evonik
JF-Expert Member
- Jun 12, 2015
- 3,998
- 5,150
Heshima kwenu Wakuu?
Nianze na lengo la uzi huu, utakuwa shuhuda wa hili kwamba ligi kuu nchini Ujerumani (Bundesliga) imeonekana kuwa bora na yenye ushindani ukilinganisha na ligi zingine za Ulaya, (nazungumzia Ulaya kwa sababu ndiko soka linakosikika sana) Lakini tukiangalia kwa undani Bundesliga kiukweli hakuna ushindani wowote uliopo imeshazoeleka kuwa Beyern Munich ndio wabaabe wa ligi, msimu uliopita walitwaa ubingwa wakiwa na mechi saba mkononi, leo hii kwenye msimamo wamewaacha Dortmund kwa takribani alama nane, tunapozungumzia ushindani wa ligi maana yake kwamba anayeongoza ligi awe anatofautiana na anayemfuata Walau kwa point (alama) tatu au nne sio mbaya,kama ilivo LA LIGA huko Spain au EPL, lakini kuachana Zaid ya alama nane kisha tuseme Kuna ushindani sidhani km inakuja, mfano LIGI ONE ya FRANCE sidhani kama ushindani huo unaozungunziwa upo kwa sababu anayeongoza ligi (PSG) hajawi poteza mechi hata moja ktk michezo yote 25 aliyoicheza, Tunapozungumzia ligi yenye amsha amsha, ushindani labda LA LIGA na EPL ndo Zina ngoza. mpaka sasa kutabiri mshind ni kazi, wengine Wana tabiri Tottenham ndo wataibuka mabingwa wengine Leicester, so ukiangalia KWELI Kuna ushindani ambapo kutabiri pia ni shughuli lakini Bundesliga mshind anajulikana ni Beyern, ukimuacha Dortmund huwezi kusema Schulke 04,Atabeba ndoo au Luverkusen au Mainz 05, Lakin kwa EPL naweza sema lolote linaeza tokea Arsenal, Leicester, Man City, Tottenham wanambio za kuwania ubingwa au LA LIGA Madrid, Barca au Atletico huwezi Bashir kirahisi Nani Atabeba ndo,
Labda kidogo Wakuu tusaidiane kidogo kuwa kama mtazamo huu ni sawa kwamba LIGI BORA dunian ni Bundesliga. Au pengine ni lugha ya KI biashara wanaitumia kukuza huduma zao.
Nawasilisha Wakuu karibun!!!!!!!!!!