Ni matokeo yaliokisi kile watanzania wanakihitaji

Ni matokeo yaliokisi kile watanzania wanakihitaji

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
8,746
Reaction score
5,771
Watanzania sio wajinga hata kidogo,maana wanahitaji maendeleo. Maana bila maendeleo maisha yanakuwa magumu kwa kila mwananchi. Mfano kila mtanzania anakumbuka wakati taifa letu lilikuwa na barabara mbovu,mtu kutoka Dar es salaaam mpaka Mwanza aliweza kusafiri kwa siku tatu,na hii sio mbali sana ilikuwa ni miaka 1997 kurudi miaka ya nyuma. Hivyo kuna hatua kubwa tumepiga.

Kwa kile awamu ya tano imeweza kufanya kwa wananchi ni dhahiri kuwa ushindi kama huu ulistahili. Najua kuwa kila sekta imeguswa kwa muda mfupi sana. Afya, Elimu ,miundo mbinu ya barabara,reli anga na majini vyote vimeimarishwa. Na haya yote hayawezi kufanyika bila ya kuwabana wakwepa kodi na mafisadi ili serikali iwe na mapato.

Mfano mmoja vimejengwa vituo vya afya zaidi ya 499 kwa muda wa miaka minne na nusu. Je mama aliyekuwa anasafiri kilomita 40 kwenda kujifungua leo hii anasafiri km 5 angewanyima kura Ccm? Na ukitilia maanani waliambiwa waweke betri tatu ili tochi iwake na sasa wanataka iwake zaidi ya awamu ya kwanza!

Wapinzani ambao walikuwa wanakwenda kwa nchi za nje na kuandika barua taifa letu lisipate mikopo kwa ajili ya maendeleo ya taifa letu walitegemea kupata kura?

Wapinzani ambao walitaka tupate shida na mateso sababu ya janga la Covid -19 walitarajia kupata kura?

Tukae chini tutafakari watanzania wamefanya maamuzi sahihi. Sasa tochi ina betri tatu zinazofana. Kwa hiyo mwanga utaowaka ni mwanga wa nguvu ambao matunda yake tutayaona ndani ya miaka miwili.
 
Nima maanisha matokeo yaliyoakisi kile watanzania wanakitaka.
 
Back
Top Bottom