Ni muda gani mtoto anastahili kupata Elimu bora?

Ni muda gani mtoto anastahili kupata Elimu bora?

Nickman

Member
Joined
Jun 23, 2014
Posts
80
Reaction score
11
Naleta kwenu huu mjadala ili tujadili kwa pamoja.

Kumekuwa na shida ya wazazi kusomesha watoto kwenye shule za gharama kubwa sana wakiwa na umri mdogo. Lakini je, ni wakati gani mtoto anatakiwa kupata msingi wa elimu? Na kumgharimu mzazi?

1.Kindergarden

2. Nursery

3.Primary

4.Secondary

5.College/University?

Naomba maoni yetu.
 
Mtoto anatakiwa kupata elimu bora akiwa bado hajajitambua vyema, namaanisha vidudu na primary kama mzazi ana uwezo. Hapo ndo aweza kumpa msingi mzuri wa elimu.

Mzazi anaweza kumpeleka shule ya ghrama kubwa mtoto wa nursery na primary, akifikia secondary anakuwa ameshapata msingi mzuri, hata akikumbwa na dhoruba la foolish-age anakuwa na msingi mzur.

Ahueni ikipatikana katika dhoruba la foolish-age anaendelea na ujenzi wa taaluma yake vyema mpaka chuo kikuu! Lakini usipomjengea msingi wa awali, foolish age ikimkumba harudi tena ndo inakuwa ndo bye bye!
 
Ni vizuri mtoto akapata elimu nzuri kuanzia Chekechea. Lakini elimu iliyo muhimu zaidi na kuwa nayo makini zaidi ni elimu ya msingi.Ngumu saana mtu aliyepata elimu ya msingi hafifu akaweza kufanikiwa huko mbele ( nammaanisha kielimu).

Ukiangalia mfumo wa elemu ya msingi utakuta kuwa kwa upande wa sekondari ni yaleyale sanasana yanapanuliwa zaidi. Labda nitoe mfano wa somo la Hesabu ambalo nililisomea tangu msingi mpaka elimu ya juu.

It is almost impossible kumiss ya msingi na kuweza kufanikiwa ya juu. Kwani Hesabu huenda zikijijenga. Ili uweze kujua kuzidisha, inatakiwa kwanza ujue kujumlisha. Ili uweze kujua hesabu za fraction inatakiwa ujue kujumlisha, kutoa kugawanya na kuzidisha, sasa endapo mtoto hakuelewa principals ya hizo nyingine itamuwia vigumu kufanya hesabu za fraction.

Mwalimu Nyerere aliona mbali alikazania sana elimu ya msingi na mtu alipomaliza shule ya msingi alikuwa na elimu katika masomo yote aliyosoma na hata aliweza kuya-apply.

Mfano mdogo tu nadhani wa Sayansi nakumbuka tulifundishwa kuwa katika hewa ujazo wa kawaida kuna Oxygen nadhani 1 ya 5. Sasa unapowafungia watoto kwenye gari bila kukumbuka Oxygen iliyopo humo ndani ni constant sijui unategemea nini. Na elimu hii tulijifunza shule ya msingi.

Pamoja na kusema hayo simaaninishi mtu aishie shule ya msingi tu bali nilikuwa naonyesha jinsi elimu ya msingi ilivyo muhimu. Mengine ya msingi nakumbuka jinsi mimea inavyopumua/ inavyotoa hewa - tofauti ya mchana na usiku. Yote hayo shule ya msingi. Huko mbele unajifunza zaidi ikiwa pamoja na kufanya kwa vitendo.

Hivyo ni muhimu kama wazazi kuhakikisha kuwa mtoto anapata the best primary education, itakuwa rahisi kwake secondary na kuendelea. Vingenevyo itamgharimu sana mtoto kufanya kazi ya ziada na mzazi kulipia gharama nyingi za hizi zinazoitwa tuition ili aweze kumake it huko mbele ya safari yake ya elimu.
 
Mtoto anatakiwa kufundishwa vizuri tokea akiwa amezaliwa. Malezi bora kwanza afu ndio elimu ifate. Elimu bora ni kuanzia pale anapoanza kukifunza iwe nursery au primary kama ndo ataanzia.

Hii itamsaidia sana kujielewa na kufahamu. Hawa wengi wa shule za kata wao hawajielewi sababu elimu waliyoipata toka wakiwa wadogo ni elimu finyu hivyo kufanya akili zao kuwa finyu pia.
 
Mleta mada... uimara wa nyumba unaanzia wapi???

Usilete mada za kukwepa majukumu, peleka mtoto shule nzuri kwenye msingi. Ningeshukru kama ungekuja na mkakati ni jinsi gani tujadili hizi shule za msingi wapunguze ADA maana ndio janga kuu la kitaifa, lakini watoto lazima wapate msingi kuanzia kuzaliwa..!
 
Mtoto anatakiwa kufundishwa vizuri tokea akiwa amezaliwa. Malezi bora kwanza afu ndio elimu ifate. Elimu bora ni kuanzia pale anapoanza kukifunza iwe nursery au primary kama ndo ataanzia.

Hii itamsaidia sana kujielewa na kufahamu. Hawa wengi wa shule za kata wao hawajielewi sababu elimu waliyoipata toka wakiwa wadogo ni elimu finyu hivyo kufanya akili zao kuwa finyu pia.
Umemaliza mkuu.
 
kuanzia baby class na kuendelea, ni uwezo wako tu
 
Back
Top Bottom