Ni maadili ya viongozi au ya wananchi ndo imeporomoka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni maadili ya viongozi au ya wananchi ndo imeporomoka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zhule, Jan 26, 2010.

 1. Z

  Zhule JF-Expert Member

  #1
  Jan 26, 2010
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 354
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Maadili na nidhamu ya watumishi wa umma yameporomoka. Polisi na wanajeshi mara kadhaa wamekuwa ni majabazi.watumishi wa umma wanasaini mikataba mibovi mingi sina budi kuzitaja.Rais wa nchi amekosa heshima kwa wananchi anasema EPA ni wazito hawakamatiki kuhusu watatetemesha nchi, Richmond anasema hatua ya Lowasa na Mawaziri kujiuzulu ETI inatosha rais huyo anasema pia wezi wa EPA wamerudisha pesa na hakuna mahakama.Mifano ni mingi.Mara nyingi watu, viongozi mbali mbali si wanasiasa wala wa dini wakisema elimu ya maadili ianze kutolewa mashuleni(sekondari,ya msingi na vyuo). Kwa lugha nyepesi mabadiliko ya maadili yaanzie chini kwenda juu na siyo juu kwenda Chini. Hapa ndo nina dukuduku. Nadhani we are born inhuman, we become human through social interaction. kwa maana nyepesi ni kwamba tunakuwa hivi tulivyo kwasababu tunaiga, au tunajifunza kutoka kwa wenzetu. Yaani tunaishi kwa mifano ya watu tuliowakuta.watoto wetu wanajifunza kutoka kwetu. Tutawezaje kutengeneza elite family from nowhere?kwa nini watawala hawataki kubadilika ili tuwafundishe watoto kwamifano na si kinadharia? Kwa mfano kikwete akianza kuingia ofisini saa mbili kila siku Ikulu nzima itabidi waingie saa moja na nusu bila hata kuambiwa maake mtu atajioea aibu kama kila siku anamkuta mkuu wake amewahi. swali langu hapa ni maabadiliko ya maadili yaanzie mashuleni then wananchi then viongozi au viongozi ndo waongoze njia wananchi wafuatie then mashuleni ili tupate maendeleo kwa haraka?.
   
Loading...