Ni kweli tunamwenzi Hayati Mwl Nyerere au? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni kweli tunamwenzi Hayati Mwl Nyerere au?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilema, Oct 15, 2009.

 1. kilema

  kilema Member

  #1
  Oct 15, 2009
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Jana tuliadhimisha miaka kumi tangu Mzee wetu mpendwa baba wa Taifa hili Mwl JK Nyerere Alipotutoka. Mwl alipotutoka ahadi nyingi zilisiskika za toka kwa watanzania mbali mbali za kuendelea kumuenzi hasa katika mambo yafuatayo;uadilifu;kuwagawa watanzania ktk Ukabila Dini au rangi;Swala la Muungano na swala la kupiga vita maadui watatu ujinga Umasikini na Maradhi. Je hivi ndivyo tunavyomuenzi ?
  Rushwa imekuwa kwa kiwango cha kutisha mpaka imebadilishwa jina kwa Ufisadi
  Uongozi unauzwa kama bidhaa sokoni kwa kununua kura kutoka kwa wapiga kura
  Udini unaingizwa kila mahali ikiwa ni pamoja na uongozi ajira muhimu , elimu huduma muhimu hata bungeni mjadala ya kidini imeshamiri
  Ukabila unaanza kuota mizizi wahaya wachaga na wanyakyusa hawatumii tena majina ya asili kama byarugaba karugendo limo kessi mwamakula mwakyembe n.k. mfano Mshindi wa BSS ni matokeo ya Ukabila
  Wageni hasa weupe wanathaminiwa zaidi kuliko wazawa hasa wahindi na wazungu
  Muungano unakejeliwa waziwazi hata na viongozi
  Maradhi yameongezeka
  Ujinga Umeongezeka (illiteracy%)
  Umasikini ndo umekithiri na pengo kati ya masikini na matajiri limekua kupita kiasi.

  Huku ndio kumuenzi Mwalimu? Nisaidieni jamani
   
Loading...