Ni kweli Tanzania hatuendelei kwenye elimu?

Ni kweli Tanzania hatuendelei kwenye elimu?

Clark cian

Senior Member
Joined
Jul 3, 2021
Posts
198
Reaction score
214
Ni matumaini yangu hamjambo ,mu wazima wa afya kabisa wakuu.

Poleni na majukumu ila Mimi Kuna kitu kinazidi kunimaliza siku Baada ya siku na hicho kitu siendi mbali ila nipo kwenye suala.la mfumo wa elimu nchini.

Mimi Tangu nimalize darasa la sana mwaka 2014 mpaka sasa sijaona mabadiliko yoyote kwenye sekta hii hususani kwenye mfumo wa utoaji elimu

Cha kwanza kabisa ni ile kasumba ya wanafunzi kupokezana madarasa yaani wengine wanaanza asubuhi ,alafu wengine wanaingia mchana aisee huu mfumo ulikuwepo tangu kipindi hicho Cha mwaka 2008 Hadi leo hii bado kinaendelea.

Sasa napata maswali kibao ni kwamba serikali Haina fedha ya kujenga madarasa au nini shida? Au uongozi ni mbovu? Mimi Kwa kawaida najua mtu darasani ukoshamwingiza mchana sidhani kama attention anakuwa nayo Kwa uhalisia serikali naomba mliangalie hili suala linaniumiza sana Kwanzia kipindi hicho hadi sasa.

Cha pili sasa ni Ile desturi ya kwamba somo ni la practical lakini walimu wanalipeleka kwenye theory aisee hiki kitu ni kibaya na kinaenda kutumaliza sisi wanafunzi hasa tunapokuja wakati wa kujitafutia maisha, utakuta yees mmefundishwa jinsi ya kutengeneza vitu mfano meza au madawati lakini hamjawahi kushika hata nyundo hivi ni kweli hapa tutafika tunapotaka kwenda kweli? Afu utakuta kiongozi mkubwa anasimama anasema vijana mjitafutie ajira wenyewe au vijana hawapendi kujishughulisha hii ni sahihi kweli waungwana?

La tatu, nne, tano, sita Hadi Kumi nazidi kuandika kwenye andiko linalofuata ila aisee serikali iangalie hili daah naumia sana na huu mfumo wa elimu.
 
Inahitajika trillion 6.5 kujenga miundombinu ya kutoshereza Mahitaji ya wanafunzi waioko shuleni Hadi 2022.

Itachukua miaka 10 kutatua hili jambo.
 
Si kweli. Tunasonga mbele hatua kwa hatua kila uchwao.
 
Haitokuja kutokea kukidhi mahitaji ya watu ambao kila leo wanaongezeka, so usiwe na logic hiyo bali hii dunia ni ya "survival for the fittest"...

tafuta pesa umsomeshe mwanao pazuri ...done...
 
Back
Top Bottom