Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

Zamani nilikua naona wanaoacha viwanja muda mrefu hawajengi kama wajinga flani hivi.

ila nimekuja gundua kuna maana kubwa sana ya kuacha kiherehere cha kuanza ujenzi kisa una pesa na unaweza.

Kile kiwanja nilinunua enzi ni pori la maana tu,haraka haraka kimbilia jenga..

Tangu zamani nilishasema sitowahi jenga uswahilini, ila sikua najua wanaojenga uswahili hawakuwahi waza kama patakuja kuwa uswahilini.

Baada ya ujenzi miaka kadhaa mbele ule mtaa haukua na tofauti na tandale, ule uswahili,vile vijumba vilivyokua vikichipuka kama uyoga nikajikuta nimewekwa mtu kati, nmezungukwa na vijumba vingiiiiiii...

Nikaona hapa Usintanie,Madalali kazi yao nini? Nikapauza kama palivyo.

Hela yote nimenunulia kiwanja sehemu nyingine, Sijengi ng'o mpaka nihakikishe ule mtaa ni wanaojielewa.

Ntapanga hivi hivi ila siwezi jenga mtaa ambao sina uhakika nawataokuja.

Hii mambo ya kuharakisha kujenga sehemu nyumba ya maana ndio unaweza jikuta unajenga mtaa kama kwa mtogole...

Baadae watoto wanakuuliza baba ilikuaje ukaja kujenga huu mtaa... Unakosa majibu.

Unatakiw ununue sehem ambay imekatw viwanja vya sqr 500 au 700 mpaka 1000 sehem amabyo vipo ving au labd vi3 au vi4 we unanua kimoja wapo hapo huwez kupata mswahili apo maan bei itakuw kubwa . Kw mfano Mimi KIGAMBONI Dege nimenunua square meter 700 katikat pembn Yang wakaja washia tupu mmoj mtumishi WA Bandar anashusha mjeng WA maan
 
Tupo pamoja hapo dege, soon naanza kushusha contemporary yangu
 
Mimi nimejenga nipo karibu kuhamia ila mbele yangu kuna mtu na sijui atakuja kujenga nin lakini barabara ya kuingia kwangu ipo nilinunua hatua kadhaa ila nimepata wazo la kupageuza kuwa hostel ya wanachuo maana nipo karibu na chuo na soko la vyumba ni kubwa hali kadhalika nina mawazo pia ya kupageuza lodge ili nikajenge pengine maana nimeshanunua kiwanja kingine kimepimwa fresh na vinauzwa na halmashauri
 
Hiki ndicho fundi amenifanyia. Kaweka papi za fito mbalimbali na matokeo yake bati zinaonekana kama hazijapigiliwa misumali hasa pale zinapoungana.

Jamani kama kuna mtaalam humu wa kuzibananisha zikae sawa ani PM
 
Attachments

  • IMG_20231118_080237.jpg
    IMG_20231118_080237.jpg
    35.3 KB · Views: 29
Nilivyouziwa sikua nagari, nikajenga nikamaliza na njia ya kuingilia na kutokea ilikuwepo kwasababu wakati wa ujenzi gari ya vifaa ilikuwa inaingia Hadi site.

Sasa nimehamia nikakaa miezi 6 nikanunua gari Alieniuzia tukaanza mgogoro mara apande miti sehemu ninayo pita mara aanzishe biashara ya tofari sehemu ninayo pita kiasi cha kubakisha kichochoro cha wapita kwa miguu.

Nikampeleka kwa mjumbe akaambiwa angoe miti yake akingoa siku chache ana panda tena, nikaona Bora niuze nikajenga sehemU salama yenye majirani wanaojielewa sio yule chawivu anaetamani kila mtu atembee kwamguu.
ningekua mimi angekubali show haki ya nani
 
Kuamini mafundi nikiambiwa cement imeisha napiga simu tu inapelekwa bila kufatilia. Kuna siku fundi anapiga simu kuwa wamesimama kazi kwa kuwa cement imeisha inabidi ipelekwe haraka.

Ikabidi niende mwenyewe kuangalia kazi imefikiaje hadi cement kuisha hivo, nilivyofika mafundi wakastuka sana maana hawakutarajia kuniona kwa wakati huo. Ikawa kila ninapoingia kukagua jamaa kama ananizuga ili niache nimsikilize yeye. Nikahisi kitu nikaongeza umakini kuangalia chumba hadi chumba.

Bwana weee! Si nikakuta kuna mifuko 9 ya cement haijatumika wameificha kwenye chumba chooni. Asee jamaa alibabaika sana akakosa la kusema.

Kheri ulijiongeza
 
Kupeana kazi za ufundi kwa kujuana kulinidharimu, ujenzi wa nyumba yangu ya kwanza nilinunua kiwanja cha sq 400, nikampa kazi mshkaji wangu ya kuchora ramani tukaenda site kuchukua vipimo pamoja na kuangalia geographia ya eneo, nilipata ramani ndani ya muda tena nzuri sana. Ishu ikaja kwenye msingi, nilipewa fundi na wife ambaye alikuwa amepanga kwao. Fundi alifanya makosa kwenye vipimo vya nyumba, kwanza sebule ilikuwa ndogo kulingana na vipimo halisi, pili nyumba ilitoka imepinda. Yule Mzee nikamnyang'anya kazi nikatafuta fundi mwingine ikabidi niingie gharama ya kuweka zege upande mmoja wa msingi ili nyumba ikae sawa. Ila nyumba haikuwa na uhalisia wa vipimo kati ya ramani na nyumba halisi
 
Kwamba huyo professional ndo anajenga?

Hujui hao huwa kazi yao kushika makaratasi tu?
Wasichokielewa wengi ni kwamba hao wataalamu mnaowasema hawana utaalamu wowote kuwazidi mafundi wapo mafundi wameenda shule wamepoteza miaka 5 au 3 utamuambia nini na yuko practical zaidi mainjinia wengi hawawezi na hawajui kazi ni makaratasi tu injinia mwenyewe anamtegemea fundi kufanya hesabu na ujenzi kiufupi ni amubane fundi yeye afanikiwe

Msiwadharau mafundi ila Mara nyng maboss ndio wanaosababisha nyumba kujengwa chini ya kiwango kumminya fundi unatoa hela ya material labda million 14 halafu hela ya ufundi laki 8 au million upaua nyumba kwa bati la kigae/versatile halafu hela kiduchu kwa ushauri wa paa nitafute inbox kukufanyia kazi ni ngumu kwani nabanwa Sana na muajiri Wang muda sipati na sipendi kuacha mafundi saiti wakaharibu kazi ya mteja
 
Back
Top Bottom