Ni kweli yalitokea

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,720
215,776
Mtoto Getrude amenifanya nikumbuke hii habari, inahusu binti anaitwa Mainda, baba yake mainda ni dereva katika ofisi za serikali, mama anajihusisha na biashara za hapa na pale, Mainda alikuwa na akili sana, alifanikiwa kupata division one form four, alipata scholaship kwenda International School of Tanganyika kwa masomo ya form five na six kukiwa pia na offer ya University Education Europe.

Pale IST watoto wengine walimuona Mainda ni wa ajabu, hakuwa na uwezo wa kuchangia activities nyingi za shule, hata kukiwa na party hakutaka kwenda kwanza hakuwa kwenye nafasi ya kuwa fashionsta.

Mainda alifaulu vizuri form six na alipata admission Ujerumani for her first degree kwa masharti familia ichangie 1/4 ya gharama na chuo kitatoa pesa iliyobaki. Kwakweli habari hii ilikuwa mzigo mkubwa kwa familia, hali iliyompelekea Mainda kupata msongo wa mawazo. Ndugu kutoka kijijini waliuza walichoweza kutoka kuku, bata, mbuzi ng'ombe n.k lakini wanaambiwa pesa iliyopatikana inatosha ticket tu pekeyake.

Familia ilimwachia Mungu swala hili, Mainda hakuweza kupata mkopo wa vyuo vya hapa kwakuwa alitoka IST. Wakati familia imekata tamaa kuna mama mmoja Mmarekani alikuwa anafundisha kile chuo cha Ujerumani, aliuliza kwanini Mainda hakutokea shule, alipewa jibu kuwa ameshindwa kumudu gharama na mpaka pale chuo kilishajitolea sana na hakuna jinsi angeweza kusaidiwa.

Yule mama alikuwa anamaliza mkataba wake wa kufundisha Ujerumani na alikuwa anarudi Marekani, alikwenda kuongea na vyuo vya Marekani kuangalia jinsi atakavyoweza kumsaidia Mainda, chuo kimoja kilitoa offer, ya ticket, gharama zote za malazi na pesa ya kujikimu, in return Mainda alitakiwa afanye kazi library weekend na akiwa likizo.

Siku Mainda anapanda ndege kwenda Marekani ilikuwa mara yake ya kwanza, nilikutana na Mainda kwenye ndege, hili sio jina lake. Ninaimani atafika mbali.
 
Hongera kwa chai tamu, hakika ukiinywa inaleta mental picture hasa pale Mainda anapopanda ndege
 
Mara nyingi wale wanaolipiwa mamilioni hawana achievements za aina hii.
 
Back
Top Bottom