Baba Jotham
Member
- Mar 6, 2012
- 84
- 40
Mara nyingi wengi wetu tumekaa tukisubiri kuja kwa fursa katika maisha yetu, lakini je ni sahihi kukaa (kubweteka) kusubiri kuja kwa fursa ? Jibu langu - HAPANA. Lakini pia ikumbukwe kwamba kama binadamu unayejielewa hauwezi kuishi kwa kutegemea bahati, (Wengi wetu utawasikia Sina bahati). Kwanini unataka kuwa tegemezi wa bahati?. Tambua unapaswa kuwa tegemezi kwa nafsi yako wewe mwenyewe.
Watu wengi wamekosa Fursa ni kwasababu hawana au wamekosa uwezo wa kutambua fursa mbali mbali zinazojitokeza. Ikumbukwe, Siku zote kutakuwa na fursa kwa wale ambao wameweza kutambua fursa na kuzichukua au kujiingiza katika hizo fursa.
NI KWANINI UKAE UKISUBIRI FURSA? TENGENEZA FURSA ZAKO MWENYEWE KWA KUFANYA HAYA YAFUATAYO
Tambua mipaka yako - Huwezi kuwa mkamilifu. Huwezi kufanya kila kitu mwenyewe. Huwezi kujenga biashara au kuishi maisha ya ndoto yako au kufanya mengi ya fedha kama haujaweza kujua udhaifu wako , uwezo na tamaa zako . Kama unajua mipaka yako na upi ni uwezo wako ,utakuwa kwenye nafasi nzur ya kujua hasa ni nini unahitaji.Pia,kujijua na kugundua udhaifu wako kunakupa nafasi ya kuujaza udhaifu wako kwa kutumia uimara wa watu wengine
Fungua macho yako. Kuna mengi zaidi yanatokea katika ulimwengu kuliko ambavyo unavyoweza kuona. Acha kusikiliza muziki wakati wote, UNAPASWA KUJICHANGANYA NA WENZAKO KUJIFUNZA ZAID. Hauwez jua labda kuna mtu ambaye anaweza kubadilisha maisha yako kwa namna moja ama nyingine. Hauwez jua labda mtu aliyeketi karibu na wewe kwenye daradara na penginepo ni biashara yako ijayo,mpenzi,mume wako / mke,au rafiki yako mpya bora. Hauwez jua, maisha hayatabirik, hivyo unapaswa daima kuweka macho yako wazi . Unaweza kuzikosa fursa kwa sababu tu wewe upo busy sana kusikiliza iPod yako au hiyo subwoofer yako ukizisubir fursa/bahati. Fungua macho yako,jifunze ata kunywa kahawa , au kutembea kwa miguu kurudi nyumbani ili kuapata fursa ya kujifunza mawazo mapya.
Usiogope kuuliza. - Usiogope ! Hakuna aibu kutokujua kitu, na hakuna aibu kuhoji jambo ili kujifunza.Kuna jamaa yangu alipata kazi kampuni A kwa kuuliza tu jambo X. Alimuliza meneja kama anaweza akapata nafasi ya kufanya kazi na hiyo kampuni A,kilichotokea meneja akamuhoji kidogo na kugundua ni mtu sahii kwake akampatia kazi.Kiufupi ni kwamba amepata kazi kwenye kampuni ambayo haikutangaza kazi ila kuuliza kwake kumempa fursa ambayo asingeipata kama angeisubir
Jenga kujiamini- Unapaswa kuwa jasiri ili watu wakuamini . Hiyo unahitaji kujiamini na kujenga ujasir 120% kwa kile unachokidhamiria.Kumbuka watu wengi huwafuata viongozi wao hata wakati ambao viongozi hao hufanya maamuzi mabaya ,lakini wanawafuata kwa sababu ya imani na status ambazo wamezijenga viongozi hao. Hivyo basi kama unaweza kujenga kujiamini na ujasir unaweza kufanya watu kukufuata na kukuamini hivyo kuweza kupata kujenga fursa nyingi zaid kwa ajili yako/kampuni yako/au sehemu yako ya kazi
Endelea kujifunza .- Kujifunza ni mchakato ambao hauna mwisho . Daima unaweza kujifunza kitu kipya. Daima dumisha mtazamo wa kuwa mwanafunzi wa mambo mapya ili kujenga fursa nyingi zaid. Kama unafikiri imetosha kujifunza basi jua unajikwamisha , lakini kama una mengi ya kufanikiwa katika maisha yako , katika nyanja zote,basi jua unapaswa kujifunza mambo mapya kila siku.
Mwisho,tambua kamwe hauwezi kupata fursa kwa kukaa na kuangalia TV siku zote au kusikiliza mziki kwenye ipad yako kila siku. Nenda nje kajichanganye , jenga hisia na tazama watu wanachofanya na kujifunza then jitengenezee fursa katika maisha yako. Kama wewe ni mtu active na mwenye mitazamo chanya basi jua mara zote utaishia mahali sahihi katika wakati sahihi.
Asanteni
NB: Kiswahili ni lugha yetu,naomba mnisamehe kama kuna sehemu nimechapia maana hii lugha nayo unaweza ukasema kura kumbe kula,unaweza ukasema kurara kumbe kulala teh teh teh teh teh HAPPY KARUME DAY