Ni kwa nini wanaume hupiga wanawake? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni kwa nini wanaume hupiga wanawake?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mzee Kibiongo, Mar 23, 2010.

 1. M

  Mzee Kibiongo JF-Expert Member

  #1
  Mar 23, 2010
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 241
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimewahi kufanya uchunguzi kwa binadamu, wanyama na ndege kuhusu mahusiano ya jinsia ya kike na kiume na sikuwahi kona wanyama wala ndege wa kiume akipigana na mwenzake wa jinsia ya kike, hilo halina ubishi. Lakini nikabaini kwamba ni binadamu tu wa kiume yaani wanaume hupiga wanawake tofauti na wanyam na ndege. Kwa kweli sikupata jibu.

  Je, wanaume (binadamu) ni katili ?
  Wanawake ni wachokozi ?
  Je, binadamu kakosa busara hata anazidiwa na wanyama na ndege ?
  Je, kuna jinsia imesahau wajibu wake wa jinsia yake ?
  Je, sababu ni nini ?

  Naomba wana JF mnisaidie.

  Mzee Kibiongo - Nisaidieni nisije nikazidi kupinda kwa kibiongo changu.
   
 2. bht

  bht JF-Expert Member

  #2
  Mar 23, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  huwa nikisikia wanandoa/watu wenye mahusiano ya mapenzi wamepigana nahisi ni ma-primitive tu
  hakuna njia nyingine ya kumalizana mpaka mdundane.....
  watu wa mara hapa ni exceptional case
   
 3. father-xmas

  father-xmas JF-Expert Member

  #3
  Mar 23, 2010
  Joined: Mar 23, 2010
  Messages: 530
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  mwanaume si kiumbe katili lkn unapompiga demu huo ndio ukatili unapokuja.
  ngumi si suluhisho!
   
 4. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #4
  Mar 23, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  na wanawake pia huwa wanawapiga wanaume ......au hamjawahi sikio hiyo?
   
 5. M

  Mzee Kibiongo JF-Expert Member

  #5
  Mar 23, 2010
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 241
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ina maana ndege na wanyama wanawazidi wanadamu - akili, busara, hekima, upendo nk.?
   
 6. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #6
  Mar 23, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Mkorofi ni lazima apewe displin- ni kawaida.
  Ukiona wanawake wanadundwa uweke question mark...WHY??
  Wanawake ni wakorofi sana jameni....KAENI NAO KWA AKILI!
   
 7. N

  Nameless- Member

  #7
  Mar 23, 2010
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inakuwaje pale mkorofi anapokuwa ndo mwenye miguvu? 'displin' yake ni nini?
  Mwanamume mjanja habondi mkewe, na mke mjanja hapigwi, ni kila mmoja kusimama ktk zamu yake. Nnachojua kwa Wakristo waume wanaagizwa kuwapenda wake zao, na Wanawake wanaagizwa Kuwatii waume zao...Hivi vitu 2 vikibalance hakuna kipigo
   
 8. Who Cares?

  Who Cares? JF-Expert Member

  #8
  Mar 23, 2010
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 3,465
  Likes Received: 1,950
  Trophy Points: 280
  hili suala ni gumu sana...hii ni ukosefu wa njia mbadala za kutuliza hasira zako (mwanaume) hasa unapokuwa umeudhiwa na mwanamke...na hii ni very common kwetu huku wa-africa au "black race"...ndio...si unaona chriss bizzo na rihana..

  wenzetu weupe wakiudhiwa na wapenzi wao/wake/waume zao humaliza hasira zao kwa kuvunja vitu vya ndani kesho wananunua vingine..sie kibongobongo hatuna hata tv wala vyombo vya kuvunja unaamua kumvunjilia mbali mpenzi wako ili hasira zitulie kisha kesho unampeleka mke hospital kwa matibabu...

  i wish kila nyumba ingekuwa na punching bag ili baba au mama akikasirishwa na mke/mme analipiga migumi mateke na bakora nyingi sanaaaaa mpaka hasira ziishe....POLENI SANA WAHANGA WA MAGOMVI KWENYE MAHUSIANO...badilini njia ya ku-control hasira zenu pindi mnapoudhiana...NI MAONI TUU
   
 9. Sydney

  Sydney Senior Member

  #9
  Mar 23, 2010
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 154
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mwanaume anayepiga mkewe ni kwasababu yeye mwenyewe kalelewa kwenye mazingira hayo hayo, yaani baba yake alikuwa hatumii ngumi tuu kwa mama yake na sio busara kutatua tatizo kati yao. Na mtoto naye akikua hata kama kaelimika vipi hiyo inakuwepo kwenye damu tayari!
   
 10. Noname

  Noname JF-Expert Member

  #10
  Mar 23, 2010
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 1,269
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  kupiga sio discipline Jimmy thats called abusing... nikiona mwanaume anadunda mwanamke I lose respect on him... man who hit woman is psycho. kweli wanawake wakorofi lakini sio kupigana bana... there are many ways kumkomesha mwanamke mkorofi.
   
 11. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #11
  Mar 23, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  hebu tusaidie mifano ya hizo mbinu ndugu........... will appreciate that........
   
 12. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #12
  Mar 23, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  nafikiri kupigana ni kiashiria ingine kuwa binadamu ni supa kuliko viumbe vingine................ ni uthibitisho mwingine wa kuwa na utashi tofauti na viumbe vingine visivyo na utashi............. ni utashi huu ndio unaopelekea kuanzisha cause-effect relationship........... akapata punisment (cause) leads to discipline (effect)...... uwezo ambo wanyama wengine hawana........... so it proves the superioriy of man over other species...............
   
 13. Noname

  Noname JF-Expert Member

  #13
  Mar 23, 2010
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 1,269
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  okay... inategemea mwanamke anaukorofi gani... lets take example mwanamke ambaye hasikii maneno ya mme wake au ni fedhuli hajui kuongea maneno mazuri na mme wake... this is what man should do... abandon her, leave her alone in the bed, and if she wanna talk to u dont listen to her...... criticize her on her behavior till she realise that next time u r not taking no shit from her...
   
 14. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #14
  Mar 23, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  ok.... that can work at least for you............... you knw everyonr is unique, this may work to you or to some in your category ........... baadhi ya makofi yaliyoo kwenye ndoa hutokea kama ajali tu, si mpango madhubuti wa discilining.......

  chukulia mtu mwenye chumba kimoja a kitanda kimpja........... akimu-abandon wife aende kulala wapi?............. suppose there is a serious case to urgue na tena yaweza kuwa time bound, ukiamua kumnunia waht will be the outcome ............. halafu kucrticise mfululizo nako inategemea her belief in what you criticise......... if it is deep rooted, hata ungrcriticise unatoa machozi ya damu it may not work..........

  jamani........ life ccant be programmed......................
   
 15. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #15
  Mar 23, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,499
  Likes Received: 1,070
  Trophy Points: 280
  Wako baadhi ya wanawake ni kama wanatamani na wanaombwa kupigwa, ni wabishi, mdomo kwa saaana!
  Kofi moja la nguvu siyo mbaya.
   
 16. Penny

  Penny JF-Expert Member

  #16
  Mar 23, 2010
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 577
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Dear, sasa huoni hapo ndio unamfungulia milango mwenyewe na mikono yako yote miwili. Mimi kwa maoni yangu nadhani ili mwanamke awe discipline, just take him somewhere nice for a dinning, then baada ya kushiba anza kuongea naye kwa utaratibu na kwa heshima zote huku ukimweleza ni nini hasa kinachokukera ktk tabia zake, na pia muombe akueleze ni nini asichopenda ktk tabia zako. Then muonge, kisha muonge na tena muonge mpaka mfikie solution. Thereafter kama bado kutakuwa na tabia hiyo hiyo...one can take action anavyopenda mwenyewe kama nikumuacha au kurudisha kwa familia yake.
   
 17. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #17
  Mar 23, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  jamani mna-assume kuwa kila mtu ana uwezo kama wenu!!!!!!!!!........... kuweni fair jamani kuna watu hata inapita siku mbili hajui mkono utaendaje kinywani............. sas ahizo hela za outing kila siku ya kutoelewana atatoa wapi............... leteni viable soltion at least that cuts acress different categories of people.......... tena unasema shibe jamani jitahidini kujua na kujali wenzenu wanaishije............ kwa wengine ushauri kama huu ni ghali zaidi ya talaka...................
   
 18. Penny

  Penny JF-Expert Member

  #18
  Mar 23, 2010
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 577
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Ok ndugu, wanaweza kuchukua vigoda chumbani mwao, then wachukue meza ile ya pembeni ndogo waiweke katikati yao na kibatari kiwakacho juu ya meza then waanze kuelezana.
   
 19. Noname

  Noname JF-Expert Member

  #19
  Mar 23, 2010
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 1,269
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  milango ya kufanya nini?
  unamchukua dinner? yani mtu kaku udhi halafu unamchukua out mbona haiendi .... .. first I will make it clear to her/him that what she/he has done was unacceptable and I am not gonna tolerate it and if she doesnt apologize then if there was an outing then I will cancel it... if there is one bed then I will sleep another side... I will pretend like he/she dont exist in my world.
   
 20. Noname

  Noname JF-Expert Member

  #20
  Mar 23, 2010
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 1,269
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  ok Akili kofi la accident likiwa halija acha any marks then she might deserve it... lakini sio kudundana jamani... duh..

  now that why i said inategemea na ugomvi nanikatoa mfano kama mwanamke akiwa hasikii maneno ya mme wake au fedhuli then he has to make her realize that he will not entertain that kind of behavior.. sasa kama kuna serious issue and need to be discussed then it has to be discussed...

  na kama kuna chumba kimoja na one bed.. then I will sleep another side, no cuddling like everyday, no goodnight kiss...nothing... :) I think if she is a good woman and love her husband she will realize.. if you love someone u wouldnt wanna see them hurt or u wouldnt be okay with him not talking to u... u know what I am saying?... but if there is no love no passion no intimacy then marriage life will not be easy...
   
Loading...