Ni kwanini anatumia sana hili neno "mbona"?

The Hidden

JF-Expert Member
Mar 26, 2017
246
102
Ndugu wanaJF habarini,

Niko na mchumba wangu ambaye kiukweli tumedumu kwa miaka kadhaa mpaka pale ambapo alijaribu kutikisa na mimi nikachukulia serious, nikavuta mchuma mwingine lakini baada ya kutambua hivo, aliumia sana na akaonesha bado ananipenda hivyo nilimpokea na kwa kuwa huyu mwingine tulikuwa hatujafika mbali sana ilikuwa rahisi kumwambia aendelee tu na maisha yake, nikamrudia huyu mchumba wangu.

Sasa wanaJF, ana vijitabia tabia vya ugomvi ugomvi but namvumilia tu nazidi kumkanya lakini pia amekuwa na tabia akikosea tu nikimwambia anatafuta nilichowahi mkosea huko nyuma anasema "mbona'' wewe ulifanya hivi na vile" hasa, lile la kuvuta mchuma mwingine analirudia kila wakati na wakati alidai amesamehe.

Sasa wakuu, hii tabia ni ya kawaida kwa wasichana, au ni tabia yake tu? Na je hii tabia naweza idhibiti vipi na je anaweza kuja nisaliti akasema "mbona ulivuta mchuma mwingine?" Au ni maneno tu ya wanawake?

Ahsanteni wakuu!
 
Hakuna cha maneno ya wanawake she mean what she say....huyo ni kichaa cha panya buku:D:D:D:D
 
Ulipo mwacha ukaenda na mwingine kisha ukarudi tena kwake, ndio chanzo cha hayo yote.
1: Anaona wewe huna msimamo na huwezi fanya lolote baya kwake.

2: Anachukulia tukio la mwanzo kama kitisho tu na hukupania kumwacha

3: Kitendo cha kumrudia ni kama mchezaji aliyejihakikishia namba hata kama akiwa majeruhi.
Jaribu kuongea nae na umwambie akue na awe Kama mwamke na sio kifanya mambo ya kufanywa na watoto.

Ila kama mpo chini ya 25 yrs sio makosa yenu, ni umri unayaruhusu hayo kutokea
 
Miaka 24 bro ni mtoto kweli?
 
Lakini si ulifanya kweli hivyo wacha akuulize tu kwani haukuwa na sababu ya kuhangaika kumbe huyo bado alikuwa anakufaa.

Pia sio vibaya ukamuelewesha kwa kuwa unaiyona ni tabia isiyofaa ili aweze kubadilika.
 
sepa 2 mkuu, lolote baya atakalokufanyia anahic ana haki na ukimlaumu anajua kicngizio anacho, na kinaanzia na "mbona"
 
Ukisepa kwa mwingine usirudi kwa yule wa zamani, kwani kufanya hivyo ni kiburi cha kwamba yeye ni bora sana kuliko wengine. Haukutakiwa kumrudia kwa hali yoyote ile. Sitaki kuwaachanisha but kama mmesharudiana vumilianeni tu.
 
Yaani Mimi mwanaume ukiniacha ukaenda pengine ukirudi nakutoa berenge..
Sasa hapo ujue na yeye anachepuka kukulipa.
Sisi huwaga tuna malipizi ya chini chini
 
Yaani Mimi mwanaume ukiniacha ukaenda pengine ukirudi nakutoa berenge..
Sasa hapo ujue na yeye anachepuka kukulipa.
Sisi huwaga tuna malipizi ya chini chini
Kwani nilirudi au alirudi? na hayo malipizi endelea nayo sana ila najua si kwa mwanamke anayejielewa
 
Back
Top Bottom