ManiTek TV
JF-Expert Member
- Jun 3, 2011
- 410
- 159
[h=1][/h]
[TABLE="class: tr-caption-container"]
[TR]
[TD]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption"]Umbile la Kubuni la iPhone 6[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
iPhone 6 kwa sasa ndio gumzo la ulimwengu wa simu. Tetesi zimepamba moto juu ya iPhone 6 baada ya karibu kampuni zote kubwa kutangaza simu zao vinara (Flagship Phone) kwa mwaka 2014, ingawa wiki chache zijazo simu kinara ya kampuni ya Life is Good (LG), ambayo inatarajiwa kuitwa LG G3 inategemewa kutangazwa ikiwa imeambatana na saa yake (Fitness band)
Wakati habari za Ulimwengu wa gajeti zimeelekea kueneza tetesi kwa kutabiri na kudanganya juu ya muonekano wa iPhone 6, huu ni wakati muafaka kwa sisi katika Gajetek kuchukua fursa hii kueleza mambo muhimu matano ambayo yataifanya iPhone 6 iwe simu itakayotamba kwa mwaka 2014. Tutayapanga mambo hayo kwa umuhimu kuanzia namba 5 kwenda namba moja:
5. Near Field Communication (NFC)
Hili ni moja kati ya mambo mengi ambayo iOS imeachwa nyuma na Android, ndio kusema kuwa watumiaji wa Android hii ni teknolojia ambayo wameanza kuitumia karibu miaka mitatu nyuma. Wakati teknolojia hii bado ipo njia panda huku ikitumiwa katika mambo machache kama vile kuunganisha na spika zisizo na waya na kufanya malipo madogo madogo kwa Google Wallet au Samsung Wallet, tunaamini ubunifu wa Apple na umaarufu wa iPhone unaweza kuleta mabadiliko makubwa juu ya jinsi watumiaji wa simu wanavyoitumia teknolojia hii.
4. iOS 8
Huu ni mwaka ambao Apple wanahitaji kufanya mabadiliko makubwa katika OS ya iPhone, iPad, iPod Touch na Apple TV. Apple wanahitaji kuwa na muelekeo wa kuingiza mambo yote muhimu ambayo Android kwa sasa imeshatekeleza bila kuonekana kuiga, na hasa katika suala la customisation. Lakini pia wateja wa Apple siku zote hutegemea mambo mapya kabisa katika bidhaa mpya. Kwa miaka ya karibuni Apple wamekuwa wakileta uchache wa features mpya katika iOS, hivyo ili Apple kuweza kuendelea kuwa namba mbili katika mauzo ya Smartphone Duniani hawana budi kufanya mapinduzi makubwa katika iOS 8, mapinduzi ambayo yatadumisha mauzo kwa miaka miwili watakapokuwa wanatoa iPhone 6S mwakani.
3. Saa (Smartwatch na Fitness band)
[TABLE="class: tr-caption-container"]
[TR]
[TD="align: center"]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"]iWatch ya kubuni ambayo inaonekana kufuata umbile na Fuelband[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Wengi wameshaipa jina la iWatch, saa hii itakayoambatana na iPhone 6 ni gajeti muhimu kwa kuifanya simu hiyo kuwa kivutio kwa wateja kwa vile saa zinazotumika na iPhone kama Nike Fuelband SE na Pebble Steele zina mapungufu mengi ukilinganisha na Simu za Gear zilizotolewa na Samsung. Mathalan Fuelband ina mambo yanayohusiana na mazoezi tu na haina mambo ya smartwatch na Pebble Steele ni smartwatch ambayo haifanyi vizuri katika masuala ya kiafya na mazoezi na pia ina skrini ya hali ya chini isiyo na mguso (touch screen)
Saa za Gear zote tatu za Samsung zilizotoka mwaka huu zinajumusha kazi zote mbili, za kiafya na smart features kama vile kupata taarifa (notification) na hata kupokea simu huku sikiwa na skrini ya hali ya juu ya aina ya Super Amoled, na Gear Fit ikiwa na umbile la kuvutia kwa vile skrini yake inapinda kufuata mzunguko wa mkono. Hili ni eneo ambalo Apple hawana budi kuingia wenyewe badala ya kuachia kampuni nyingine kuwatengenezea saa sa iPhone. Vile vile wakati Google wanatarajiwa kutangaza Android ya Saa kwenye kwenye mkutano wa Google I/O, hali itazidi kuwa ngumu kwa iPhone iwapo hawatatoa smartwatch mwaka huu.
2. Betri
Mara zote Apple wana utamaduni wa kuvifanya vifaa vyao kuwa vyembamba zaidi hata kuongoza soko katika sifa hii; gajeti kama vile iPad Air, Macbook Air na iMac ya 2013 ni ushahidi wa hili, hata hivyo kwetu sisi kuna umuhimu mkubwa wa kuboresha uhai wa betri walau kufikia mtumiaji wa hali ya juu kutumia simu bila kuhitaji kurudia kuichaji kabla ya mwisho wa siku ya kawaida, hata kama hili litapelekea iPhone kuwa nene kidogo hadi kufikia inchi 8. Tunazungumzia kuwa nene kidogo kwa sababu ni ukweli usiopingika katika ulimwengu wa leo kwamba teknolojia ya betri iliyopo inahitaji betri kuwa kubwa zaidi ili kuwa na nguvu ya kudumu muda mrefu, mpaka hapo patakapofanyika ugunduzi mwengine katika namna betri ya simu inavyodumu zaidi, wakati wa kutoa iPhone Air haukufika.
1. Ukubwa wa Skrini
Hili ni jambo muhimu kuliko yote. Ni matarajio yetu kuwa Apple watatoa simu yenye skrini yenye ukubwa wa kiasi cha inchi 5. Kwa sasa skrini ya iPhone 5S ambayo ina ukubwa wa inchi 4 ni kichekesho hasa ikizingatia kuwa ni ndogo kuliko matoleo mini ya simu vinara za kampuni nyingine, hapa tunazungumzia simu kama vile HTC One mini na Samsung Galaxy S4 Mini ambazo zote zina skrini ya ukubwa wa 4.3, Apple kungangania falsafa ya simu kunaweza kukamatika na kutumika kwa mkono mmoja ni kujichimbia kaburi kwani utafiti umeonyesha kwamba wengi miongoni mwa wanunuzi wa Samsung Galaxy S5 ni watumiaji wa iPhone. Hivyo watu wataendelea kuihama iPhone bila ya badiliko hili muhimu.
Jibu la nini kitakuwemo kwenye iPhone 6 linatarajiwa kutoka mwezi wa 9 au wa 10 mwaka huu. Hata hivyo mkutano wa WWDC 2014 ambao umeshtangazwa na utaanza tarehe 2 ya mwezi Juni utatoa mwangaza juu ya muelekeo wa Apple kwenye Smartwatch na iPhone 6. Wakati ugunduzi na Apple ni jambo la kawaida, huu ni wakati ambao Apple wanahitaji kugundua ili kuilinda hadhi ya kampuni yao na kuimarisha biashara yao kwa upande wa simu.
Chanzo: gajetek habari
[TABLE="class: tr-caption-container"]
[TR]
[TD]
[/TD][/TR]