Ni kweli Tanzania haihitaji takwimu hizi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni kweli Tanzania haihitaji takwimu hizi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ralph Feksi, Jun 13, 2012.

 1. R

  Ralph Feksi Member

  #1
  Jun 13, 2012
  Joined: May 5, 2012
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wana JF.

  Miongoni mwa babari zilizogonga vichwa vya habari leo ni kuhusu umuhimu wa kupata idadi ya waumini wa dini mbalimbali katika sensa ijayo. Ingawa serikali na baadhi ya vingozi wanasema si muhimu kuwa na takwimu hizo lakini hivi ni kweli hazihitajiki? Kweli si vema kujua Tanzania kuna Wazungu wangapi, Wahindi, Waaarabu, na kila kabila lina idadi ya watu wangapi? Hivi ni sahihi kusema kuwa na takwimu hizi itahatarisha amani ya nchi!

  MY TAKE: Ninaamini watafiti wa sayansi jamii, wanasaikolojia, viongozi wa dini nk wangependa kupitia sensa ya taifa wapate takwimu hizi.

  Ninawasilisha.
   
 2. m

  masssaiboi JF-Expert Member

  #2
  Jun 13, 2012
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 637
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 33
  Ukweli ni kwamba hizi takwimu ni muhimu sana tu ili kujua mgawanyiko wa Watz ktk makundi tofauti. Ila sasa inapokuja issue ya maendeleo hatuhitaji kujua dini wala kabila la watu ili kuwapatia huduma muhimu, na hii ni kwa sababu watz tumechanganyikana kwa kila aina unayoweza kuifikiria. Tatizo kubwa ni kuna watu wachache wanataka kuitumia nafasi hii kisiasa au kwa maslaji binafsi, kama makanisa au misikiti inataka kujua idadi ya waumini wao si wakahesabu wenyewe!!! Na je ukishajua wepi wengi inasaidia nini??? Wapi huduma za kiserikali zinatolewa kwa misingi ya dini au kabila???? Mie nina ndg waislam, wakristo na wapagani na tumeoa na kuolewa na makabila kutoka kila kona na nje ya TZ, je hapa idadi ya kikabila inasaidia nini esp mtu kama mimi ambaye najua kiswahili labda na English tu na sifungamani na kabila lolote!!!!!!!
   
 3. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #3
  Jun 13, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Kwaupande wangu sioni Tatizo lolote kwa Tanzania Kuwa na Takwimu hizo kwani Vyovyote iwavyo wakristo watakuwa wakristo na waislam watabaki kuwa waislam mwisho wa siku na Watanzania watabaki kuwa watanzania Hoja hapa ni Utanzania na sio DINI,tuwe nazo tu takwimu kwani hazitoathili chochote
   
 4. w

  wikolo JF-Expert Member

  #4
  Jun 13, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 801
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Dhehebu linalotaka kujua idadi ya waumini wake linashindwaje kuwahesabu lenyewe mpaka lipitie kwenye mgongo wa sensa ya taifa? Hawa waumini wetu mbona tunao kwenye nyumba zetu za ibada karibu kila siku? Mambo kama haya ni kuleta misuguano isiyokuwa na lazima katika jamii.
   
 5. m

  mamajack JF-Expert Member

  #5
  Jun 13, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  wafanye wenyewe na kwa g'harama zao,si sadaka zinatolewa???acha mabo ya ajabu bwana.
   
 6. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #6
  Jun 13, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Wazo lako ni zuri, lakini mawazo ya wenzako wale wa "matamko" ni kwamba wanataka pato la taifa ligawanywe kufuata uwiano wa idadi ya watu kidini na nafasi za uongozi wa taifa vile vile. Kwa mantiki hiyo, wasukuma ambao ni 20% ya idadi ya watanzania wote nao watakuwa na haki ya kudai kupata 20% ya pato la taifa. Mwisho wa siku sijui tutafika wapi!
   
 7. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #7
  Jun 13, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Comrade liweke sawa hilo neno lilo colored wa "matamko" sio wenzangu, wenzangu mimi ni wajamaa,Comrade wajua tatizo ni Serikali kutotaka mabo haya kujadiliwa kwa uwazi kwa sababu huenda hata wale wa Umsho hawana sababu za msingi lakini kwa sababu hamtaki kuwasikiliza wanaonekana nao wanasababu Tuwaache watanzania wazungumze lakini si kila watakachokisema basi kichukuliwe,ni hayo tu Comrade
   
 8. Cha Moto

  Cha Moto JF-Expert Member

  #8
  Jun 13, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 945
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kwa nini tuwe na kitu ambacho hakina maana wala athari? kama ulivyosema?
  Huoni kama nikupoteza nguvu kwa jambo lisilo la kimaendeleo?
  Kama halina athari hakuna haja ya kuwa na hizi TAKWIMU.
   
 9. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #9
  Jun 13, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,838
  Trophy Points: 280
  vitu kama kama vinahitajika kwa ajili ya dini kwa nini makanisa na misikiti wasihesabiane huko huko??
  kuna watu wengi tu hapa bongo hawana dini kwa nini muanze kuingiza dini kwenye suala la kitaifa??
  hata kwa suala la makabila si nyeti sana kama watu wanavyodhani
   
 10. K

  Kahinda JF-Expert Member

  #10
  Jun 13, 2012
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 849
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 60
  Mkuu
  Ni kweli na nina amini kwamba kila dhehebu linajua au lina idadi ya waumini wao.
  Lakini serikali inatakiwa kujua hilo zaidi. (itatokana na jinsi unavyojua umuhimu wa kuwa na tarakimu)
   
 11. mnyikungu

  mnyikungu JF-Expert Member

  #11
  Jun 13, 2012
  Joined: Jul 26, 2009
  Messages: 1,441
  Likes Received: 581
  Trophy Points: 280
  brother kwani sensa ni nini? je senza inapofanywa huwa ni kwa matumizi ya maendeleo ya selikali tu?je unafahamu umuhimu wa sensa wewe? mfano kuna kabila moja hapa tanzania linahitaji uangalizi na mahitaji maalu je usipojua idadi yao selikali itapangaje bajeti kwa ajiri ya kuwahudumia hawa watu?, kuna watu wa mahitaji maalum kama albino je usipojua idadi yao utawasaidiaje?, but pia sensa ndo source of information, watu wote na taasisi ndo tunatakiwa tutoe huko data.
   
Loading...