Ni kwanini Final za Uefa champion league zisionyeshwe kijazi interchange?

menny terry

JF-Expert Member
Mar 18, 2011
509
667
Wakuu,

Tarehe 28 kutakuwa Na fainali za UEFA champion league Na tukio hilo litaonyeshwa pale Tanzanite bridge sambamba Na filamu ya Royal Tour! Ni jambo zuri sana Ila mtazamo wangu kwanini wasingetumia pale Kijazi interchange? Maana kuna ile sehemu ya mwendokasi ambayo ni kubwa sana Na haijaanza kutumika mpaka sasa kuliko kulifunga DARAJA la Tanzanite kwa muda wote wa mechi.

Nawasilisha.

Sawa tumechukua maoni yako na tupo katika mchakato wa kuhamisha tukio hilo kutoka Tanzanite Bridge na kulipeleka Kijazi interchange

Tunajivunia kuwa wananchi wenye maoni mazuri kama ww na hii inatupa urahisi sisi viongozi ktk kuwaongoza vzr

Ahsante
 
Mkuu siku hio Tanzanite bridge watalifunga watu watatumia old selander bridge. Sasa Kijazi ukiifunga itakuwaje siku hio? Au waangalie mpira pale katikati huku magari yanapita pembeni yao? Kutakuwa na usalama hapo? Halafu walengwa wengi wa hilo tukio wanatoka upande wa Tanzanite.
 
Mkuu hii taarifa ni ya ukweli?
 
Mkuu siku hio Tanzanite bridge watalifunga watu watatumia old selander bridge. Sasa Kijazi ukiifunga itakuwaje siku hio? Au waangalie mpira pale katikati huku magari yanapita pembeni yao? Kutakuwa na usalama hapo? Halafu walengwa wengi wa hilo tukio wanatoka upande wa Tanzanite.
Mkuu kwahyo sisi wa mbagala sio walengwa?

Hata hivyo tutazamia tu hapo chap kwa haraka.
 
yaani upige party katikati ya barabara na huku magari yakiendelea kupita huko pembeni kua serious mkuu
 
Mkuu siku hio Tanzanite bridge watalifunga watu watatumia old selander bridge. Sasa Kijazi ukiifunga itakuwaje siku hio? Au waangalie mpira pale katikati huku magari yanapita pembeni yao? Kutakuwa na usalama hapo? Halafu walengwa wengi wa hilo tukio wanatoka upande wa Tanzanite.
Magari si yatapita chini kwenye mataa. Sioni shida yoyote
 
Tatizo nyie wa mbagala mnakunywa serengeti light wakati walengwa wa hii kitu ni wanywaji wa Heineken
Hizo serengeti ni premium kwetu mkuu. Huwa tunakunywa tukiwa na hela nyingi.
Kikawaida ni k vant ili tulewe haraka mambo yasiwe mengi.
 
Sawa tumechukua maoni yako na tupo katika mchakato wa kuhamisha tukio hilo kutoka Tanzanite Bridge na kulipeleka Kijazi interchange

Tunajivunia kuwa wananchi wenye maoni mazuri kama ww na hii inatupa urahisi sisi viongozi ktk kuwaongoza vzr

Ahsante
Izi id fake tutajuaje Kama unayoyaahidi Ni kweli yatafanyika na kweli ww Ni kiongoz?
 
Pale kijaz hapafai maana ina movement ya magari muda wote so waache Kulekule Tanzanite ili game ikiisha tunashuka zetu coco kumalizia. Usiku uliobaki
 
Back
Top Bottom