Ni kweli kifo cha CUF kimetimia

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,226
3,290
Hili ni suali muhimu baada ya kilichotokea Zanzibar.

Kwa kuwa CUF haikushiriki uchaguzi wa marejeo na kule kukosa ushiriki katika serikali na Baraza la wawakilishi wengine husema ndio mwisho wao.


Wengine husema CCM itatumia mwanya huo kubadili sheria nyingi na kuanzisha NYENGINE MPYA ILI KUJILINDA NA KUZIBA NAFASI KWA CUF HAPO BAADAE.


Wengine husema ni afadhali CUf haikushiriki ili kulinda heshima yake kidunia na kulinda falsafa yake ya HAKI SAWA KWA WOTE. Wanasema hawakuwa tyari kushiriki katika BATILI.


Maoni yangu yatakuja baaadae lakini nitangulize kionjo kwa suali juu ya suali. ikiwa hivyo ndivyo jee kinyume chake ndio kusema CCM itanawiri na kukubalika zaidi Zanzibar?


Tungoje tuone.
 
Kwa Zanzibar labda wafute vyama vingi lakini si RAHISI kuwabadili watu wa Visiwani.Nje utawaona si wamoja lakini ndani ni wa moja.
 
Back
Top Bottom