Ni kwanini wanawake wanakuwa na shauku sana wanapovalishwa pete za uchumba?

barafuyamoto

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
32,324
29,587
Habari zenu,

Kama kichwa cha habari kisemavyo,

Nimekuja tambua kuwa wanawake wanaovalishwa pete za uchumba wanakuwa na 'furaha' sana, unawakuta mitaani ananyoosha kidole chake kuhakikisha pete ya uchumba inaonekana.

Au hata kama hawajaulizwa, akikutana na mtu ambaye alikuwa hajui kuwa kavalishwa pete basi ni lazima atamwambia.

Kwenye status zao mitandao ya kijamii kama whatsapp, instagram, twitter ni fujo tupu.

Status zimejaa sura za 'furaha' zikiambatana na pete za uchumba, pia ni full kupongezana kwa kina dada, HONGERA KWA HATUA ULIYOFIKIA na vitu kama hivyo, kuna wanawake wengine pia wanawalingishia wenzao kuwa wamevalishwa pete.

Je sababu ya hizi 'furaha' ni nini haswa maana ni tofauti na wanaume, mwanaume anayekuwa kamvalisha pete mwanamke wala haangaiki kufahamisha watu kama wanawake.
 
kwani huko kwenu ulipo wanawachukuliaje wanawake wasio na waume lakini wamezaa wanaishi wenyewe?

na wale waliolewa wanaishi na waume wanachukuliwaje kwa ujumla?
Kwa hiyo furaha yao ni uwezekano wa kutokuwa single parents??
 
Ni kwasababu hawajui ndoa ni nini hasa ndio maana hufurahi kupita kiasi,ila wengi wao baada ya ndoa furaha zao hubadilika na kua mateso coz wanakua hawakujiandaa kisaikolojia kua ndoa ina up & down,

Wanaume wanachukulia ni kawaida tu coz wengi wao wanatambua kua wameingia kwenye level nyingine ya maisha yaani kifupi ni kwamba wamejiongezea majukumu mengine ya ziada.
 
Wanawake siku zote ni watu wa kupenda matukio tu kwao ndio furaha... cku hizi unaona mapicha shughuli ya pete ya uchumba utadhani ndoa,watu na sare wanavaa
 
Back
Top Bottom