Ni mimi nazeeka au mziki mzuri unapotea !?

TheChoji

JF-Expert Member
Apr 14, 2009
4,974
15,310
Mimi sio mtaalamu wa muziki. Ila mimi ni mpenzi wa muziki kuanzia zilipendwa, RnB, Bongo Fleva, na hata Bolingo. Nimejaribu kuangalia muziki unavyokwenda naona kama kadri siku zinavyoenda na mziki unazidi kuzorota sio tuu hapa Tanzania, bali sehemu nyingi duniani. Imefikia wakati siku hizi ni nadra sana kusikia wimbo mzuri ukakusisimua.. Tatizo ni nini?
Mfano mimi nimekua miaka ya 90. Enzi hizo mimi nakua kulikua kuna miziki mingi sana mizuri ambayo hadi leo hii ikipigwa watu wanaikubali. Pia kulikua na wasanii wakali kweli kweli ambao sijaona mimi mtu wa kumfananisha nao kwa sasa. Kwa maneno mengine, sijaona mwanamziki sasa hivi anaeweza kutoa albamu ikanishawishi kununua..!
Kwa mfano tukiangalia mziki wa nje.. Miaka ya 1990 mpaka miaka ya 2005 kulikua na vipaji hatari kwenye RnB na Hip Hop mamtoni. RnB walikuepo kina R. Kelly, Joe Thomas, Tyrese, Toni Braxton, Brandy, BabyFace, KCI & JOJO, Celine Dion, Mariah Carey, Boyz 2 Men, Blackstreet, Westlife, Enrique Iglesias, Whitney Houston, Alicia Keys, Usher Raymond, Marc Anthony na wengine..
Hip Hop kulikua na kina 2Pac, Biggie, Nas, PDiddy, Fabulous, JaRule, DMX, Busta Rhymes, Xzibit, Snoop, Dre, Eminem, Fat Joe, Lil Kim, Da Brat,.. Na wengine wengi sana ambao kiukweli leo hii ukiniambia kuna mwanamuziki wa levo hizo nakataa.
Hata ukijaribu kuangalia muziki wa Congo wa miaka hiyo tajwa utakubaliana na mimi kwamba vipaji kama vya kina Pepe Kale, Madilu, Kanda Bongo Man, Yondo Sister, Koffi Olomide, Wenge Musica, Xtra Musica, Defao, Tabuley, Mbilia Bell n.k huwezi kuvipata kwa sasa.
Tukija hapa Tanzania hali ni hivyo hivyo.. Kuna wakati hapa ilikua ni shughuli maana kila msanii alikua mzuri na alikua anatoa nyimbo kali..! Sasa hivi siuoni kabisa ule ushindani na ubora wa enzi za kina Sugu, Afande Sele, Wanaume TMK, Sir Nature, Prof J, Daz Nundaz, Solo Thang, Stara Thomas, Banana Zorro, n.k.
Sasa ndio najiuliza.. ni kwamba siku hizi nyimbo nzuri hamna au mimi ndio nimezeeka kwahiyo sizioni hizo nyimbo za sasa kama ni nzuri..? Maana hata nikienda club bado naona nyimbo za miaka ya 2000 kurudi nyuma zinashangiliwa saana tofauti na za sasa..!
 
Hakuna muziki siku hizi mkuu, we natafuta shughuli nyingine ufanye, au endelea na zilipendwa.
 
zaman mziki ulikua ni kipaji,saiz umekua ni kazi ko mtu akipata mtaji tu wa kurekod anatoa wimbo na video hapo ndo keshakua msanii.mengine atakua anajifunzia mbele ya safari,ndo mana wanaigana style,wanaibiana nyimbo nk,by the way wachache wapo wapo japo nao wanaathirika na soko linavyoenda ko wanachange ili nao washibe
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom