Ni lazima alipe kisasi

Ni lazima alipe kisasi

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
360,096
Reaction score
828,932
Hili jambo bichi kabisa! Yaani ni halijaisha.. Ana usongo mkali na limemkaa shingoni

Mimi ni ile aina ya watu wasiokaa na kitu moyoni.. Sitaki kabisa kuhifadhi sumu mwilini.. Zina madhara.. Ni mwepesi mno kupotezeq jambo na ku move on!

LAKINI kuna watu wengine sio mama mimi.. Wao hawapotezei.. Ni watu wa visasi ni watu wa vivyongo! Ni lazima walipe kisasi kwa namna yoyote ile!

Akikosa kabisa namna ya kulipa kisasi basi ili kujipa nafuu ya moyo atakubwatukia bila kujali yeye ni nani yuko wapi na anafanya nini

Kwenye medani za vita kuna kitu kinaitwa gorilla war Ni vita ya mtaa kwa mtaa vita ya kuviziana! Vita ya piga nikupige!

Waswahel wanasema kimemlamba Rachel Dangwa anapenda sana hilo neno.. Mnajua ile ilikuwa ni perfect timing! Ukiingia kwenye anga za watu lazima upigwe na kitu kizito!

Wandengereko wanasema kumkoma nyani jiladi yaani ukitaka kumuua nyani usimwangalie usoni! Maana utamuonea huruma! Wewe bonda tu mpaka roho itoke!

Bwana Msema Chochote alipata nafasi adhimu na hakufanya kosa! Akaitumia vilivyo😀 Nadhani alishaandaa helmet imara la kutembea nalo!

Alipomaliza yake akampa pande bwana mwenza naye aseme chochote.. Kwa mshangao wa wengi naye akapita mulemule, hakutaka kupindisha wala kumung'unya maneno! Akanyooka kama rura! Naye akampasua.. Alipata golden chance akaitumia vilivyo! Atembee na bullet proof sasa!

Hii sasa imedhihirika ni vita ya one against two Au kinyume chake! Kama vita ya sasa tuu!

Kwenye msahafu mmoja kuna kitabu cha mesali Hicho kitabu yaliyomo yamo.. Maana kinajua kusimanga! Ila sikuwahi kujua na kitabu cha Wafalme nacho kina vipengele vyake vilivyobeba uhalisia mchungu kwa wakosefu wa uumbaji walionajisi ardhi takatifu!

Kile kipande kilisomwa kwa sauti ya utulivu sana na binti mmoja mpole msafi wa moyo na mwili.. Ukali wa yale maneno mbele ya hadhira iliyokaa kimya kwa utulivu yalikuwa kama hukumu ya upanga ukatao kuwili..

Yalipenya na kusambaratisha kiburi na majivuno yote! Yalihukumu bila huruma!

Ukimya huongea! Kuna moments kuna mambo hutokea kwenye ukimya yanatisha sana!

Mtu anaweza kuondoka mahali ni kama vile anaenda gerezani baada ya hukumu kupita!

1772378945807.jpg
 
Hili jambo bichi kabisa! Yaani ni halijaisha.. Ana usongo mkali na limemkaa shingoni
Mimi ni ile aina ya watu wasiokaa na kitu moyoni.. Sitaki kabisa kuhifadhi sumu mwilini.. Zina madhara.. Ni mwepesi mno kupotezeq jambo na ku move on!

LAKINI kuna watu wengine sio mama mimi.. Wao hawapotezei.. Ni watu wa visasi ni watu wa vivyongo! Ni lazima walipe kisasi kwa namna yoyote ile!
Akikosa kabisa namna ya kulipa kisasi basi ili kujipa nafuu ya moyo atakubwatukia bila kujali yeye ni nani yuko wapi na anafanya nini
Kwenye medani za vita kuna kitu kinaitwa gorilla war Ni vita ya mtaa kwa mtaa vita ya kuviziana! Vita ya piga nikupige!
Waswahel wanasema kimemlamba Rachel Dangwa anapenda sana hilo neno.. Mnajua ile ilikuwa ni perfect timing! Ukiingia kwenye anga za watu lazima upigwe na kitu kizito!

Wandengereko wanasema kumkoma nyani jiladi yaani ukitaka kumuua nyani usimwangalie usoni! Maana utamuonea huruma! Wewe bonda tu mpaka roho itoke!

Bwana Msema Chochote alipata nafasi adhimu na hakufanya kosa! Akaitumia vilivyo😀 Nadhani alishaandaa helmet imara la kutembea nalo!

Alipomaliza yake akampa pande bwana mwenza naye aseme chochote.. Kwa mshangao wa wengi naye akapita mulemule, hakutaka kupindisha wala kumung'unya maneno! Akanyooka kama rura! Naye akampasua.. Alipata golden chance akaitumia vilivyo! Atembee na bullet proof sasa!
Hii sasa imedhihirika ni vita ya one against two Au kinyume chake! Kama vita ya sasa tuu!
Kwenye msahafu mmoja kuna kitabu cha mesali Hicho kitabu yaliyomo yamo.. Maana kinajua kusimanga! Ila sikuwahi kujua na kitabu cha Mwanzo nacho kina vipengele vyake vilivyobeba uhalisia mchungu kwa wakosefu wa uumbaji walionajisi ardhi takatifu!
Kile kipande kilisomwa kwa sauti ya utulivu sana na binti mmoja mpole msafi wa moyo na mwili.. Ukali wa yale maneno mbele ya hadhira iliyokaa kimya kwa utulivu yalikuwa kama hukumu ya upanga ukatao kuwili.. Yalipenya na kusambaratisha kiburi na majivuno yote! Yalihukumu bila huruma!
Ukimya huongea! Kuna moments kuna mambo hutokea kwenye ukimya yanatisha sana!
Mtu anaweza kuondoka mahali ni kama vile anaenda gerezani baada ya hukumu kupita!View attachment 3551450
Aisee kumbe kitabu cha 'Beginning' kina mambo mengi Sana.
 
Ukamwambie, ukisema, BWANA asema hivi, Je! Umeua, ukatamalaki? Nawe utamwambia, kusema, BWANA asema hivi, Mahali pale mbwa walipoiramba damu ya Nabothi, mbwa watairamba na damu yako,..!
Kuna kifungu yule dada mwenye 'mawani' alipofika akainua kichwa then akamaintain 'eye contact' kwa muda. Mambo ya Siti za mbele sio kabisa. Ni heri back benching.
 
Back
Top Bottom