Ni lini Mwl Salma Kikwete alitolewa katika Payroll ya Serikali (HAZINA)?

Suala hili kweli linataka majibu maana ni la msingi pia kwa watanzania kujua mke wa Rais wao ambaye alikuwa mwalimu na baada ya kuingia Ikulu tu ualimu ukaota mbawa na sasa ni Boss wa taasisi yake mweneyewe.
 
kwa taarifa yako JF ni zaidi ya wizara ya elimu au utumishi kama hujui kitu funga bakuli lako usijidai kuweka vinamba utadhani mleta mada kakuomba namba..
Nadhani Bwana/bibi minamba hajui kama JF uwanja wenye majibu ya kila kitu labda siri za watu mioyoni mwao!
 
Majibu ya maswali haya yatapatikana Nov 2015 baada ya kuwamwaga hawa manyang'au.
 
Nafikiri ni vizuri tukiyapata sasa hivi.

2015 wasipomwagika itakuwaje? Wanaweza wakawa wanang'ang'ania huku wanamwagika ikawa kazi ngumu kama kuukata mlenda unaomwagika toka bakulini.

Kama unajua tujuze basi.
 
Mbona hata viongozi wa cwt wanalipwa kwenye payroll hiyohiyo kwani wanafundisha?
Viongozi wa CWT wanafundisha na wanalipwa na serikali ispokuwa wale wa kuajiriwa kama Makatibu wa Wilaya, Mikoa na Katibu Mkuu pamoja na wahasibu (watendaji) Wenyeviti wanachaguliwa so wanaendelea na ajira zao na wakimaliza kipindi chao wanabaki walimu wa kawaida. Nenda pale Benjamin Mkapa High school ukathibitishe kama Gratian Mkoba hafundishi.

Back to the topic, kama Salma analipwa mshahara ni kosa la Mwajiri, yeye ndie anayemlipa mtumishi asiyekuwepo kazini ingawa kama Mke wa Rais alipaswa kuwajibika kutoa taarifa. Kiutaratibu alipaswa kuandika barua ya kuomba ruhusa isiyokuwa na malipo (Leave Without pay) au kuacha kazi kwa mujibu wa taratibu zilizopo.

Narudia alumiwe Mkurugenzi wa Halmshauri yake na Hazina ambao wanatoa mishahara hewa na Ofisi ya Celina Kombani (menejimenti ya Utumishi wa Umma).
 
Nilisikia ana likizo ya malipo kwa miaka kumi.
Likizo ya Malipo? Tena ya miaka 10? Never, hakuna kitu kama hicho. Likizo yenye malipo ni ugonjwa, likizo ya mwaka (siku 28), likizo ya dharura haizidi siku 14, likizo ya uzazi (maternity na Paternity leave-siku 84/3) likizo ya masomo (Study leave) na Sabbatical leave (miezi 12). Likizo ya zaidi ya hapo ni likizo bila malipo (leave Without pay) ambayo hutolewa na Katibu Mkuu Kiongozi kupitia kwa Katibu Mkuu Utumishi (Establishment). Kama ni miaka 10 itakuwa ni likizo bila Malipo
 
Mwaka 2008, juni niliwahi kuambiwa mtumishi wa Wizara ya Fedha kuwa Mwl Salma japokuwa si mtumishi wa Serikali lakini bado alikuwa anapokea mshahara toka Serikalini. Yaani mshahara ulikuwa unaingia katika account yake.

Miezi kadhaa baada ya walimu kuingia mgogoro na Serikali kupitia CWT, ulianza mkakati/zoezi la kuhakiki walimu hewa. Minong'ono iliendelea kuhusu Mwl Salma

Swali la msingi ni lini Mwl Salma aliondolewa/aliacha kulipwa na Serikali kama mwalimu (mtumishi wa serikali)?. Ikumbukwe alianza kuingia kwenye kampeni za Uchaguzi mkuu toka Septemba 2005.

MUHMU:Kama hujui lolote pita kimyakimya, wako wenye majibu ama dokezo/dondoo zitakazotupeleka kwenye majibu.

proceedure ni kwamba yule mama still ni mtumishi wa serikal na kwa circumstance kama yake ni kuwa likizo bila malipo mpaka siku ya kustaafu..hapo ndo anakuwa removed from payroll kwa kilipwa haki zake za utumishi kwa kipindi chote alichokuwa ndan ya kazi.sasa je hiki ndo kinachofanyika..mnaolijua hili vizuri inabidi muanzie hapa...
 
ni kosa la mwajiri wake.mwajiri wake ambaye ni halmashauri alipaswa kkumuandikia barua ya kutoonekana kazini na baadaye kusitisha mshahara wake.hata kama ni mimi nikiona mwajiri ananipa mshahara bila kufanya kazi nitakaa kimya.

Ni kweli kabisa kuwa kosa ni la mwajiri lakini hauoni kuwa mume wake ndio mwajiri mku hapa nchini? Kama kumbukumbu zangu ziko sawa, siku alipowataka Watanzania kuchanganya akili za Mgaya na zile zamtanzania mmoja mmoja, rais wetu alisema kuwa yeye ndiye mwajiri mku hapa nchini na hivyo basi, alipaswa kuliona hilo kuwa wapo wafanyakazi wake ambao wanakula mshahara bila kufanya kazi. Tena hili, angeliona mapema sana kwani naye annufaika nalo. Angepata kumuuliza kuwa mwenzangu hizi pesa unazoninunulia zawadi unazipata wapi na angepewa jibu la kazi anayoifanya wife wake.
 
  • Thanks
Reactions: SG8
Anayemlipa mshahara alipata Division 0 Zero kama Mulugo, nani kati ya hawa wawili atajaribu kukata mshahara wa Salma Kikwete maana wanaishi kwa huruma ya Kikwete mwenyewe
 
  • Thanks
Reactions: SG8
Viongozi wa CWT wanafundisha na wanalipwa na serikali ispokuwa wale wa kuajiriwa kama Makatibu wa Wilaya, Mikoa na Katibu Mkuu pamoja na wahasibu (watendaji) Wenyeviti wanachaguliwa so wanaendelea na ajira zao na wakimaliza kipindi chao wanabaki walimu wa kawaida. Nenda pale Benjamin Mkapa High school ukathibitishe kama Gratian Mkoba hafundishi.

Back to the topic, kama Salma analipwa mshahara ni kosa la Mwajiri, yeye ndie anayemlipa mtumishi asiyekuwepo kazini ingawa kama Mke wa Rais alipaswa kuwajibika kutoa taarifa. Kiutaratibu alipaswa kuandika barua ya kuomba ruhusa isiyokuwa na malipo (Leave Without pay) au kuacha kazi kwa mujibu wa taratibu zilizopo.

Narudia alumiwe Mkurugenzi wa Halmshauri yake na Hazina ambao wanatoa mishahara hewa na Ofisi ya Celina Kombani (menejimenti ya Utumishi wa Umma).

Kwahiyo mlolongo wa lawama uwe hivi:
1. Mwalimu Salma kwa kutofuata utaratibu ( huku akijua kwa hakika kuwa anakwenda kwenye shughuli za kisiasa katika ofisi kubwa nchini)
2. Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni (kutozingatia taratibu za ajira)
3. Wizara ya Fedha/HAZINA (kwa kuendelea kutoa mshahara hali jina la mpewa mshahara linajulikana si la mtumishi wa umma ikiwa pia wanayofursa ya kuhoji taarifa za mihusika)
4. Waziri wa Nchi Menejimenti ya Utumishi wa Umma ( kwa kutozifanyia kazi taarifa za uhakiki wa watumishihewa specifically kwa waalimu)

Wale wa Ofisi ya Komban tuambieni, jina la Mwl Salma lilikuja kwenu kama mfanyakazi hewa?
 
Likizo ya Malipo? Tena ya miaka 10? Never, hakuna kitu kama hicho.

Likizo yenye malipo ni:-
  • ugonjwa
  • likizo ya mwaka (siku 28)
  • likizo ya dharura haizidi siku 14
  • likizo ya uzazi (maternity na Paternity leave-siku 84/3)
  • likizo ya masomo (Study leave)
  • Sabbatical leave (miezi 12).
Likizo ya zaidi ya hapo ni likizo bila malipo (leave Without pay) ambayo hutolewa na Katibu Mkuu Kiongozi kupitia kwa Katibu Mkuu Utumishi (Establishment).

Kama ni miaka 10 itakuwa ni likizo bila Malipo

Kazi ni ile ile ila nimeinyambulisha tu.

Ufafanuzi wako ni makini.
 
  • Thanks
Reactions: SG8
Kwahiyo mlolongo wa lawama uwe hivi:
1. Mwalimu Salma kwa kutofuata utaratibu ( huku akijua kwa hakika kuwa anakwenda kwenye shughuli za kisiasa katika ofisi kubwa nchini)
2. Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni (kutozingatia taratibu za ajira)
3. Wizara ya Fedha/HAZINA (kwa kuendelea kutoa mshahara hali jina la mpewa mshahara linajulikana si la mtumishi wa umma ikiwa pia wanayofursa ya kuhoji taarifa za mihusika)
4. Waziri wa Nchi Menejimenti ya Utumishi wa Umma ( kwa kutozifanyia kazi taarifa za uhakiki wa watumishihewa specifically kwa waalimu)

Wale wa Ofisi ya Komban tuambieni, jina la Mwl Salma lilikuja kwenu kama mfanyakazi hewa?
Hakika wewe ni Mnyamahodzo (mwenye mawazo), lakini yenye akili. Kuchukua mshahara au malipo kwa kazi usiyofanya ni makosa kisheria na unaweza kushtakiwa na kufungwa au kulazimiak kulipa. Salma kama Mwajiriwa aliyeacha kazi anapaswa kuwa wa kwanza kuwajibishwa kama bado analipwa mshahara. Mambo yanayohusu Utumishi ni ya Mtumishi husika pamoja na Mwajiri wake, wote wawili wanawajibika. Ila kama ni kweli anaendelea kupokea hizo laki 3 za Ualimu basi nchi hii kuna wafanyakazi hewa wengi ingawa najua itakuwa ni kwa makusudi tu.
Kama Salma yupo Ikulu anapata mshahara je Mwalimu aliekuwa anafundisha Sodike, Ikangamwani, Itegelematwi,Soliwaya na Ikulimambo huko itakuwaje? Si hadi marehemu watakuwa bado wanalipwa? Ndifwaha veeeee!
 
Si Mwl Salma tu anayeendelea kulipwa mshahara hadi leo. Kuna Esther Sumaye, yeye wakati mumewe anachaguliwa kuwa WM alikuwa akifanya kazi Wizara ya Sheria, kutokana na protokali ilibidi asije kazini lakini hadi leo salary yake inaingia hadi leo.
 
Mwaka 2008, juni niliwahi kuambiwa mtumishi wa Wizara ya Fedha kuwa Mwl Salma japokuwa si mtumishi wa Serikali lakini bado alikuwa anapokea mshahara toka Serikalini. Yaani mshahara ulikuwa unaingia katika account yake.

Miezi kadhaa baada ya walimu kuingia mgogoro na Serikali kupitia CWT, ulianza mkakati/zoezi la kuhakiki walimu hewa. Minong'ono iliendelea kuhusu Mwl Salma

Swali la msingi ni lini Mwl Salma aliondolewa/aliacha kulipwa na Serikali kama mwalimu (mtumishi wa serikali)?. Ikumbukwe alianza kuingia kwenye kampeni za Uchaguzi mkuu toka Septemba 2005.

MUHMU:Kama hujui lolote pita kimyakimya, wako wenye majibu ama dokezo/dondoo zitakazotupeleka kwenye majibu.

Hivi ile DIPLOMA aliyokuwa akisoma huko chuo cha ualimu Morogoro alimaliza? Alifukuzwa au alisitisha?
 
Back
Top Bottom