Jinsi Hofu inavyoweza kukwamisha mafanikio ya mtu.

realMamy

JF-Expert Member
Apr 28, 2024
1,357
2,869
Hofu inaweza kukufanya ukaona Jambo ni kubwa kama watu wanavyolizungumzia Kumbe hata hawalijui vizuri.

Mimi tangu nakua nimekutana na watu wanaojua kumtia mtu hofu ikiwamo hata wazazi wenyewe.

Nakumbuka kipindi hicho nilifeli Mtihani wa Form two nikapaswa kurudia shule ile ile lakini watu wanaonizunguka wananiuliza utaweza? Maneno ya kumtia mtu hofu yakawa mengi.
Wengine walidiriki kuniambia kama umeshindwa shule acha njoo tutafute pesa.
Lakini nilipiga Moyo konde nikarudia na nikafaulu vizuri mtihani wa Form Four.

Ikaja Chuo nikawa nimefaulu kawaida mtihani wa Form six na katika ku apply Chuo nikatajiwa vyuo ambavyo havitaweza kunichukua na waliokuwa wananishauri ni watu wazima ninaowaheshimu.

Wasijue nini kinaendelea kichwani kwangu nikaamua kuomba vyuo hivyo hivyo walivyoniambia sitachukuliwa.
Matokeo yake nikachukuliwa UDSM chuo nilichoambiwa yani pale hautaweza 😅.
Wakabaki kuduwaa.

Hata kazini hivo hivo nimekuwa nikijaribu kufanya vitu ambavyo mtu anakushauri ni ngumu sana hiyo.
Lakini unafanya vizuri sana.
Niko hapa kuwapa Moyo usitishwe na kitu chochote kikubwa fuata Sheria zote.

Hakuna Jambo linaloshindikana mbele za Mungu.
 
Back
Top Bottom