Ni kweli au ana tatizo hataki kusema?

Mbochong'a

JF-Expert Member
May 2, 2011
759
1,293
Habari ladies and gentlemen, hope mko vizuri. Ok. Moja kwa moja kwenye mada. Ni hivi, miaka kama minne nyuma kuna binti alikuja kufanya field kazini kwetu kipindi hicho mimi ndio nilikuwa nina mwaka hapo job tangu niajiriwe. Basi binti alikuwa mwaka wa pili ni binti flani mpole na maadili flani ya kilokole then ni mzuri yaani wife material kabisa.

Basi fresh akawa pale tunamfundisha kazi za hapa na pale mpaka akamaliza field yake vizuri, tulikuwa tupo vizuri tu kawaida tunaheshimiana na mpaka anaondoka sikuwahi kumtongoza wala kuchukuwa namba zake. Then ikapita kama mwaka hivi kuna siku nikakutana nae maeneo ya town tukasalimiana vizuri na ndio ulikuwa mwanzo wa kuchukuwa namba. Then tuka agana kila mtu akasepa na njia zake.

Then kama kawaida kwa mtoto wa kiume ukichukuwa namba ya binti. Nikawa nachat nae sana tu mpaka nikamtongoza. Hapo sasa shida ilipoanzia. Binti amekubali vizuri, lakini anasema yeye kupatikana kwake ni kwa shida sana na sijui kama nitaweza kuvumilia. Kwa sababu mkishakuwa wapenzi lazima kuwe na ukaribu.

Nikawa nipo curious sana kujua kwa nini kupatikana kwake ni kwa shida na ukizingatia ni binti mkubwa tu na ameshamaliza chuo. Basi kweli bwana me nikamkubalia nikamwambia fresh tu nitakuvumilia. Nikamwambia vipi nataka tuonane, coz anaishi Kigamboni halafu mimi niko huku njia ya Moro road kwa wachaga! Mtoto akaniambia mimi bwana kuonana inatakiwa sehemu ambayo sio nyumbani wala bar. Nikamwambia wapi sasa? Akasema sehemu nzuri ni Sunrise beach kule Mjemwema Kigamboni. Me nikamwambia fresh haina noma. Tukapanga siku ya kwenda freesh kabisa.

Kweli tukaenda Sunrise tukapunga upepo na kupiga story za hapa na pale. Kumbuka hiyo ndio ilikuwa first time kukutana baada ya kutongozana kwenye simu. Basi manzi akaniambia jinsi anavyoishi kwao kuwa yuko bize sana na huwa hapatagi kabisa muda wa kutoka toka home imepelekea yeye kuwa single kwa maana hakuna mwanaume ambae anaweza kumvumilia.

Basi kweli aisee na mimi nikaanza ku- experience yale mambo aliyokuwa akiniambia. Coz kila nikimwambia aje home anasema hawezi kuja kwa sababu ya home kwao wanambana. Nikamuuliza wanakubanaje na wewe ni binti mkubwa hivyo!? It means huwezi hata kuwaambia unaenda kwa rafiki yako? Basi binti hana hata majibu ya maana anazingua tu. Kuna siku nilikuwa nimelewa nikampigia simu nikamchana sanaaa ilifikia point nikamwambia sikutaki demu gani unakuwa kama mtoto. Kesho yake akanipigia akaniambia naona jana ulienda kunilewea ili unipe ukweli wangu. Basi mzee nikawa naomba msamaha manzi akagoma kunisamehe na akasema anaomba mahusiano yaishe.

Kweli mzee baba ikabidi ni move on. Sasa yule binti namba yangu alikuwa hafuti.. anakaa ikipita kama mwezi hivi ananitafuta tunachata then naanza upya kumtongoza but anakuwa anakumbushia yale maneno niliyomwambiaga then tunaishia hapo. Kuna kipindi tulikaa kimya kama mwaka hivi. Akanitafuta tena. Then kama kawaida nikatongoza tena.

Safari hii nimejaribu kumkomalia na kumwambia me nitakubali kuwa nawe na hayo mazingira magumu ya kwenu. Binti anakubali but ananiambia mazingira bado ni yale yale ya kutopatikana coz kwao bado wanambana.

Sasa wanazengo me nashindwa kumuelewa huyu binti. Ni kweli anabanwa au ana matatizo flani hataki kuniambia. Kwa sababu mpaka sasa hivi nahisi ana kama miaka 28+ but ndio kama hivyo haeleweki. Je huyu binti anaweza akawa na shida gani?

Ni hayo tu watu wangu.
 
Kwamba wewe ni kidumu.. 🤣 🤣

Mimi nahisi anapenda kuwa kwenye uhusiano,bali ana vigezo vyake ambavyo wewe hujavi meet...so kakuweka Pending..akikosa kabisa ataolewa na wewe,ila akitokea mtu wa vigezo vyake ujue utabwagwa au kuwa cheated on...
 
kuna kitu kinaitwa barua tomb@ we peleka tu kwao watakuwa wanamruhusu wenyewe aje kwako
 
Sasa huyo ndio mke wakuweka ndani wee unataka demu ukigosa tuu tayari kaleta paphchi gheto unajigegedea hahahaba

Sii umesema mwenyewe kuwa ni wife material nenda mpaka kwao mzee utangaze nia.
 
Kwamba wewe ni kidumu.. 🤣 🤣

Mimi nahisi anapenda kuwa kwenye uhusiano,bali ana vigezo vyake ambavyo wewe hujavi meet...so kakuweka Pending..akikosa kabisa ataolewa na wewe,ila akitokea mtu wa vigezo vyake ujue utabwagwa au kuwa cheated on...

Siendelei kusoma coment zingine hapa ushamaliza kila kitu , yan yeye ajiongeze mwenyewe.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Hapo unapigwa changa la macho tu jombii. Kuna baharia anamiliki zaga hilo wewe huyo mamsii anakunare nare tu.

Ukiona amekuvungia mda akakutafuta ujue labda wameleteana na huyo mjuba wake anakufanya kama sehemu yake ya kujiliwaza tu wakielewana anaamsha zake.
 
Kwamba wewe ni kidumu.. 🤣 🤣

Mimi nahisi anapenda kuwa kwenye uhusiano,bali ana vigezo vyake ambavyo wewe hujavi meet...so kakuweka Pending..akikosa kabisa ataolewa na wewe,ila akitokea mtu wa vigezo vyake ujue utabwagwa au kuwa cheated on...

Mwaka wa tatu huu mtu wa 28+ hajaliwa na mtu kwamba anabanwa ? aisee kuna fala anakula huo mzigo kimasihara. Nlikuwaga na kitoto ivyo ivyo kinanichengua kinoma, sasa nikakibembeleza kila aina kikaja gheto/ home kilivyokuja kikawa kinashangaa shangaa alafu me nikamfanyia makusudi sikumrarua, kaenda kwao kila saa I miss u baby nikamwacha mwenyewe aniletee kishindu chake nicheze nacho, wanawake wana mambo yao usipoyajua utahangaika sana.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kweli mkuu.. ngoja nitambae zangu mdogo mdogo
Hapo unapigwa changa la macho tu jombii. Kuna baharia anamiliki zaga hilo wewe huyo mamsii anakunare nare tu.

Ukiona amekuvungia mda akakutafuta ujue labda wameleteana na huyo mjuba wake anakufanya kama sehemu yake ya kujiliwaza tu wakielewana anaamsha zake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwaka wa tatu huu mtu wa 28+ hajaliwa na mtu kwamba anabanwa ? aisee kuna fala anakula huo mzigo kimasihara. Nlikuwaga na kitoto ivyo ivyo kinanichengua kinoma, sasa nikakibembeleza kila aina kikaja gheto/ home kilivyokuja kikawa kinashangaa shangaa alafu me nikamfanyia makusudi sikumrarua, kaenda kwao kila saa I miss u baby nikamwacha mwenyewe aniletee kishindu chake nicheze nacho, wanawake wana mambo yao usipoyajua utahangaika sana.

Sent from my iPhone using JamiiForums
Ndio hivyo mkuu. Pasua kichwa sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom