Ni migomo kila mahali.......silaha ya mwisho ya mnyonge.............. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni migomo kila mahali.......silaha ya mwisho ya mnyonge..............

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Rutashubanyuma, Feb 2, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Feb 2, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 417,643
  Trophy Points: 280
  Chuo Kikuu cha SMMUCo waingia katika mgomo


  na Rodrick Mushi, Moshi


  [​IMG] WIMBI la wanafunzi wa vyuo vikuu kuendelea kugoma limeendelea kushika kasi ambapo jana wanafunzi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Tumaini cha kumbukumbu ya Askofu Stefano tawi la Moshi mjini (SMMUCo) wamegoma kuingia darasani kwa muda wa siku mbili wakilalamikia kutopatiwa fedha za kujikimu toka Bodi ya Mikopo.
  Wakizungumza mbele ya Mkuu wa Chuo hicho, Arnold Temu, walisema wataendelea na mgomo wao hadi watakapohakikisha changamoto zilizopo chuoni hapo zinatatuliwa, ikiwemo tatizo la mawasiliano ya intaneti, ubovu wa miundombinu pamoja uhaba wa vitabu.
  Hata hivyo kutokana na mgomo huo unaoendelea, Jeshi la Polisi mkoani hapa lililazimika kuweka kambi ya muda kuzunguka chuo hicho ili kuzuia vurugu ambazo zingeweza kutokea.
  Walidai kuwa kuchelewa kukabidhiwa fedha zao kuna uwezekano wa uongozi wa chuo hicho kudiriki kutumia kiasi cha sh milioni 7 ambazo zinadaiwa kutoka bodi ya mikopo.
  Wanafunzi hao ambao walionekana wakiimba nyimbo za muasisi wa Taifi Hayati Mwalimu Julius Nyerere walisema kuwa mazingira ya chuo hicho yamekuwa mabovu kiasi cha kuhatarisha maisha ya wanafunzi hao.
  “Tumekuwa tukiwasilisha matatizo haya mara kwa mara katika uongozi lakini wamekuwa hawatusikilizi na hivyo tutaendelea kugoma na hatuna imani na serikali ya wanafunzi..tutapiga kura ya kutokuwa na imani nao,” walisema.
  Kutokana na mgomo huo wanafunzi wa mwaka wa kwanza na wa tatu walishindwa kufanya mitihani ambayo ilikuwa ikiendelea chuoni hapo


  [​IMG]

   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Feb 2, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 417,643
  Trophy Points: 280
  Waalimu wapya wagoma wakidai malipo ya mishahara


  na Ramadhani Siwayombe, Arusha


  [​IMG] WAALIMU wapya walioajiriwa mwaka jana katika manispaa ya Arusha jana waliandamana hadi katika ofisi za mkurugenzi wa manispaa hiyo wakidai malipo yao ya kujikimu ambayo hawajalipwa mpaka sasa.
  Walimu hao wakiwa wameshika mabango yaliyosomeka ‘serikali fedha za kulipa Dowans zipo, lakini posho za kujikimu walimu hakuna, huu ni ufisadi wa hali ya juu'; huku wakiapa kutoingia madarasani mpaka watakapolipwa fedha hizo kutokana na kuishi kwa shida toka wameanza kazi.
  Huku wakiimba nyimbo mbalimbali za kuhamasishana nje ya ofisi hizo walisema kuwa wanashangaa kutolipwa fedha zao za kujikimu za siku 124 mpaka leo wakati maeneo mengine wameishalipwa.
  "Sisi mpaka sasa hatujui tutaishi vipi, kutokana na madeni ya wenye nyumba wakati manispaa inafahamu kuwa sisi ni wageni katika maeneo ya kazi tuliyopangiwa," walieleza.
  Naye Mwalimu Andrew Paul wa Shule ya Sekondari Kaloleni, alisema kuwa wanasikitishwa na kitendo cha Manispaa kuwanyima posho zao ambazo wana uhakika hazina walishawatumia, ila zinabanwa tu kwa sababu za kiufisadi.
  Alisema kuwa waalimu wanaostahili kulipwa ni wale wa stashahada ambao wako zaidi ya 80 na wa shahada 89.
  Mkurugenzi wa Manispaa ya Arusha, Estomiah Chang'ah, alilazimika kutoka nje ya ofisi yake na kuwaomba walimu hao kukubali kupokea fedha nusu ya madai yao na nyingine wasubiri mpaka Hazina itakapoleta.
   
Loading...