Rutorial k
JF-Expert Member
- Jun 8, 2014
- 1,069
- 1,062
Shule binafsi zinapata soko kubwa sana nchini kwasababu watoto wanatiliwa mkazo kujua kiingereza. Siyo hilo tu hata chekechea siku hizi walimu wa mitaani wamegundua wazazi wanhitaji kiingeleza hivyo wanahakikisha watoto wanakalili japo salamu na kuhesabu pamoja nakutaja majina ya vitu kama wanyama nk.
Mtazamo wa serikali
Kwa namna ilivyo serilikali haioni umuhimu wa lugha ya kiingereza hivyo haina njia zozote za kuhakikisha watoto wanaifahamu lugha hii..hivyo kumekuwa na ukatishwaji tamaa wa makusudi unaofanywa na baadhi ya wadau wa elimu eti elimu haina usiano na lugha...wakitoa mifano ya wachina.
Msimamo wa baba wa taifa
Aliwahi kusema..kiingereza ni kiswahili cha dunia..kukiacha kife ni ujinga. Baba wataifa ni miongoni mwa wanafalsafa wa elimu ambae alitetea elimu ya ujamaa na kujitegemea( education for self reliance) lakini bado aliona umuhimu wa lugha ya kimataifa (kingereza)
Tatizo ninaloliona kuhusu kiingereza..
Siyo kwamba hatukipendi kiingereza ila kinahitaji rasilimali nyingi sana ili watoto waweze kukimudu..kwa mfano walimu wa lugha hiyo wanatakiwa angalau kupelekwa nchi zinazongumza lugha hiyo ili waweze kuzoea kuwasiliana kwa mda wote ( aculturation).
Sasa kutana na Mwl wa kiingereza wa hapa kwetu ujionee vituko...yaani hata dakika tano hafiki akiwa anaongea kingereza..matamshi ndio usiseme..huu ni utani katika soko la ajira la kimataifa.
Ushauri wangu kwa serikali.
Isiogope kutumia rasilimali katika kuwapa wananchi wake elimu..waache kutumia walimu wa kidato cha nne kufundisha watoto kingereza wakati hawajui matamshi ya lugha hiyo kwa kuwa phonology haifundishwi O level ili mwalimu aajiriwe kufundisha kiingereza lazima afanyiwe usaili katika nyanja kuongea na kuandika.
Mwisho..
Kiswahili ni chetu na tayari kimekita mizizi ...tutilie mkazo kiingereza ambacho hatuna ili tuwe na vyote..Asanteni