kijana wa leo
JF-Expert Member
- Nov 28, 2011
- 2,916
- 7,164
Habarini wakuu,
Napenda kupongeza kasi ya Mh. JPM ya utumbuaji majipu na nimekua mstari wa mbele kumuombea afya njema ili aendelee na utumbuaji majipu hadi nchi ikae sawa mana mkwere alipoifikisha mungu ndo anajua na atatulipia kwa hayo mateso tuliyosababishiwa na mkwere.
Kilichonifanya niulete uzi huu apa ni kutokana nakutoamini macho yangu kila siku inapopita bila kusikia tanesco jipu limetumbuliwa. Naamini kati ya shirika linalochangia kurudisha maendeleo ya watanzania nyuma ni TANESCO,

- Wote tunaelewa umuhimu wa nishati katika kukua kwa maendeleo kiuchumi, lakini hili shirika toka lianzishwe halijawahi kumudu kuhudumia wananchi kwa kiwango kinachotakiwa,
- Halijawahi kujiendesha lenyewe kwa asilimia 100 (kumbuka hadi leo linategemea ruzuku serikalini kulipia mishahara wafanyakazi wake)
- TANESCO wameshindwa kuondoa tatizo la mgao wa umeme toka tupate uhuru na hakuna jitihada zozote zilizofanyika kuondoa tatizo hilo zaidi ya siasa tu.Atleast ata wangeweza kuweka umeme wa uhakika sehemu muhimu kama mahospitalini.
- Ndio shirika linaloongoza kwa kashfa za ufisadi wa pesa kubwa za walipa kodi na linaongoza kwa mikataba iliyoliingiza taifa katika hasara kubwa.
- Ni shirika ambalo haliwezi kutatua matatizo ya upatikanaji wa nishati ya umeme kwa kutumia vyanzo vyake vya ndani kama makaa ya mawe, upepo,gas na hata material kama transformer (Tuna kiwanda tanzania na TANESCO wana share ila tunaagiza nje transformer) sijui tumerogwa na nani!!!