Ni kweli pesa za EPA zimerudi? Tuaaminije?! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni kweli pesa za EPA zimerudi? Tuaaminije?!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Phillemon Mikael, Sep 4, 2008.

 1. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #1
  Sep 4, 2008
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,427
  Trophy Points: 280
  ..MOD naomba hata kama hii mada itabidi kuiunganisha ikae kwa muda......


  wadau lengo la kuiweka hii thread tofauti kidogo na thread mama ..ni kuchokoza mada....

  taarifa tunazopata kutoka kwa vyanzo mbali mbali juu ya kurudishwa kwa pesa za EPA ni tata....watu wengi waelewa wamefikia kuamini kuwa hakuna pesa ya EPA iliyorudishwa ..na KUWA hili jambo linafanywa kisiasa tu ili kufunika kombe ..mwanaharamu apite....

  naomba kutoa hoja kuwa vitengo vyote vya JF viingie kazini ili kuchunguza kama kuna ukweli wa hizi fedha kurudishwa..kwani zaidi ya muheshimiwa rais kututaka tuamini tu eti kwa kuwa kuna mabwana tunawaona wanatembea mjinii wamechika [hata kama wanajifanyisha]..haiingii akilini....mashujaa hapa jf walimudu kubaini fedha zilivyochukuliwa ...namba za hundi..makampuni..tarehe na kila kitu....SASA TUNAOMBA TUCHUNGUZE KAMA PESA ZIMERUDI ZIMERUDI KWA HUNDI ZIPI? ZA MAKAMPUNI GANI??..ZIMEINGIA AKAUNTI IPI?....ets....itabainika tu.,......!!!..kwani haya yote yanafichwa......siamini kama pesa zilitumika kugharamia shughuli za wanamtandao...zitarudije.....sioni mantiki ya kibiasharaa ...zaidi ya kuleta KANUNI YA IMANI ...kama baadhi ya dini zinapoubiri kuwa YESU atarudi tena ...NA wote wanaubiri juu ya kiama...inabidi kuamini tu..hakuna swali....SASA JE WATANZANIA TUNATAKA KUAMINI TU HIVI HIVI KUWA PESA ZIMERUDI BILA USHAHIDI WA KUELEWEKA ...HILI HALIWEZEKANI!!!

  NAPENDA KUTOA ANGALIZO KWA KIKWETE..KUWA KAMA WANANCHI WANADANGANYWA PESA ZIMERUDI ..IPO SIKU ITAJULIKANA UKWELI......NA TUTATAKA KUJUA TENA KAMA ZIMERUDI...HAO WAKULIMA ALIOWAKOPESHA WAKO WAPI..........MASHAMBA YAO YAKO WAPI..nak...naamini kuwa kama hazijarudi na wanajifanya wanapeleka kukopesha wakulima ..itabidi wakopeshe wakulima hewa ...kwa kuwa kimsingi PESA HAKUNA...zaidi ya HEKAYA ZA ABUNUWASI au KUFIKIRIKA.....

  nina mashaka makubwa.....
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Sep 4, 2008
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  PM,
  Kama unaamini kuwa pesa hizo zimerudi ninacho kiwanja safi sana Kigamboni nitakuuzia kwa shillingi elfu tatu.
   
 3. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #3
  Sep 5, 2008
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,427
  Trophy Points: 280

  ...jasusi ,yebo,mwanakijiji,FMES[MZEE WA MABOMU,REV na wote WANA JF ..HESHIMA MBELE..MNAJUA MARA YA KWANZA KABISA KAMA SIKOSEI FMES ....HII KITU ILIANZIA HAPA!!!

  ..KWELI TUTASHINDWA KUBAINI...HIII GAME ..THESE IS SERIOUS ...WE NEED KUINGIA KAZINI HARAKA SANA ...FOR WHICH I KNOW..WE SHALL SMOKE THEM OUT!!!!!!!!!!

  ..KWELI WABUNGE WANADANGANYWA PESA ZINAENDA KWA WAKULIMA NA WANAPIGA MAKOFI....MKULIMA YUPI TANZANIA MWENYE UWEZO WA KUKOPA...???....UNLESS TUNGEKUWA NA COMMERCIAL FAMMERS....THIS IS THE GAME WAZEE!!???

  sasa tatizo watanzania wengi wanaweza kuamini zimerudi ......na haya maandamano yanayolazimishiwa..
   
 4. Kipunguni

  Kipunguni Senior Member

  #4
  Sep 5, 2008
  Joined: Jun 20, 2008
  Messages: 151
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Bwana PM,

  Umeiona signature ya Invincible .... Tanzania - Dola dhaifu, Viongozi wababe, Wananchi usingizini ... ame-summarize vizuri sana!
   
 5. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #5
  Sep 5, 2008
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,427
  Trophy Points: 280

  true ..naomba afanye marekebisho kidogo.....DOLA DHAIFU,KIONGOZI MWOGA,FISADI,WANANCHI USINGIZINI..[usingizi mzito,tunahitaji kuamshwa tupigwa nyundo]

  nani atatupiga nyundo..au nyundo ya mafisadi itatuamsha??
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Sep 5, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,496
  Likes Received: 81,812
  Trophy Points: 280
  PM, hakuna pesa zilizorudishwa ndiyo maana kila anyeongea kuhusu pesa zilizorudishwa anatoa amount tofauti na mwingine. Mara utasikia zilizorudishwa ni shilingi 60 bilioni, mara 55 billion, mara 53 billioni na wala hakuna anayejua pesa hizo zimewekwa wapi. Kwenye bajeti ya mwaka kesho watafanya usanii na kutangaza bungeni kwamba pesa zilizorudishwa na mafisadi wa EPA zimeshaingizwa kwenye bajeti ya wizara ya kilimo na hivyo kuendeleza ufisadi wao dhidi ya Taifa la Wadanganyika.
   
 7. Tonga

  Tonga Senior Member

  #7
  Sep 5, 2008
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 175
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Na kama ni USANII JK ndio kinara, kwasababu yeye ndio anayeshikilia kusema zimerudi na hata kuitangazia Dunia the same lie ili aonekane anafanya kazi,(na ili apewe misaada zaidi). Ila kama ni uongo, basi yeye ndio wa kwanza kushikwa na kutueleza ukweli.
  Hapendwi mtu hapa ni haki mpaka kieleweke.
   
 8. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #8
  Sep 5, 2008
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,427
  Trophy Points: 280
  ......zaidi ya pesa rais kusema zinapelekwa wizara ya kilimo...ni kiini macho kwani marekebisho kwenye bajeti ya wizara ya kilimo hayakufanyika ili kuingiza pesa za RPA...wote tunajua taratibu za bajeti ya serikali hapa,....huwezi kuingiza pesa kiholela bila kuwa kwenye fungu la bajeti...ingebidi bunge lifanye marekebisho bajeti ya kkilimo kuingiza hilo fungu kama kweli lipo.......inatia shaka...

  wizara ya kilimo ipo chini ya msiri wa jk ...stephen wasira........
   
 9. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #9
  Sep 5, 2008
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  ...miye nina wasiwasi kuwa zile pesa (sijui 20mill $) alizoenda 'kujiombeleza' tena kule US kwa ajili ya kilimo ni kwa ajili ya kuleta confusion kutokana na yale aliyoyatamka kwenye hotuba pale Bungeni. Ya kuwa, pesa karibia kiwango kile kile zitakazo kombolewa zielekezwe kwenye kilimo. ndipo hapo watu wa upinzani walipokuja juu kuhusu hili, upinzani wao ukapambwa na CCM na ukaonekana anti-maendeleo ya wakulima.. kumbe sivyo!
   
 10. M

  Mwanagenzi JF-Expert Member

  #10
  Sep 5, 2008
  Joined: Sep 11, 2006
  Messages: 690
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  Hata mimi niliposikia USAID na AfDB wanatoa pesa kwa ajili ya wakulima kupitia CRDB machale yalinicheza...na hao jamaa wa IMF nao ndo washamsifu na kwamba kwao mjadala umekwisha! Nashangaa Lipumba anawashangaa (wafadhili wetu)sasa!!
   
 11. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #11
  Sep 5, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Kwanini wasipeleke Wizara ya Miundombinu ambako kitu kikijengwa tunaweza kukiona na kutathmini thamani yake kulingana na pesa zilizotumika? Ni vigumu sana kutathmini thamani halisi ya mazao au utafiti utaofanywa kwa kutumia pesa hizo kwenye Wizara ya Kilimo. Kama kweli wanataka kutuondolea mashaka na pesa hizi, na kama kweli zimerudishwa, wajengee barabara.....!!!!

  Ni rahisi mno kuthibitisha matumizi ya pesa hizo kama zitatumika kujengea barabara! Kwa mfano, barabara kuu zinakonda mikoani (Trunk Roads) zinatumia wastani wa Shilingi milioni 100 mpaka 150 kwa kila kilometa moja! Kwa hiyo Shilingi bilioni 60 zitajenga barabara yenye urefu usiopungua kilometa 400!!! Hii ndio njia pekee ya kutuondolea mashaka wananchi....!!!!

  Kinyume na hapo ni kiini macho tu! Inasikitisha kwamba tunaishi kwenye nchi ya viongozi wasio na uchungu kabisa!
   
 12. Bonnie1974

  Bonnie1974 JF-Expert Member

  #12
  Sep 5, 2008
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 407
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  MKUU with all due respect naomba UAMINI HIVYO.
  Msemo wa sasa wanasema HABARI NDIYO HIYO...
  Madamu Mama amekwambia mtoto huyu ni wako.TOKEA SAA ILE AMINI HIVYO,kwa manufaa ya mtoto mwenyewe na familia yako kwa ujumla mbele ya macho ya ndugu,majirani na marafiki,ingawa mzee unajua kuwa hapa napigwa changa la macho.
  Katika maisha ndugu yangu WE NEED TO LET A LOT OF THINGS GO......OR ELSE WE SHOULD GET OURSELVES READY FOR DISAPPOINTMENTS.
   
 13. RR

  RR JF-Expert Member

  #13
  Sep 5, 2008
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,717
  Likes Received: 205
  Trophy Points: 160
  Enyi kizazi cha nyoka chenye uhaba wa imani.... yaani hadi muone ndipo muamini? Acheni utomaso wenu tufanyeni kazi kwa bidii ili tuzalishe zaidi ya hizo tunazosema ziliibiwa.
  Si mlimsikia Mkuu (ambaye mlimpigia kura za kishindo, 80%) akisema kwamba fedha zimerudi na nyingine zinarudi kabla ya Octoba 31? Mnataka uthibitisho gani zaidi? Mbona mnakuwa wasumbufu kiasi hiki?
  Hamkumsikia Mkuu akisema kwamba tabasamu lake si tijara kwa mafisadi? Kwamba 'He might be wearing a smile but he is firm on issues'?
  Hamjui kwamba ana nguvu nyingi sana (alizopewa na 80% ya Watz)? Kwamba anaweza kuamuru wana JF wote wawekwe lupango na wakawekwa? Bila maswali? Lakini hizo nguvu hazifiki kwa mafisadi?
  Amini, amini nawaambieni msiporekebika na kuamini kwamba neno la Mkuu ni la mwisho basi mnaweza kupata matatizo lukuki.
   
 14. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #14
  Sep 6, 2008
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,427
  Trophy Points: 280

  AAMEN!!!!..........na iwe hivyo...

  kuna mkulu amesema hapa ingejengwa barabara kubwa ambayo wala haikuwa kwenye mipango...kwa fedha za EPA....tungefanya kama mnara wa kumuenzi kikwete ...lakini kwa hii ya kupeleka kwenye tafiti na mikopo isiyolipika....tutabaki kuzua EPA JUU YA EPA...
   
Loading...