ama unafurahisha genge!!! Sijaona alieku support hapa, hujaji shtukia?
 
Kaka ni kweli unayosema ama unafurahisha genge!!! Sijaona alieku support hapa, hujaji shtukia??

nikidanganya napata faida gani? watu hawapendi ukweli mchungu.. nina vitu vingi sana vya thamani zaidi ya simu.. na hata kununua simu sio kitu cha kuwaza kwangu... mimi nanunua kitu kutokana na kazi inayoweza kufanywa na hiko kitu, tangu naanza maisha nilisema siwezi nunua simu laki 5 au milioni moja huku nafua kwa mkono gheto kwangu wakati bei ya mashine ya kufua ni hiyo hiyo

hizi link za page za biashara zangu ndogo ndogo zichunguze vizuri ukadirie kwa siku nahudumia watu wangapi.. na natumia tecno f 2 ya laki na 30 tu

1. https://www.instagram.com/tshirt_garage_mabibo_hostel/

2. https://www.instagram.com/photo_studio_mabibo_hostel/

3. https://www.instagram.com/dobi_sinza_vunja_bei/
 
mimi na run 3 small business via insta.. per day najibu dm, napost, whatsapp sms na mengineyo mengi.. natumia tecno f2 ya laki na 30 na inamudu... ila nina wadogo zangu mabinti wana i phone 6 plus zao.. wanaomba vocha kila siku kwangu.. nikiwaambia wahamie tecno hela zingine waweke vocha wanasema blaza mkoloni na mshamba...
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]ndo hoja yenu hiii.kuna mmoja alitaja mpaka kipato anachopata kwa mwezi,af anakwambia na anatumia tekno P5 na anadunda safii tuuu.Ila mke wake ndo anatumia iphone.Mwenyewe ndo akajiona bingwaaa kama wewe hapo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]ndo hoja yenu hiii.kuna mmoja alitaja mpaka kipato anachopata kwa mwezi,af anakwambia na anatumia tekno P5 na anadunda safii tuuu.Ila mke wake ndo anatumia iphone.Mwenyewe ndo akajiona bingwaaa kama wewe hapo.

Sent using Jamii Forums mobile app

wapo wengi tu wana simu za laki 8 ila wanafua nguo kwa mikono , wanagombania madala dala, wengine za milioni ila wanapoishi anaona aibu kukukaribisha..

maisha ni muhimu kujua vipaumbele,,,, mimi namuelewa mtu mwenye simu ya gharama kwa ajiri ya kuingiza pesa.. ila sio kwa ajili ya kushangaa instagram, au whatsapp tu.. why usinunue low cost smart phone.. mimi biashara nazorun zinafanyika hata na tecno ya laki moja.. so why ninunue simu ya laki 5...

nilishaacha huo ujinga zamani.. nanunua kitu kutokana na mahitaji ya lazima

angalia nguvu ya tecno ya laki moja tu





 
Nani kakwambia tecno wanatengeneza betri
 
Zaidi ya 90% ya iphone hapa bongo ni iphone 6, simu za mwaka 2015 ambazo bei ni sawa na tecno spark 4
 
Kama kuna kitu kinawaangusha Apple Inc katika bidhaa zao basi sio kitu kingine ni Battery za devices zao tofauti kutokukaa na chaji kwa muda mrefu, yaani ukimkuta mtumiaji wa iphone basi pembeni ni lazima atakuwa na power bank.

Ila upande wa Tecno japo upande wa software wanatuangusha lakini kwenye betri wapo vizuri sana, Betri zao huwa zinadumu sana na chaji huwezi mkuta mtumiaji wa tecno anatembea na mipower bank. Ni muda sasa Apple waombe hata ujuzi kwa Tecno awatengenezee betri maana simu zao ni nzuri kwenye software lakini kwenye betri wanachemka kila kukicha.

Nafikiria kuiuza iphone yangu ni heri nihamie Xiaomi au Huawei maana nao wapo vizuri, suala la betri linachosha.

Sent using Jamii Forums mobile app

iPhone refurbished ndo zinaisha chaji na ndo asilimia kubwa watu wanazo wao wanadhani ni mpya, zimejaa kkoo na kijitonyama na maeneo mengine ya nchi , hizi tunazoita full box

. Ukichukua iPhone mpya toka apple store utabadili haya uliyoandika.
 
Back
Top Bottom