Ni lini Dunia itashitukia ugaidi wa wamarekani?

Ni lini Dunia itashitukia ugaidi wa wamarekani?

Mzee2000

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2009
Posts
528
Reaction score
221
Habari inayolindima sasa hivi ni hili suala la wapiganaji wa Iraq wajulikanao kama ISIL. Ukiangalia historia ya ISIL utaona kwamba kama wamarekani wasingevamia Iraq 2003, ISIL isingekuwa kama ilivyo sasa hivi. Hebu tuangalie wamerakani wamesababisha vikundi vingapi vya ugaidi duniani.

1) Hamas- Miaka ile kulikuwa na machafuko kati ya Hamas na Fatah, wakati huo Hamas kilikuwa chama kidogo tu lakini Marekani ilisupport Hamas kwa kuipa silaha, mwisho wake sasa Hamas ni chama kikubwa cha ‘kigaidi’ kwa mujibu wa wamarekani.
2) Inajulikana Alqaeda ilipata misaada lukuku kutoka marekani wakati wanapikana na warusi.
3) Wamarekani waliua viongozi wengi sana wa kikabila huko Somalia, hii ilisababisha vacuum ambayo iliupa mwanya alshabab kuchukua nchi.

Marekani ikiingilia mapigano nchi za nje inafanya mambo yawe mabaya Zaidi. Mimi sioni sababu ya mmarekani kuingilia mapigano ya ISIL na kurds. Kwanini? Kwa sababu nina uhakika kama wairaq wakichoka utawala wa ISIL watawafukuza tu? Hata Iran ina uwezo wa kuwasambaratisha ISIL bila kutaja Saudi Arabia ambayo ina mamia ya ndege na vifaru kutoka marekani. Kwanini Marekani iliyopo mbali hivyo na Iraq iwe na mapenzi na watu wa Iraq kuliko wairaq au hata nchi za jirani?

Kuwapa siraha Kurds ni mchezo wa hatari sana kwa sababu hawa jamaa wataanza kuwaua wasunni, wasunni watataka kulipiza kisasi halafu mwishowe tutaona mauaji ya wenyewe kwa wenyewe yakiendelea tena.
Sababu ya Marekani kuingilia vita isiyoihusu ni nia yake ya kucontrol middle east, haitaki kuona nchi yoyote sehemu hii ya dunia kuwa na nguvu.

Mimi sio mwislamu, lakini kuna ubaya gani kama waislamu wakiamua kufuata sharia katika nchi zao ambazo ni 99 percent Muslim? Kwa mfano Misri?
​
Wandugu, tabia za wamarekani na wamagharibi zinazua chuki za kidini ambazo hapo mbeleni zitasababisha vita vya kidini baina ya jamii ambazo hazijawahi kuwa na mikwaruzano.
 
Nakubaliana na wewe kuwa chanzo cha ugaidi ni marekani, na kama ilivyokwisha vita ya Angola baada ya Marekani na Uingereza kusitisha msaada kwa kikundi cha waasi, hivyo hivyo itakuwa kwa waarabu. Lakini pia tukubaliane waarabu ni watu wa ajabu sana. Kwa nini wananulika kwa bei rahisi hivyo? Na hapa naamanisha kuanzia nafasi ya mtu moja hadi taifa. Waarabu walidanganywa kwamba sadamu ni tatizo akanyongwa, wakadanganywa Gadafi ni tatizo akauawa. Sasa wanaendelea kudanganywa piganeni tutawapa silaha. Kikundi. Kikundi kikianza kushinda Marekani anasema ni cha kigaidi anatoa msaada kinafutwa, then anatengeneza kingine mchezo unaendelea.... Waarabu kataeni Mzee2000
 
Last edited by a moderator:
Kamili,

Kweli naamini kama Saudi arabia wakisema Kesho wanawawekea vikwazo Eu na Marekani yaani hawawauzii mafuta kwa miezi sita tu, lazima marekani itaacha kusaidia waisraeli nao watakaa chini Na kuongea na wapelestina.

Inakuwaje waarabu wanaamini kwamba marekani inaweza kutatua matatizo yao?
 
imebaki afrika tu mkuu urusi,china,iran,n.korea,cuba,venezuela n.k walishawashtukia longtime
 
Mzee2000
si waarabu wote mkuu nchi kama qatar,syria hawamwamini mmarekani na ndio maana hawapatani hata na saudiarabia ambaye ni mshirika wakaribu wa marekani.
 
Last edited by a moderator:
Tatizo Qatar haina msuli kama Saudi.Kwanza Qatar ni kanchi kadogo ambako wageni ni wengi kuliko wazawa.
 
Tatizo Qatar haina msuli kama Saudi.Kwanza Qatar ni kanchi kadogo ambako wageni ni wengi kuliko wazawa.
ukitoa saud ambao wanaongoza kwa kununua silaha marekani hapa duniani,nchi inayofuata ni Qatar.

Qatar ni ndogo sana,inazidiwa kidogo na gaza,lakini ina mambo makubwa sana.
 
Qatar ni mshirika wa marekani na ulaya si unajua ndio wa kwanza kutetea ghadafi kupigwa mabomu?Bila america qatar haina kitu
 
Marekani ilimtorosha jela Charles Taylor ikamkabidhi silaha akafanye mapinduz nchini kwake liberia kilichotokea wote tulishuhudia ni mauaji ya kutisha kuanzia liberia mpk sierra leone watu zaidi ya million 1 walipoteza maisha
 
kamili

Ni kweli ndugu yangu. Hawa jamaa ni wepesi kudanganywa. Ndo maana tunajaribu kuweka wazi ili watu wote wajue picha halisi.
Sasa Marekani na washirika wake wamelewa urahisi wanaoupata kwa waarabu, wakaingia choo cha kike wakataka kumwendesha Russia kama wanavyowaendesha waarabu. Sasa wamejikwaa kwenye kisiki kikubwa balaa.
 
Last edited by a moderator:
Mzee2000

Mkuu nakuunga mkono kabisa naamini baada ya isis kuisha hawa wakurd watajitangazia uhuru tu
 
Last edited by a moderator:
Mzee2000

Saudi Arabia walishafanya hivyo mwaka 1967 baada ya Israel kuingia vitani na Misri,jordan,lebanon na syria...wakati huo mfalme wa Saudi alikuwa akiitwa KING FAISAL akakata oil supplies kwenda soko la dunia...ili kuwaadhibu wote wanaounga mkono harakati za Occupation ya Israel....illitwa ''OIL CRISIS"

lakini huyu Faisal hakudumu kwanoi baada ya vita kuisha lilitengenezwa "Zengwe" au "inside Job" akawa Assasinated ndani ya Kasri lake huko Riyadh...na crown prince wake...

so viongozi walifuata wanaogopa yaliyomkuta FAISAL
 
Last edited by a moderator:
Mzee2000

Saudi Arabia hawana ubavu huo hata wafanyaje, wao ni kibaraka mkuu wa US akifuatiwa na EU.

Wakati fukufuku la US na Russia linaanza awali mwaka huu, Obama alienda Saudia kuwaambia wafungulie mafuta na gas ili Russia wapate loss.

Hata hivyo, Saudi ina assets zao nyingi sana US.
 
Last edited by a moderator:
JustDoItNow

Aslimia kubwa ya watu humu duniani wanajua ulaghai wa US ila hawana jinsi kwasababu wamebanwa kila sehemu.

Unadhani Africa tuna nini cha kuongea?? Wakati tulikaa kushuhudia Ghadafi anauwawa??
 
Last edited by a moderator:
Tumeshajua ya kwamba hawa jamaa sio ila tatizo linakuja nani wa kumvisha paka kengele?
Nalog off
 
Mzee2000

Nani alikwambia marekani ana shida na mafuta?anayo tele na yamejaa kwa matumizi hata ya miaka mia mbele.lazima ieleweke kuwa mmarekani ni mbabe hivyo lazima afanye juu chini kuhakikisha wengine hawawi na nguvu kiuchumi,kiteknolojia na zaidi kijeshi.dunia yote inafahamu namna anavyotumia mbinu zote kutekeleza haya.aliyekutangulia katangulia tu tusiwalaumu waarabu
 
Last edited by a moderator:
Mzee2000
Great thinkers kama wewe wamebaki wachache sana huku JF sikuizi tumebaki na mipumbavu tu huku utaona watavyo mwaga uharo sasaivi we subiri
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom