Ni kweli Wambura anaonewa?

Ndakilawe

JF-Expert Member
Jul 6, 2011
4,817
2,000Umati wa wanachama na wapenzi wa simba, waliofika klabuni hapo jana mchana, na kushinikiza Wambura arudishwe kwenye uchaguzi, au wapewe sababu za Wambuea kuenguliwa!

Je, Wambura kweli hastili kwa mujibu wa taratibu za soka, au anaogopwa?
 
Sibonike

JF-Expert Member
Dec 23, 2010
16,676
2,000Umati wa wanachama na wapenzi wa simba, waliofika klabuni hapo jana mchana, na kushinikiza Wambura arudishwe kwenye uchaguzi, au wapewe sababu za Wambuea kuenguliwa!

Je, Wambura kweli hastili kwa mujibu wa taratibu za soka, au anaogopwa?

Huyu Wambura alishakuwa kiongizi wa Simba na TFF siku za nyuma. Hivi najiuliza ana kitu gani kipya safari hii?
Tusifanye recycling ya viongozi wakati watu wengine wapo. Huyu haonewi. Apumzike tu
 
Petro E. Mselewa

Verified Member
Dec 27, 2012
9,484
2,000
Unajua viongozi wa soka wa nchi hii hawajui kumaliza masuala yao kidiplomasia.Kilichotakiwa kufanyika ni kumruhusu kugombea halafu kumnyima kura. Uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya Simba chini ya Wakili Msomi mwenzangu Dr.Damas Ndumbaro umeacha shaka kuu.

Katika uamuzi huo,Kamati imejikita katika sababu kuu mbili.Ya kwanza ni kwamba Wambura aliwahi kupeleka suala la soka Mahakamani.Ya pili ni kuwa aliwahi kufukuzwa uanachama. Lakini,hata Mwenyekiti wa sasa wa Simba,Ismail Aden Rage alimteuwa Wambura kuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji.

Sasa, aliteuliwaje mtu asiye mwanachama wa Simba kuwa kwenye Kamati Tendaji? Halafu,Wambura,kama si mwanachama wa Simba,alipewaje fomu za kugombea na kuruhusiwa kufanya mchakato mzima wa kugombea nafasi ya Urais. Nikiwa na heshima kubwa kwa Kamati ya Wakili Msomi mwenzangu Ndumbaro,nauona uamuzi wa kumuengua kama uliojaa ukakasi na bifu la kimichezo tu.

Suala hili kwasasa linaonekana dogo.Lakini,baadaye litakuwa kubwa na kuibua mgogoro Klabuni hapo ambao unaweza kuepukwa sasa.

Muhimu : Mimi si mwanachama wa Klabu yoyote Tanzania lakini ni mshabiki wa Klabu ya Yanga ya Tanzania na AC Milan/Barcelona za Ulaya.
 
Jospina

JF-Expert Member
Apr 19, 2013
2,423

Mkuu hebu soma maoni haya niliyoyadadavua sehemu:-
"Michael Wambura ameenguliwa kwenye uchaguzi wa Simba kwa kuelezewa kwamba si mwanachama halali baada ya kusimamishwa uanachama mwaka 2010 kwa kuifikisha Simba mahakamani. Tukiwa na dhamira ya kutenda haki, tutafakari haya:-
1) Mwaka ule 2010 Wambura aliomba Mahakama iwatake wanaodai yeye ni mchafu waileze Mahakama uchafu wake na wakishindwa basi yeye abaki kuwa msafi aendelee na uchaguzi. Kuulizia uchafu wako kwa mahakama kunahusiana nini na soka hasa ikizingatiwa kuwa alikuwa akitajwa kuwamchafu bila kuelezwa uchafu wake?
2) Aliposimamishwa uanachama alipewa haki ya msingi ya kujieleza ikifahamika kwamba "audi alteram partem" (sikiliza pande zote za kesi) ni msingi mmoja mkubwa wa maamuzi ya haki? Je, alisimamishwa uanachama bila kupewa haki hiyo? Kama hakupewa haki hiyo kusimamishwa kwake ni batili.
3) Kwa kuwa mgogoro uliohusu kusimamishwa kwake ulihusu uchaguzi uliomhusisha Aden Rage. Je kwenye kikao cha kumsimamisha uanachama, Rage alikuwepo? Kama alikuwepo ina maana alikuwa mwamuzi kwenye kesi iliyomhusu wakati msingi mmoja mkubwa wa maamuzi ya haki ni "nemo judex in causa sua" (mtu asiwe jaji kwenye kesi inayomhusu). Kwa hiyo kusimamishwa kwake kunakuwa batili.
4) Baada ya kusimamishwa uanachama, Wambura hakufanya mambo yoyote yanayohusu uanachama wake kama kuhudhuria mikutano, kulipia ada nk ikiwemo kuchukua fomu za kugombea uongozi (zinazotolewa kwa wanachama tu)? Kama alifanya mambo hayo, ina maana impliedly uamuzi wa kumsimamisha uanachama ulikuwa umefutwa. Vinginevyo,angezuiwa asifanye lolote kati ya hayo kwa kusimamishwa uanachama.
5) Kwa kufuata kanuni ya Estoppel, kwa kumfanya Wambura aamini kwamba ni mwanachama halali, mamlaka ya Simba inazuiwa kutangaza kinyume chake kwani imemshawishi aamini kwamba ni mwanachama halali na yeye ametekeleza mambo yote mwananachama wa Simba anayopaswa kutekeleza ikiwemo kuchukua fomu za kugombea uongozi
6) Baada yakusimamishwa uanachama hakuna hatua iliyoendelea na hivyo kuzua utata wa endapo kusimamishwa huko kunaendelea au hapana na utata huo unaimarishwa na Wambura kuendelea kushiriki shughuli za Simba kama mwanachama. Katika suala lolote la kisheria, kukitokea utata, utata huo humnufaisha mlalamikiwa ambapo katika kesi hii aliyelalamika ni mamlaka ya Simba dhidi ya mwanachama Wambura. "in pari delicto potior est conditio defendentis" (panapotokea utata kwenye kesi,utata huo humnufaisha mdaiwa)
7) Itasemwa hatua zote za misingi ya haki zilizoelezwa zinapaswa kuchukuliwa si katika kumsimamisha mwanachama bali katika kesi ya kumpa adhabu. Hapana, hoja hii haina nguvu kwa sababu huku kusimamishwa tu kunasababisha mwanachama huyu apoteze haki zake nyingi ikiwemo ya kuchaguliwa, hivyo taratibu hizo zilipaswa zifuatwe kuanzia hatua hii ya kumsimamisha uanachama kwani ni hatua kubwa dhidi ya haki zake.
8) Haki ya kikatiba ya mtu kujumuika na wenzake,kuchagua na kuchaguliwa isichezewe kwa hoja za kuungaunga.
Sina urafiki wala ujamaa na Michael Wambura na zaidi ya yote hatufahamiani ila siku zote napenda kuona haki ikitendeka kwa yeyote. Yeyote kwenye uchaguzi huu na wa Yanga akichezewa faulo, nitapaaza sauti kama mwaka ule alivyochezewa faulo Kifukwe wa Yanga, nilivyopaaza sauti kwenye gazeti la Bingwa.
Narudia kueleza niliyoeleza siku kadhaa nyuma, Mambo ya Wambura sasa yametosha, mwacheni awe huru, ajisikie kuwa sehemu ya Simba na sehemu ya Watanzania."
Huyu ni Ibrahim Mkamba mwanasheria.
 
VOICE OF MTWARA

JF-Expert Member
Dec 20, 2012
2,556
2,000
huu uzi umetulia. binafsi ni mwanayanga ila sifurahishwi na upuuzi huu wa ndumbaro na wenzake. natoa rai kwa malinzi na tff yake kumtendea haki wambura ikizingatiwa kuwa malinzi nae alishakuwa muhanga wa ubabaishaji kama huu
 
white wizard

JF-Expert Member
May 18, 2011
4,491
2,000
huu uzi umetulia. binafsi ni mwanayanga ila sifurahishwi na upuuzi huu wa ndumbaro na wenzake. natoa rai kwa malinzi na tff yake kumtendea haki wambura ikizingatiwa kuwa malinzi nae alishakuwa muhanga wa ubabaishaji kama huu

Soka la bongo ukishaonekana tu wewe ni tishio kwa mgombea waliomuandaa wao,na kwenye sakata hili Aveva ndio ameandaliwa sasa njia ya kumsafishia njia ni kumchinjia baharini wambura,si ndio yale yale ya uchaguzi wa TFF,Kwani hizo fitina ndio alikutana nazo malinzi.
 
mwangalingimungu

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
1,285
2,000
Mimi naishangaa jamii yetu Watanzania. Inaelekea wengi wetu tunashindwa kuelewa nia na madhumuni ya Katiba, sheria, kanuni na taratibu. Katiba za FIFA, TFF na Simba zinamruhusu kila mwanachama wa Simba kugombea nafasi ya uongozi. Wambura alifanya hivyo akiamini yeye ni mwanachama wa Simba. Aliziwiwa? Hapana kwa sababu Katiba haimziwii mgombea kuwasilisha fomu ya kugombea. Katiba inaruhusu mwanachama kumwekea pingamizi mgombea anayemwona hastahiki. Wanachama wamefuata katiba hiyo na kuweka pingamizi dhidi ya Wambura. Katiba imeipa uwezo Kamati ya uchaguzi ya Simba kusikiliza pingamizi hizo na kuzitolea maamuzi. Ndicho kilichofanyika. Katiba inaishia hapo? Hapana. Inampa uhuru asiyeridhika na maamuzi hayo kukata rufaa TFF. ndicho kilichofanyika. Huko kufunga mtaa kwa maandamano na kujitoa ugombea ni ishara kwamba hao wahusika (wagombea na wafuasi wa Wambura) hawana uelewa wa mchakato wa kikatiba ya timu yao wenyewe. Wataongoza na kuongozeka vipi? Maoni yanayofaa kukubalika kuwa ndio ukweli ni ya waliopewa jukumu la kusikiliza na kuamua kesi kisheria pekee. Tuliobaki tunapaswa kuwacha maoni yetu yawe maoni yetu, tusiyafanye maoni yetu kuwa ndio ukweli wenyewe. Kasoro hii ndani ya jamii yetu ndio iliotufikisha tulipo hata kwenye mchakato wa Katiba ya nchi yetu. Halafu eti tunawashangaa Wabunge!
 
Master J

Senior Member
Apr 19, 2013
131
195
Unajua viongozi wa soka wa nchi hii hawajui kumaliza masuala yao kidiplomasia.Kilichotakiwa kufanyika ni kumruhusu kugombea halafu kumnyima kura. Uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya Simba chini ya Wakili Msomi mwenzangu Dr.Damas Ndumbaro umeacha shaka kuu.

Katika uamuzi huo,Kamati imejikita katika sababu kuu mbili.Ya kwanza ni kwamba Wambura aliwahi kupeleka suala la soka Mahakamani.Ya pili ni kuwa aliwahi kufukuzwa uanachama. Lakini,hata Mwenyekiti wa sasa wa Simba,Ismail Aden Rage alimteuwa Wambura kuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji.

Sasa, aliteuliwaje mtu asiye mwanachama wa Simba kuwa kwenye Kamati Tendaji? Halafu,Wambura,kama si mwanachama wa Simba,alipewaje fomu za kugombea na kuruhusiwa kufanya mchakato mzima wa kugombea nafasi ya Urais. Nikiwa na heshima kubwa kwa Kamati ya Wakili Msomi mwenzangu Ndumbaro,nauona uamuzi wa kumuengua kama uliojaa ukakasi na bifu la kimichezo tu.

Suala hili kwasasa linaonekana dogo.Lakini,baadaye litakuwa kubwa na kuibua mgogoro Klabuni hapo ambao unaweza kuepukwa sasa.

Muhimu : Mimi si mwanachama wa Klabu yoyote Tanzania lakini ni mshabiki wa Klabu ya Yanga ya Tanzania na AC Milan/Barcelona za Ulaya.

Simba hawamtaki ila Yanga wanamtaka awe kiongozi wa Simba. ADUI MWOMBEE NJAA
 
Bavaria

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
48,397
2,000
Ngoja kwanza,

Kabla hamjachangia kuhusu mambo ya kina wambura naomba kuuliza.

Huu umati wote hivi wafanya biashara wanafanyaje biashara zao huu mtaa?

Kutiana umasikini huku
 
Jospina

JF-Expert Member
Apr 19, 2013
2,423
2,000
Mimi naishangaa jamii yetu Watanzania. Inaelekea wengi wetu tunashindwa kuelewa nia na madhumuni ya Katiba, sheria, kanuni na taratibu. Katiba za FIFA, TFF na Simba zinamruhusu kila mwanachama wa Simba kugombea nafasi ya uongozi. Wambura alifanya hivyo akiamini yeye ni mwanachama wa Simba. Aliziwiwa? Hapana kwa sababu Katiba haimziwii mgombea kuwasilisha fomu ya kugombea. Katiba inaruhusu mwanachama kumwekea pingamizi mgombea anayemwona hastahiki. Wanachama wamefuata katiba hiyo na kuweka pingamizi dhidi ya Wambura. Katiba imeipa uwezo Kamati ya uchaguzi ya Simba kusikiliza pingamizi hizo na kuzitolea maamuzi. Ndicho kilichofanyika. Katiba inaishia hapo? Hapana. Inampa uhuru asiyeridhika na maamuzi hayo kukata rufaa TFF. ndicho kilichofanyika. Huko kufunga mtaa kwa maandamano na kujitoa ugombea ni ishara kwamba hao wahusika (wagombea na wafuasi wa Wambura) hawana uelewa wa mchakato wa kikatiba ya timu yao wenyewe. Wataongoza na kuongozeka vipi? Maoni yanayofaa kukubalika kuwa ndio ukweli ni ya waliopewa jukumu la kusikiliza na kuamua kesi kisheria pekee. Tuliobaki tunapaswa kuwacha maoni yetu yawe maoni yetu, tusiyafanye maoni yetu kuwa ndio ukweli wenyewe. Kasoro hii ndani ya jamii yetu ndio iliotufikisha tulipo hata kwenye mchakato wa Katiba ya nchi yetu. Halafu eti tunawashangaa Wabunge!
unasemaje juu ya mtu asiye mwanachama kushiriki vikao halali vya chama na kupitisha katiba ya chama? ni kama mtu asiyejiandikisha kupiga kura, je hiyo kura itakuwa ni halali? si ndio uchaguzi wote utakuwa ni batili
 
mwangalingimungu

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
1,285
2,000
unasemaje juu ya mtu asiye mwanachama kushiriki vikao halali vya chama na kupitisha katiba ya chama? ni kama mtu asiyejiandikisha kupiga kura, je hiyo kura itakuwa ni halali? si ndio uchaguzi wote utakuwa ni batili
vyovyote nitakavyosema, yatabaki kuwa ni maoni yangu. Wa kujibu hoja hiyo ni mamlaka iliyopewa jukumu la kutoa maamuzi. Ila kwa maoni yangu hayohayo, kura hiyo ni batili, lakini si lazima maamuzi yote ya kikao hicho yawe batili. Kama maamuzi hayo yalipita kwa tofauti ya kura moja, yanaweza kuwa ni maamuzi batili. Kwa sababu kuna haki ya kuamini kwamba kura hiyo batili ndiyo iliyopitisha maamuzi hayo. Lakini kama maamuzi yalipitishwa kwa tofauti ya zaidi ya kura moja, bado yatabaki kuwa ni maamuzi halali kwa sababu hata kura hiyo batili ingefutwa, bado kungebaki kura za kutosha kupitisha maamuzi hayo. Nasisitiza tena kwamba hayo ni maoni yangu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom