Ni madhara yapi yatatokea kwa kuzuia Mahindi kutoka nje ya nchi mwaka huu 2020?

Alejandroz

JF-Expert Member
Feb 14, 2017
327
376
Habari wajasiliamali wenzangu,

Mimi ni mjasiliamali mdogo ambaye mwaka huu nilitaka nijikite katika kilimo cha mahindi pamoja kununua zao hilo.

Nimeshalima heka 5 na zinaendelea vizuri hadi sasa na nimeandaa bajeti kwaajili yakuongezea mahindi yakununua ili niyahifadhi kwa pamoja hadi bei itakapo kua yakuridhisha.

Lakini nimesikia kua Mh rais ametangaza kua mwaka huu 2020 mahindi yatazuiliwa kutoka nje ya nchi kwasababu ya uhaba wa chakula unaotazamiwa kutokea hapo baadae.

Kwakawaida hatua hii huwa inasababisha bei kuwa ya chini sana,, Nilikua naomba kujuzwa ni kwa jinsi gani kupungua hku kwa bei hutokea (hata kama ndani ya nchi kuna uhaba wa chakula) na pia nawezaje kuepuka au kupunguza madhara haya!

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom