Ni lini CCM wamewahi kupinga hadharani jambo linalofanywa na Raisi alie madarakani?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,694
149,920
Kama lipo nitajie na hasa yale maamuzi ambayo kwa namna moja au nyingine yameligharimu Taifa hili.


Na pie nitajieni jambo ambalo wapinzani kwa nguvu zao zote walishauri vinginevyo na mwisho wa siku wakaishia kuumbuka.

Ukipata majibu ya maswali hayo,basi utakuwa umepata jibu la hatima nzima la sakata hili la mchanga wa dhahabu kwa hapo baadae.
 
Kazi yao kubwa ni kusifia na kupigia makofi hata kwenye upumbavu.

Marais wanaojaza vijembe kuliko Maendeleo ya Taifa.

Marais wanaothamini ubaguzi na matusi kuliko umoja wa kitaifa.

Marais wanaojali kuua Watanzania wanaohoji kuliko kulinda Uhai wa RAIA na bado wako busy kupiga Makofi.
 
Haijawahi kutokea wao ni kila kitu wanaunga mkono hata la aibu wao ni kusifia tu na kupiga makofi. Ndio walivyo na tumefika humu shimoni kutokana na ma-ccm.
 
Hakuna Hata siku moja. Ya kipuuzi wanayasifia na bungeni kwa wingi wanaitikia ndioooooo na makofi juu.

Lakini ya wapinzani ya Maana yanapuuziwa,mwishoni inageuka kuwa jiwe walilolikataa waashi.
 
Labda sehemu ya awamu ya pili. Lakini sehemu ya awamu ya pili mpaka ya tano sio rahisi kwa sababu Mwenyekiti ndie Rais. Halafu kumpinga Rais aliye madarakani (hasa kwenye kipindi cha kwanza) ni sawa na kuwaambia wapiga kura hafai hivyo uchaguzi ujao akae kando.
 
Back
Top Bottom