Simu za iphone kwa hili litaleta kelele sasa, hairuhusiwi kutumia fundi asiesajiliwa

High Vampire

JF-Expert Member
Nov 17, 2012
2,915
2,131
Watumiaji wa simu za iPhone 6 (walio pakua iOS mpya) ambao walitengeneza simu zao kupitia mafundi ambao hawajaandikishwa na Apple wamepatwa na hali ya sintofahamu baada ya simu zao kufungiwa baada ya update ya OS hiyo.

Simu hizi ambazo zimegundulika zilitengenezwa na mafundi wasio sajiliwa na kampuni hii zimefungiwa na zinaonesha Error 53 hakuna unachoweza kufanya hata kama utataka kurudi katika OS ya zamani pia hilo hutaweza.

Error 53
Kiufundi ni kwamba unapofanya update ya software ya iPhone 6 basi inafikia mahali hii OS mpya inaichunguza simu kama kuna kifaa ambacho sio kutoka kwa mafundi wake walio sajiliwa kufanya matengenezo ya simu hizo ambazo zina gharama kubwa.

Mtandao wa the Guardian wa huko Uingereza unaripoti kwamba watumiaji wa simu za iPhone 6 ambao kwa namna moja au nyingine walifanya matengenezo ya simu zao ambayo yalihusisha kubadilisha baadhi ya vifaa na kuwekewa vifaa ambavyo sio vile vilivyothibitishwa basi wamekutana na kadhia hii.

Baada ya ripoti hii kuchapishwa na jarida hilo, Apple walitoa statement kusema kwamba wanachukulia usalama wa watumiaji wao kuwa ni kitu muhimu na kwamba Error 53 imewekwa ili kuhakikisha kwamba vifaa vya home button vinaendana na vifaa vingine ndani ya simu yako na pia ni vile ambavyo ni halali.

Taarifa kutoka Apple inawataka watumiaji ambao wanakumbana na kadhia hiyo kuwasiliana na huduma kwa wateja wa Apple kwa msaada zaidi.

Tayari kuna makundi yanafikiria kuishtaki Apple
Fikiria umenunua gari kutoka Toyota na ikasumbua ukaenda kwa fundi wako wa bei rahisi na akarekebisha labda kwa kubadili kifaa kama vile alternator. Baada ya muda Toyota wakigundua hilo wazuie gari lako kufanya kazi kabisa kisa tuu hujatumia huduma zao ambazo huwa ni za bei ya juu….hili suala halileti maana.

Na inaonekana kama mashitaki hayo yakifika mahakamani basi kuna uwezekano mkubwa Apple watakutwa na hatia kisheria.

Error 53 itakuwa ni sababu nyingine kwa watumiaji wa kipato cha chini huku Afrika mashariki kuzikimbia simu hizi kwani pindi zinapo pata matatizo ni gharama sana kutengeneza ukilinganisha na simu za Android ambazo mafundi wake wapo wengi sana mitaani.

Na kwa wale ambao wanamiliki simu za iPhone 6 na wanajua kwamba walifanya matengenezo kwa mafundi wa mtaani basi ni busara kukwepa kufanya update ya OS ya simu maana inaweza ikakugharimu.
 
Hawa Apple ni wndawazi, yaani ukinunua Simu yao tu, wewe ushakuwa wanakumiliki hunamaamuzi tena, lazima ufanye watakavyo wao kwenye simu yako mwenyewe.
nimeishia kucheka tu....

nipo na Note yangu hapa nakula raha za smart kwa uhuru woooteeee
 
ndo maana sinaga kabisa hata wazo la kununua iphone, mambo ya ku update os kila mara yalinishinda. pole yenu kwa watumiaji wa iphone, lakin naamin kama umeweza kununua iphone 6 bas utaweza kumudu garama za matengenezo, labda kama ulinunua kwa kufuata mkumbo, akat hela yako ya kuungaunga. we ndo itakula kwako.
 
Apple sio kwa watu masikini masikini wa kipato
Apple wanamelenga wateja wanaojiweza tu na ndio maana wana product moja tu ya simu yaanj high end

Sasa wale wenzangu na mimi simu ikiharibika unakimbilia spea za kichina apple wamesema big no, maana mavifaa haya yaneweza kutumika kubypass security za apple

Usiwalaumu apple laumu uwezo wetu mdogo
 
Apple sio kwa watu masikini masikini wa kipato
Apple wanamelenga wateja wanaojiweza tu na ndio maana wana product moja tu ya simu yaanj high end

Sasa wale wenzangu na mimi simu ikiharibika unakimbilia spea za kichina apple wamesema big no, maana mavifaa haya yaneweza kutumika kubypass security za apple

Usiwalaumu apple laumu uwezo wetu mdogo

Kwa hiyo sasa tusinunue? We unacheza na sisi wabongo kwa kupenda sifa tutanunua tu hata km ni kuchezea game
 
iphone-error-53.png
 
Kwa hiyo sasa tusinunue? We unacheza na sisi wabongo kwa kupenda sifa tutanunua tu hata km ni kuchezea game
Hapana mkuu sijamaanisha hivyo
Namaanisha ukinunua bidhaa za Apple usiwe na hela ya mawazo maana utashindwa kui maintain ikikorofisha
Sasa unaambiwa hiyo buton ikiharibika apple wanatoza dola 200 na ukiweka ya mchina imekula kwaki mazima

Bora ukanunua kimeo cha adroid kwa dola 200 utapata cha maana tu
 
Back
Top Bottom