mr mkiki
JF-Expert Member
- Sep 22, 2016
- 5,588
- 11,668
Ni miaka 50 sasa tangu kutangazwa kwa Azimio la Arusha. Siku kama ya leo 29/01/1967 Kamati Juu ya Chama cha TANU iliyoketi kwa siku tatu (26-29 Januari 1967) ilitoka na Azimio moja la kuasisiwa kwa UJAMAA nchini Tanzania.
Azimio lilikuja kuzinduliwa/Kutangazwa rasmi 05-02-1967 huko mjini Arusha na kupewa jina la "AZIMIO LA ARUSHA" baada ya kutangazwa rasmi katika mji huo wa kitalii nchini Tanzania!
Tunaweza kujadili kwa wiki nzima (29 Januari -05 Februari 2017) tunaweza kujadili kwa kuyatizamia maswali haya;
1. Je, kwa miaka 50 tunaweza kuliongeleaje azimio hilo lililoiweka Tanzania katika nchi yenye kujiendesha Kijamaa ?
2. Je, ilikuwa sahihi kwa nchi yetu kuingia kwenye UJAMAA kwa wakati ule ?
3. Kuna faida ambazo kama nchi tulizipata kutokana na kuingia kwenye mfumo wa KIJAMAA ?
4. Je, azimio la Arusha lilifanikiwa kama ilivyotarajiwa ? Na kama lilifanikiwa, lilifanikiwa kwa kiasi gani au halikufanikiwa kwa ilivyotarajiwa ?
5. Je, nchi yetu bado ipo kwenye mfumo huo wa KIJAMAA kama ilivyoainishwa kwenye ibara ya 3 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ? Na kama bado UJAMAA upo, je tunaishi katika UJAMAA ?
6. Je,tunahaja ya kuendelea nao (Kama upo/haupo ) mfumo huu wa Kijamaa ?