Nini muarobaini wa wizi wa mali za umma nchini?

VYEMELO

JF-Expert Member
Jul 21, 2020
348
459
Ndugu wana JF, nawasalimia ktk jina la Jamhuri ya Muungano!

Nianze mada yangu kwa kutoa masikitiko yangu, kwamba, JF imeanza kupoteza sura yake ya awali na lengo la kuanzishwa kwake, bila shaka.

Hazijadiliwi tena mada zenye maslahi mapana kwa Taifa letu na badala yake mambo mengi yanayojadiliwa humu yanaonesha ni jinsi gani, haiyumkiniki, watu walivyokata tamaa, na au, hawajali, au hawajui mambo mbalimbali yanayoendelea nchini.

JF ni majukwaa ya kijamii yaliyoanzishwa kukutanisha Watanzania pamoja kwa majadiliano juu ya uchumi, siasa, jamii, na mambo mengine yanayoathiri maisha yetu Watanzania.

Hali hii inatutesa sana tulioanza na JF na tulio na umri wa makamu kuelekea 70s. Tunajiuliza, ... Hawa vijana wetu wa kizazi hiki wanakwenda wapi? Future yao ikoje? Vijana wasiojua kutetea maslahi yao.

Vijana wanaoonekana wamekata tamaa isivyo haki na wameweka kama vile rehani maisha yao yawe determined na 'wajanja' wachache. Sijui kama ni kutojielewa au Ni kukata tamaa.

Vijana wa Kitanzania, amkeni kwani hatma ya ndoto za maisha yenu imo mikononi mwenu!

Nimalizie kwa kusashirikisha mada kuntu hiyo hapo juu. Tuijadili na kutoa ushauri kwa wahusika lipi lifanyike kama dawa ya kudhibiti hali hii isiyofaa ya wizi uliokithiri wa mali za umma hususani fedha za umma.

Hali ni mbaya. Wizi huu umekithiri hasa kwa Watumishi wa sekta ya umma, yaani, Serikalini. Watu tuliowaamini, kimsingi, tukawaajiri watuhudumie; wametugeuka! Matokeo ni mabaya sana:
  • Hali ya maisha imepanda. Maisha mtaani hayaeleweki.
  • Watanzania wanakufa kwa kukosa madawa na huduma stahiki za matibabu.
  • Kuongezeka kwa vifo vitokanavyo na ajali, vifo ambavyo kiuhalisia kwa teknolojia ya sasa hivi duniani, ajali hizi zingeweza kuzuilika kirahisi tu. Ajali za barabarani, majini, anga, na kadhalika.
  • Biashara za watu zinaporomoka kila kukicha, yaani, unaanzisha biashara kwa lengo ikue na kutajirika, badala
ya biashara isonge mbele, Inaporomoka tena kwa kasi ya 4G!

Orodha ni ndefu.

Mambo haya yamefikia hatua hadi wabunge kuvunja ukimya pamoja na 'uchawa' wao kwa chama-dola na Serikali.

Kwa kweli siyo Sekta ya umma pekee, hata Sekta binafsi ni kupigwa tuu! Si unaona hizi bundles za Internet na muda wa maongezi?

Haya vijana, karibuni kwa mjadala wenye tija!
 
Tatizo si vijana tu hata wazee, maana nyie ndio mmetangulia kwenye hii mifumo na vijana tume ikuta.
 
Back
Top Bottom