sirluta
JF-Expert Member
- Nov 28, 2012
- 6,325
- 2,486
Habari za wakati huu wadau? Kwa masikitiko makubwa motor lawama kwa mbunge wangu wa Rombo profesa Adolf mkenda kwa kushindwa kumweleza raisi Samia Suluhu matatizo ya Wana Rombo. Nakumbuka ziara ya hayati magufuli mkoani manyara wilayani babati alielezwa tatizo la wananchi kutokuunganishiwa umeme kwa muda mrefu na alitatua tatizo lile ndani ya siku 3 zaidi ya wananchi 4000 wakafingiwa umeme.
Wilayani Rombo Kuna wananchi walihamasiahwa kufunga umeme tangu mradi wa REA umezaliwa mwaka 2016 kama sijakosea, wananchi hao kwakuwa waliaminiashwa umeme ni maendeleo, na warombo wanapenda maendeleo, waliuza Kila kitu hadi vyakula na mifugo ili waweze kufunga umeme. Cha ajabu mpaka Leo, wapo waliofariki hawajauona huo umeme, wapo waliobaki na nyaya ndani mpaka Leo hakuna umeme, wengine wamefuatilia mpaka wamefilisika wakifuatilia kufungiwa umeme bila mafanikio, wapo walioletewa nguzo mpaka kwenye nyumba zao lakini hawanashushiwa umeme, wapo waliopata umeme huo(wengi wao wakiwa ni matajiri) kero ya kuunganishiwa umeme kwa wananchi wa Rombo ni mojawapo ya tatizo kubwa lakini viongozi wanalitumia kama mradi wa kisiasa. Ikifika wakati wa uchaguzi ahadi za kufungiwa umeme zinakuwa nyingi na kubwa lakini uchaguzi ukishapita wananchi wanabaki na kero hiyo hiyo.
Namshangaa sana mkenda kutolisemea hili kwa mheshimiwa rais ama kwakuwa kwake na ndugu zake Kuna umeme hivyo si tatizo lake.
Mheshimiwa waziri wa nishati kaka yangu January Makamba nakujua ni mchapakazi mzuri, naomba chukua kero hii na unapoichukua tambua wahujumu wa Kwanza wa miradi hii ni watendaji wa tanesco hivyo ujue Rombo wilayani Kuna jipu la tanesco ambalo ukitaka kujua ni jipu kweli kweli, fuatilia habari zake kwa wananchi na vyanzo vingine vya habari vinavyoweza kukusaidia.
Hivi sasa Kuna habari za kusikitisha zinazoenezwa kwamba baada ya Dr Kalemani kutumbuliwa, mradi wa REA haupo tena. Inawezekana ni majipu haya haya ya Kalemani ndo yanaeneza habari hizi hivyo simama na Wana Rombo wanaoiamini serikali Yao wapate nishati hiyo adhimu kwao.
Naomba kuwasilisha.