Ni kweli mwanaume akifa bila kuacha mtoto, maiti yake uchomekwa mkaa au betri sehemu ya haja kubwa?

Mtoto Wabibi

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
451
294
Katika pita pita zangu hii leo ni mara ya pili kusikia kitu kama hiki. Kwa mara ya kwanza nilisikia katika vijiwe vyetu.Lakini leo nimeshuhudia Mjomba akimwambia mpwa wake...

" Eti mwanaume endapo anafariki bila mtoto basi maiti yake itachomekwa mkaa ( kaa la moto lililopoa) au vibettery vile vidogo sehemu ya haja kubwa".

Baada ya kumhoji zaidi huyo aliyeambiwa akasema katika tamaduni zetu za kiafrika mwanaume akifa bila mtoto ni mkosi katika ukoo kwa walio hai na hasa kwa wale watakaoitwa jina la marehemu hapo baadae.

Nimetafakari lakini sijaelewa kama kweli haya yanafanyika au ni uzushi. kwa wale wazoefu na maiti Je nini kinafanyika endapo mwanaume anakufa bila mtoto? Na kwa mwanamke je? Kama ndivyo ilivyo,

Je, si kumdharirisha marehemu kwa kumchomeka mkaa(kaa la moto lililopoa) au betri hizi ndogo sehemu ya haja kubwa?

Unaweza ukawa umekwepa ushoga lakini mara ya mwisho wanakuweka kitu kigumu.

Karibuni wadau
 
Mimi nilisikia kuwa kwa wasukuma mwanaume akifariki bila ya kuwa na mtoto wanamuwekea bunzi sehemu ya aja kubwa, naomba wajuzi watujuze
 
mila na desturi ni za kuchuja. sijui juu ya hili. lakini kama linafanyika sio sawa. hakuna laana. kykosa mtoto ni jambo la kawaida kwani mtoto ni zawadi kutoka kwa Mungu na siyo wote hupewa.
 
Hiyo ni sehemu ya mila iliyopo kwa Wachagga mpaka leo hasa wale wa vijijini ambao hawajashika dini sana ILA wanachofanya ni kumwingiza ile sehemu ya katikati ya mgomba (kipande cha mgomba)

Kuna aina flani ya mgomba una rangi flan kama ya zambarau kama si reddish kiasi.
 
Katika pita pita zangu hii leo ni mara ya pili kusikia kitu kama hiki. Kwa mara ya kwanza nilisikia katika vijiwe vyetu.Lakini leo nimeshuhudia Mjomba akimwambia mpwa wake...

" Eti mwanaume endapo anafariki bila mtoto basi maiti yake itachomekwa mkaa ( kaa la moto lililopoa) au vibettery vile vidogo sehemu ya haja kubwa".

Baada ya kumhoji zaidi huyo aliyeambiwa akasema katika tamaduni zetu za kiafrika mwanaume akifa bila mtoto ni mkosi katika ukoo kwa walio hai na hasa kwa wale watakaoitwa jina la marehemu hapo baadae.

Nimetafakari lakini sijaelewa kama kweli haya yanafanyika au ni uzushi. kwa wale wazoefu na maiti Je nini kinafanyika endapo mwanaume anakufa bila mtoto? Na kwa mwanamke je? Kama ndivyo ilivyo,

Je, si kumdharirisha marehemu kwa kumchomeka mkaa(kaa la moto lililopoa) au betri hizi ndogo sehemu ya haja kubwa?

Unaweza ukawa umekwepa ushoga lakini mara ya mwisho wanakuweka kitu kigumu.

Karibuni wadau
Sio kwa waafrika wote, sema kwa baadhi ya jamii/ makabila.

Mfano, kwa Tanzania najua Wachagga wana hiyo mila ila marehemu anaingiziwa kipande cha mgomba ikiaminika ni kufunga hiyo laana ya kutokuzaa mtoto.
 
kumbe kutokuzaa ni laana,ngoja tuchangamke daah!
 
Back
Top Bottom