Ni mashine gani ambayo ukiipata itafungua njia zako za kibiashara?

Vijana mkiwa mnahitaji mashine za ku watoa zingatieni haya:

*Kodi ya Import duty
*Spare au vipuri vya machine
*Power consumption yake
*Production rate ukiliganisha na soko
*Technology na mafundi wa hizo machines.

Watu wengi wameimport machine ila zimewashida kitumia either gharama yake ya oparation iko juu au ni outdated Technology au kukosa spare zake,
nina machine moja GTO 52 ila fundi wake na msafirisha kutoka mbali kweli kweli.
Hili liliwahi kutukuta kwenye mashine ya kutengeneza ice cream au mabonge ya barafu,aisee ilikuwa inakamua umeme hatari,kwa siku inaweza kula umeme wa 10,000
 
Huu uzi bila kumpata kicheche wa kutupenyezea mizigo bandarini kwa nusu bei tutateseka Sana maana hapo alibaba au kwenye xampuni za China kitu kinakuwa ni laki kikufika bandarini ndo unachanganyikiwa kwa kodi
Sio kweli mashine hazitozwi kodi nyingi kama bidhaa zingine.
Kwasababu zinachukuliwa kama zina boost ukuaji wa viwanda.

Mashine hazitozwi import duty, zinatozwa railway levy, na vat na gharama zingine kwa uchache.

Niliwahi import machine fulani kutoka US na huo ndio mchanganuo niliopigiana hesabu na watu wa custom japo ilikua kwa ndege.

Kwa bandarini nadhani mawakala wanachukua pia percentage yao kwenye clearance.

Kwa wale wanaotumia cargo forwarders wakina gnm nadhani wanao gharama zao za usafiri zina cover process za clearance za mzigo wako pindi unapofika.

Kuna kitu cha muhimu sana
Kuna mdau Covax hapo juu kazungumzia, usikimbilie kununua mashine pasipo kujua upatikanaji wa spares na urahisi wa matengenezo, mashine zote zinahitaji maintenance mana vipuri huchoka na kuhitaji replacement, sasa ukienda kichwa kichwa umeagiza mashine biashara imechachamaa wateja wamekolea mashine inapata shida utajua hujui.

Cha mwisho mashine nyingi za mchina ni bei ya chini kwasababu wanaunda kwa kutumia vifaa hafifu, hii haina maana hawana vifaa imara isipokua wanapunguza gharama za uzalishaji ili waipate hiyo ela yako ndogo.

Mashine nzuri zipo ila ni gharama.
 
Machine za kutengeneza mkaa mbadala kwa kutumia taka zote za mimea mkihitaji kuona huo mkaa unavyowaka Tembelea hiyo page Instagram mtaona..
IMG_20220330_115007.jpg
View attachment 2247776

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom