Ni Maajabu Ambayo Hayajawahi Kutokea, Mwenye Mali Kujadiliana na Jambazi Kuweka Njia Nzuri za Kuzuia Ujambazi

Hamatan

JF-Expert Member
Nov 10, 2020
3,183
7,645
Taifa letu na sisi wananchi wake, tunaishi kwenye ndoto za kinadharia ambazo kihalisia, hazipo.

Watanzania wote, wawe wanaCCM, wapinzani na wasio na vyama, wenye uelewa na wakweli wa nafsi zao, wanajua kabisa kuwa mfumo wa utawala katika nchi yetu ni mbaya. Ni mfumo unaoenzi udikteta wa Rais.

Hata ile nadharia ya mihimili mitatu ni nadharia ya ndoto za mchana. Rais anateua Jaji Mkuu na Katibu Mkuu wa Bunge. Halafu kwa hadaa, tunaambiwa kuwa anayemteua na aliyeteuliwa, wapo sawa! Magufuli alikuwa mkweli aliposema kuwa yeye ni mhimili wenye mizizi mirefu kuliko mahakama na Bunge.

Mwalimu Nyerere aliwahi kukiri kuwa katiba yetu ni mbaya kwa sababu inamfanya Rais kuwa dikteta. Wananchi nao, kwa kupitia report ya Jaji Warioba, wakasema wanataka katiba mpya.

MASWALI MUHIMU:

1) Kama Baba wa Taifa, aliyeongoza kwa miaka mingi kuliko yeyote, alisema Katiba yetu inamfanya Rais kuwa dikteta, Samia, yeye anasemaje? Anafurahia kuwa Rais dikteta?

2) Kama wananchi walisema wanataka Katiba mpya, Rais Samia anafurahia kuwa kinyume cha matakwa ya wananchi? Kama anafurahia kuwa kinyume cha matakwa ya wananchi, ina maana ameamua kwa nguvu na ubabe, ameamua kuwatawala watu kwa namna anavyotaka yeye na siyo kwa namna ambayo wananchi wanataka waongozwe.

WATU WANASEMA WANAMWOMBA RAIS AFUFUE MCHAKATO WA KATIBA.

Maswali muhimu:

1) Hivi mnadhani Samia hajui kuwa katiba ya sasa ni ya kidikteta?

2) Anapotaka kuendelea kutumia katiba inayomfanya yeye kuwa dikteta, mnadhani anaudhiwa na mamlaka ya Urais wa kiditeta?

3) Hivi mnadhani katiba ya kidikteta inampa hasara gani Samia?

4) Tangu lini anayedhulumiwa akaondokana na kudhulumiwa kwa kutegemea hisani ya anayemdhulumu amwekee utaratibu wa yeye kutomdhulumu anayemdhulumu?

Someni historia, kisha jikumbusheni kanuni ya pili ya maendeleo:

THE LAW OPRESSION AND STRUGGLE OF THE OPPOSITE.

Samia na watu wake ni wanufaika wa katiba ya kidikteta, wananchi ndio wanaogandamizwa kutokana na katiba ya kidikteta. Wakati Samia anawagandamiza wananchi kutumia katiba ya kidikteta, ni lazima wanaogandamizwa wagome kugandamizwa, iwe kwa amani au shari, lakini kwa vyovyote lazima kuwe na struggle ya wanaogandamizwa kugoma kugandamizwa.

Kukaa na kuzidi kumwambia Samia, tunaomba uanzishe mchakato wa katiba mpya, ni kupoteza muda. Anayeonewa, anayegandamizwa, ni lazima apambane kukitafuta alichoporwa, japo si lazima iwe kwa panga au rungu. Mwalimu Nyerere alipambana, akaipatia Tanganyika uhuru, hakutumia bunduki, panga au rungu, lakini alipambana.

Nasi ni lazima nyakati zetu hizi tupambane kupata katiba mpya bora itakayowapa mamlaka wananchi, na siyo hii iliyopora mamlaka ya wananchi, na kuyaweka mikononi mwa Rais.
 
Kwa hiyo ulitaka wafanye nn hao wasio na mali

USSR
 
Hapa alikuwa ndio ametoka mchambawima hata kumechisha hajui. Leo anawapa watanganyika kesi za ugaidi ila magaidi wa kweli kina Sheikh Mselemu kawatoa.
2970761_Tutamtoa_Mkoloni_Mweusi_Soon_on_Instagram3A_E2809CMwenyekiti_wa_Chadema_Taifa_akisalim...jpg
 
Back
Top Bottom