Ni lini tuta tenganisha chama na serikali? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni lini tuta tenganisha chama na serikali?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MwanaFalsafa1, Jun 30, 2011.

 1. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #1
  Jun 30, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Tanzania ina tatizo kubwa sana la kutenganisha na kusambaza madaraka. Bunge limekua chombo cha kuridhia kila jambo linalo fanywa na serikali na kupitishwa na baraza la mawaziri. Wakuu wa mikoa na wilaya wana pokea maagizo yote toka juu. Ila leo haswa nataka kuzungumzia hili swala la chama na serikali kuwa kitu kimoja.

  Natambua kwa muda mrefu Tanzania ilikua nchi ya chama kimoja. Kwa maana hiyo chama ndiyo ilikua serikali na serikali ilikua ni chama. Kwa bahati mbaya hata baada ya vyama vya upinzani kutambulishwa hili halikubadilika na hili ilitokana na katiba kuto kubadilishwa bali kuwekewa viraka.

  Kuna mifano mingi ya kushindwa kwetu kutenganisha chama na serikali. Leo tunaona mali nyingi za serikali kutumika kwa shughuli za kichama. Kwa mfano vikao vya chama kufanyika ikulu, wafanyakazi wa serikali kutumika kwa ajili ya shughuli za chama, baadhi ya ofisi za serikali kama vile za mtaa kupeperusha bendera za chama na kikubwa ambacho nimeanza kuona siku hizi ni viongozi wa chama kuisemea na kuitetea serikali.

  Madhara ya hili tunaona leo ambapo hakuna chombo kinacho weza kuidhibiti serikali. Serikali imekua na nguvu nyingi kwa maana watu wanaoendesha serikali na wanaotakiwa kuikosoa serikali ni hao hao. Ni sawa sawa na kutegemea mtoto amseme vibaya baba, hilo ni nadra sana.

  Katika kipindi hichitunacho zungumzia katiba mpya nadhani ni muhimu pia tuzungumzie mfumo utakayo tenganisha chama na serikali. Nadhani hii ndiyo sababu kuu ya matatizo ya kiutendaji na kiuongozi tunaoona leo.

  Nawakilisha....
   
 2. T

  Technology JF-Expert Member

  #2
  Jun 30, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 733
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 60
  Siku Mrema akichukua nchi hii! Does it make sence to you!!! How this is possible... Well I didnt like your long sentences, you could have done it in three lines.
   
Loading...