Ni kweli serikali yetu inasaidia kukuza soka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni kweli serikali yetu inasaidia kukuza soka

Discussion in 'Sports' started by Japhari the Gun, Nov 1, 2011.

 1. J

  Japhari the Gun Member

  #1
  Nov 1, 2011
  Joined: Aug 19, 2011
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  NI KWELI SERIKALI YETU INASAIDIA KUKUZA SOKA? Habari zenu wasomaji wangu popote pale mlipo lisomwapo jarida hili mahiri la mpira wa miguu Tanzania,leo nimekuja na mada kuu moja iliyopo mezani je umewahi kujiuliza swali dogo lakini la msingi kama hili “eti jamani ni kweli serikali yetu inasaidia kukuza maendeleo ya Soka hapa nchini? Je kama inasaidia kivipi? Na kwa kiasi gani? Jibu naamini kila mtu analo sihitaji kulitoa maana liko wazi hata kwa mtoto mdogo. Mimi si kwamba nabeza serikali yetu inachofanya la! Imejenga Kiwanja kizuri na bora sana,kutuletea makocha wengi tu wakigeni,kuanzisha mashindano kwa Watumishi wake wa kada mbalimbali na mambo mengineyo mengi. Swali je ni kweli Serikali yetu ina paswa kuishia hapo katika mchezo huu wa soka ili tuweze kusonga mbele? Mimi nataka kuwafumbua macho Watanzania wengi ambao hawajaliona hili si kwamba mimi najua sana la! kwani wengi tunaona kuwa serikali yetu inasaidia Kukuza michezo hapa nchini kitu ambacho si kweli kwa mtazamo wangu, kama kweli inasaidia kukuza, swali linanijia mbona sioni kinachofanyika katika kukuza michezo hii zaidi ya hizi zima moto za kuleta hawa wanaoitwa Wataalam na baadaye kushinei tunalala chali bila ya mafanikio yoyote katika soka Sasa nimegundua kuwa zima moto hizi zinazofanywa kisiasa na kisha kujisifu kwenye majukwaa nimefanya hiki mie nimefanya kile mie hamwoni kisha kushangiliwa na kutimiza haja zao si kwa ajili ya kuinua soka bali Soka imekuwa mtaji wao wa kutafutia kuaminiwa na watu, Watanzania naomba tuamke na kukataa kugeuzwa kuku wa kienyeji kutohudumiwa lakini ukinenepa unachinjwa tena kwa makeke. Sasa tujiulize kama serikali yetu iko serious na kusaidia michezo mbona Umiseta na Umitashumita vimerudishwa halafu hakuna bajeti yake mtokeo yake mikoa husika iliyopewa kufanya mashindano hayo kwa majaribio ilifanya kudunduliza na kufanya maandalizi hafifu tena ilikuwa kwa mikoa michache je ikiwa mikoa yote ya Tanzania bara itakuwaje? Kisha tunaambiwa wamejipanga kuifanya vizuri zaidi kuliko ilivyokuwa sasa unajiuliza je vijana watakao patikana katika mashindano hayo watakwenda wapi maana wenzetu wakiwapata uwapeleka katika sports academy zao na kulelewa huko kisha kuwa nyota, sisi wakipatikana inakuwaje? Pia napongeza sana kwa kurudisha hadhi ya chuo cha Malya cha mkoani Mwanza lakini mshaliona hili Mbona mnaandaa walimu na viongozi wa michezo ambao hawana wanafunzi na watu wakuwaongoza,hivi unajiuliza hao walimu wa michezo Watakao hitimu huko Malya watafundishaje?,wapi? Maana mazingira ya shule zetu za kawaida zinajulikana ni mpira mmoja ambao ulitolewa na Diwani wakati wa kampeni ili achaguliwe sasa unajiuliza ni kweli serikali hii inajipanga kweli kwa kusaidia kukuza soka hapa inchini?Je ushajiuliza hadhina ya wanasoka tulionayo Tanzania maana kila Mtaalam anayeletwa anakili hilo hata Carlos Alberto Pereira alikili hili na kutabili kama tutawatunza wale vijana waliokwenda South Africa basi twaweza kucheza kombe la Dunia mwaka 2014 huko kwao Brazil, sasa najiuliza wako wapi maana aliyekuwa kipa Bora sasa ni Konda huko Rock City,hawa wanasoka wanao kuwa ovyo bila msingi wa soka lakini bado wakitoka hapa inchini wanaonekana balaa mifano ni mingi sana nadhani ni kupoteza muda kuitaja,sasa kwa nini serikali isitilie mahanani na kuwapa hawa vijana ajira yenye mvuto na inayoheshimika katika jamii kwa angalau kuwakusanya katika shule moja na kuhudumiwa pamoja? Je ni nani amewahi kusikia Wizara ya michezo imetenga fedha kwa ajili ya kuendesha na kuendeleza michezo hapa inchini hata kwa kujenga shule moja tu ya mpira wa miguu ambayo ni rahisi kumjua mchezaji kwani unachezwa hata barabarani,hivi ushaona mtu anamiliki gari lisilo na matairi kisha akasema yeye ni hodari wa kulipa road license? Sasa hicho ndicho watanzania tunafanyiwa kwani haiwezekani wewe ukamiliki viwanja zaidi ya kumi halafu huna hata timu moja hii inamaanisha hivi viwanja vimepatikana kiujanjajanja tu na kuwafunika wananchi macho,jamani tuache siasa kama tunataka kukuza soka basi tufanye yale yanayotakiwa kufanywa soka liende mbele sio kuziba matundu ya Panya kwa vipande vya Mkate. Je ni kweli serikali yetu inashindwa hata kujenga Shule za Michezo (Sports Academy) angalau tatu kwa Tanzania bara na moja tu huko upande wa Zenji zenye ukubwa wa kuchukua wanamichezo chipukizi wenye umri mdogo 500 tu kwa kila kituo,kwa idadi hii inaamanisha kila mwaka wa mwisho tutakua na wanamichezo 2000 yaani 1500 kutoka Tanzania Bara na 500 kutoka Tanzania Visiwani. Mfano wanaweza kufungua kikanda yaani Mwanza ikakusanya kanda ya ziwa,Mbeya ikakusanya kwa kanda ya juu kusini,Arusha kwa kanda ya kasikazini,na mashariki ikawakirishwa na Dar-es-Salaam kisha wakapata mashindano maalum yatakayo jumuisha na zile za watu binafsi pamoja na Timu za kitaa yaani kama haya ya Kopa Cocacola, kisha Timu za ligi kuu kuchukua baadhi ya wchezaji waliokwisha kuwa na umri wa kutosha kucheza ligi kuu na kuwatumia naamini baada ya miaka mitano tu matunda yataonekana na tutakuwa na bonge la kiwanda cha wacheza hapa Tanzania. Kwa maana hiyo hawa Makocha wanaoletwa na kulipwa mafedha yakutosha wangekuwa wanapata krimu nzuri ya wanasoka wazuri na kutisha katika mashindano mbalimbali,Mimi kama kijana bado lawama zangu naitupia serikali kwani kwa kutambua kuwa michezo ni muhim iliunda mpaka wizara inayohusika na suala hili ikimaanisha imejipanga na iko serious mbona hatua hatupigi je kuna mtu anaweza akasema nini Wizara imefanya kuinua michezo je ni kukabidhi tu bendera ya taifa kwa wanamichezo wanaofanya juhudi binafsi na kufanikiwa kushiriki mashindano mbalimbali ambayo pia uchemka na kurudi wakitwambia wamejifunza kitu je nilini tutaambiwa wameshinda kitu Naamini jibu sahihi ni Serikali kutenga bajeti na kuhakikisha inafanya kazi iliyopangiwa ya kuendeleza michezo na wala si kuajiri watu wasiokuwa na cha kufanya, mfano maafisa utamaduni na maafisa wa michezo wanafanya nini kwani hata zile timu za MIKOA ambazo zinashiriki Mashindano ya Taifa Cup huwa zinageuka ombaomba pale tu mashindano yanapoanza utasikia eti jamani watu mliotoka mkoa Fulani mnaombwa kujitokeza kusaidia timu ya mkoa wenu ili ifanye vizuri, Je hivi ndivyo wenzetu waliopiga hatua katika soka walianza jamani? Ukiwa mpenda soka kama mimi nadhani utakuwa umeshajua nini na zungumzia hapa yaani namaanisha sapoti inayotolewa na serikali yetu ni ile ya msimu na kufaidisha watu fulani hasa wanasiasa kwa ajili ya malengo yao binafsi hivi ushajiuliza atakapoondoka huyu Rais tuliyenaye soka itakuwa katika hali gani?je kungekuwa na miundo mbinu sahihi ya kuendeleza soka inaamanisha angeondoka akatuacha pa zuri kwani tungekuwa na fursa ya kuendeleza kilichoachwa Naamini baadaye viwanja hivi vitaanza kubadilishwa matumizi kwani nina uhakika kama mambo yatakuwa kama hivi basi tujiandae viwanja kubadilishwa matumizi kama ilivyoanza huko Rock city na huko Kagera au wengine walivyo ufanya uko kusini kuanikia Mpunga au kuona uwanja wa Taifa ukawa wa matamasha na kiwanja cha uziduzi wa albam za Wasanii. Je pia ushajiuliza ni kiasi gani cha pesa kinatumika kuendesha mashindano ya TAMISEMI, na mashindanno ya SHIMIWI? Kwa nini hizi zisitumike kuendeleza michezo kwani kila mwaka fedha itumikayo inaweza kabisa kujenga shule moja na ikakamilika au kukaribia kukamilika kwani ukiangalia kwa undani mashindano haya hayana maana badala yake ingeagiza kila indara husika kuwa na Timu za vijana au wachezaji wasiozidi umri wa miaka 25 na kushiriki mashindano hayo au ligi nyinginezo kwani pia tungepata chanzo kingine kizuri cha wachezaji wa ligi kuu hapa inchini. Hayo mamilioni yanapotea bila faida je nini tumepata tangu hayo mashindano hayo yaanze kufanyika zaidi ya kuchangia mfarakano ndani ya ndoa za watu napengine kuchangia kueneza ukimwi.Mbona wakati nakua nilisikia wanasoka wengi wakitokea katika Mashirika na makampuni mbalimbali kwa nini sio sasa wakati soka inalipa sana hata kibongobongo tu. Jamani Wahusika huko naomba muamke,hasa kwa nyinyi mnaokwenda kupewa hivi viti vya mawaziri hebu naomba mje na plan B ya kukuza hili Soka letu, mimi huwa naumia sana kwani hata mimi nilikuwa mchezaji mwenye matumaini mengi lakini mwisho wa siku nikafulia sipendi kuona vijana wenzangu wakipita tundu lile baya nililopita.Serikali naomba mtusaidie mjenge hata shule moja tu ya maana kama mfano ili watoto watakaopatikana katika mashindano ya UMISETA, UMITASHUMITA na Kopa Cocacola wakasome uko ili tutambue kuwa vijana waliofanya vizuri katika mashindano mbalimbali tutawapata wapi? Naomba na nyinyi watu mliopewa dhamana ya kuendesha michezo kuamka na kutuma rasmu mbalimbali kwa serikali kwa ajili ya kuendeleza soka hapa inchini siyo kulalamika tu kuwa mmepata hasara katika mashindano,Hiki nikilio na maswali Tunategemea Waziri unayeshika Wizara hii utatusaidia kwa hili, Wasalaam. Na Magesa JaphariE-mail:magesajaph@yahoo.co.ukMobile No.0784269812 or 0714368843
   
Loading...