Ni kwanini Upinzani umeshuka katika Kanda ya Ziwa na Kaskazini?

MSELA WA MANZESE

JF-Expert Member
Apr 22, 2017
1,606
2,000
Nimejaribu kufatilia kiwango cha
Upinzani katika kanda ya kaskazini
Na kanda ya ziwa umeshuka katika
Kiwango cha juu

Nimezungumza hivyo baada ya kuvuta picha hali ya kisiasa miaka
Kumi na mbili ilivyokuwa kuanzia
2005 hadi 2015 hadi sasa tulipofikia.

Kwa Wale wenye kumbukumbu vizuli mtakumbuka vuguvugu la
Mabadiliko na maandamano ilkfikia hatua ukipanda daladala
Unaisifia ccm unashushwa .

Kwa Wale mliowahi Kuishi
Arusha mtakumbuka kipindi
Lema alivyovuliwa ubunge na
Alivyowekwa ndani arusha ililipuka
Kwa maandamano watu walipigwa
Kweliii sio hivo tuu Arusha .

Kwa Wale wanaokumbuka machafuko ya arusha hali ilikuwa
Tete sana na kwa wale wanaokumbuka uchaguzi wa
Marudio arumeru mashariki mliona
Jinsi Nassari alivyoshinda jimbo
La arumeru.

Kanda ya ziwa kwa Wale mnaokumbuka maandamano
Ya vuguvugu la mabadiliko ya
Lililomtoa Masha na diallo uchaguzi Mkuu 2010 jinsi gani
Ilivyokuwa hadi mwanza ikalipuka
Watu walivyopambana

Ni mengi ya kuzungumzia ila tukirudi katika ukweli ukiangalia
Uchaguzi marudio wa kata 22 na
43 mwaka huu ambazo ccm wameshinda kwa kishindo na wapinzani wametulia wamekubali
Matokeo ni dhahiri tukubaliane
Upinzani umeangukaa.

Enzi zilee chaguzi Kama hizi ni
Lazima itokee patashika kati
Upinzani na ccm na ni lazima
Zipigwe kweli kwelii lakini tukirudi
Katika mada ya msingi upinzani
Umeanguka au ume drop .

Je tatizo ni nini haswaa?
 

imhotep

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
24,652
2,000
Kwa Wale wenye kumbukumbu vizuli mtakumbuka vuguvugu la
Mabadiliko na maandamano ilkfikia hatua ukipanda daladala
Unaisifia ccm unashushwa
Au unapokea kipigo kabisa,hata kutembea umevaa nguo za chama ilikuwa unapigwa mawe.
 

Crimea

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
13,529
2,000
Wanategemea hisani ya ccm kufanya siasa! Yani eti ccm wakisema hakuna siasa na wao wanaufyata!
 

MSELA WA MANZESE

JF-Expert Member
Apr 22, 2017
1,606
2,000
Toa ujinga wako hapa, utumie polisi na tume kushinda alafu useme upinzani umeshuka?
Kuna vitu inabidi tukubaliane kusema kweliii .

Ivi kipindi akina lema na nassari
Mpaka wanashinda majimbo ya
Arumeru na Arusha.

Unataka kuniambia polisi walikuwa hawatumiki.
 

Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
38,343
2,000
Kuna vitu inabidi tukubaliane kusema kweliii .

Ivi kipindi akina lema na nassari
Mpaka wanashinda majimbo ya
Arumeru na Arusha.

Unataka kuniambia polisi walikuwa hawatumiki.
Kwa hiyo unajifanya kipofu? watu wanapigwa mpaka wanavunjwa na wanakamatwa hovyo au kwa vile upo CCM unaona kila kitu ni sawa? kumbuka hata Mugambe alikuwa anashinda kwa 99% lakini hao hao walimtoa.
 

jiwe la majiwe

JF-Expert Member
Sep 18, 2016
2,539
2,000
Nimejaribu kuangalia harakati
Za kisiasa enzi zilee na hadi sasa
Huo utafiti wako umekaa kiccm kwasababu umeamua kijitoa ufahamu kabisaaaaa....!!!!!!

Wewe unanyima shughuli za chama ambazo ziko kikatiba alafu unasema upinzani umeshuka..???

Wewe unatumia dola kushinda chaguzi alafu unasema upizani umeshuka...????

Wewe unabambikiza watu kesi alafu unasema upinzani umeshuka..???

Watu wanapotea/wanaumizwa kwa kusema kweli alafu unasema upinzani umeshuka..???
 

MSELA WA MANZESE

JF-Expert Member
Apr 22, 2017
1,606
2,000
utafiti wako chaka huo...
Chakaaa kivipi wakati ccm inashinda kanda ya kaskazini
Na kanda ya ziwa ambazo ndio
Ngome kuu ya upinzani

Ushindi wa kata 43 ni lazima upinzani tujiulize ivi imekuwaje
Tumepoteza na ndio ngomee

Kuu mbona miaka ya zamani
Piga uaaa ni lazima upinzani
Ushinde
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom