Ni "kuapiza" au "Kuapisha" ?

Steve Dii

JF-Expert Member
Jun 25, 2007
6,402
1,254
Lipi au yapi ni sahihi katika sentensi zifuatazo, naomba msaada kufahamu matumizi fasaha tafadhali.

--- Waziri ameapishwa na Rais
--- Waziri ameapizwa na Rais

--- Waziri atamwapisha katibu wake
--- Waziri atamwapiza katibu wake

Akhsanteni.

SteveD.
 
Yote sawa.
Hakuna haja ya complication SteveD
 
Kuapisha ni kumfanya mtu ale kiapo. Kuapiza ni kumtakia mtu mabaya.

Rais haapizi mawaziri bali anawaapisha. Kuna wazee wanaoapiza watoto wao kama hawawatendei haki.
 
Kuapisha ni kumfanya mtu ale kiapo. Kuapiza ni kumtakia mtu mabaya.

Rais haapizi mawaziri bali anawaapisha. Kuna wazee wanaoapiza watoto wao kama hawawatendei haki.

Kwa nyongeza neno hapiza ni kumlani mtu...! Kuachiwa ladhi mbaya...
 
Kwa nyongeza neno hapiza ni kumlani mtu...! Kuachiwa ladhi mbaya...

Si kuachiwa "ladhi" bali ni kuachiwa "radhi". Imebidi kumsahihisha msahihishaji!

Inashangaza jinsi Watanzania wengi wasivyoweza kutofautisha kati ya "r" na "l". What is the root cause of that?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom