Ni lini Mwl Salma Kikwete alitolewa katika Payroll ya Serikali (HAZINA)?

Huu ni uzembe wa utawala wetu kutokuwa makini katika mapato na matumizi ya nchi.
Wanafuatilia mambo madogo madogo na kuacha makubwa yanayoingizia taifa hasara.
 
Hivi ile DIPLOMA aliyokuwa akisoma huko chuo cha ualimu Morogoro alimaliza? Alifukuzwa au alisitisha?

Ilikuwa Certificate, haikuwa Diploma. Tetesi zinasema hakumaliza ila alipasishwa kumagumashi (kimjini-mjini).
 
Mwaka 2011 alifanya paper la form six, Hkl akapa A tatu yaani division 1 ya point 3. Mie najua hili tu.
 
Alikwisha wahi kuandika barua kwa mwajiri wake kuacha kazi?
Alikwisha wahi kuandika barua ya kuomba likizo bila malipo?

Kulingana na kanuni na taratibu za utumishi wa Umma kuna muda maalum ambao ukipita bila kutinga kazini na bila taarifa rasmi kuhusu wapi ulipo, unajifukuza kazi kwa hiyo mwajiri anakufuta kwenye payroll, sasa kama hakuandika barua ya kuacha au kuomba likizo bila malipo ambayo ni kwa muda wa mwaka mmoja tu, alikuwa mtoro kazini.
 
Kwani huyo jamaa alokupa taarifa toka Hazina kuwa bado analipwa mshahara keshafukuzwa kwa kuvujisha siri?
Kama yupo hebu rudi tena kamuulize kama hiyo payroll yaendelea kuingia au lah!!!
 
Atalipwa hadi akimaliza urais wa wanawake Tanzania..na hakuna wa kumfunga paka kengele!chezea visasi wewe?zamu ni yao sasa kama hutaki shauri yako ila ndio hivyo!

Mkuu Lambardi, nani ni paka katika muktadha ws maelezp yako?

Leo ndiyo najua kwa upya kuwa Salma ni Rais wa wanawake ndiyo maana aliwaambia kwa kidhungu wamemdisapoint.
 
Mimi nipo napiga chabo tu hapa jinsi magreter thinker mnavyo tiririka.
Ila kama majengo ya halmashauri yangeweza kusahini barua ya kutengua ajira hapo ingewezekena.
Embu wewe ungekuwa afisa elimu wilaya au mkoa ungefanyaje? Ungefuata taratibu na sheria za nchi?
Kuna maamuzi mengine ngumu kuyameza.
 
Achunguzwe haraka. Huu nao utakuwa ugaidi wa mali za umma. DPP andaa mashitaka kwa huyu mama/ mwalimu kama mi kweli amepokea mshahara tangu mumewe awe presidaa.
 
Kama ana elimu ya kidato cha nne muacheni apewe tu hako kaposho katamsaidia kuwawezesha wanachama wake kueneza ukimwi vyuoni
 
Mkifikiri huyu mama anahitaji mshahara wa mwalimu mnacheza.

Huyu mama ni mtu wa kuvuta kutoka benki kuu, mabilioni, kwa akaunti ya "Usalama wa Taifa".

Kama mshahara wa ualimu unaendelezwa ni uzembe tu. Si kwamba anauhitaji.

After all first ladies typically wanapewa kila kitu bure, na allowances nzito juu.
 
Mwaka 2008, juni niliwahi kuambiwa mtumishi wa Wizara ya Fedha kuwa Mwl Salma japokuwa si mtumishi wa Serikali lakini bado alikuwa anapokea mshahara toka Serikalini. Yaani mshahara ulikuwa unaingia katika account yake.

Miezi kadhaa baada ya walimu kuingia mgogoro na Serikali kupitia CWT, ulianza mkakati/zoezi la kuhakiki walimu hewa. Minong'ono iliendelea kuhusu Mwl Salma

Swali la msingi ni lini Mwl Salma aliondolewa/aliacha kulipwa na Serikali kama mwalimu (mtumishi wa serikali)?. Ikumbukwe alianza kuingia kwenye kampeni za Uchaguzi mkuu toka Septemba 2005.

MUHMU:Kama hujui lolote pita kimyakimya, wako wenye majibu ama dokezo/dondoo zitakazotupeleka kwenye majibu.

kimya !
 
Back
Top Bottom